Majeruhi wa Liliondo Tanzania walia na usalama wao, baadhi wakidaiwa kukimbilia Kenya kwa matibabu
Iliyochapishwa
Baadhi ya majeruhi katika makabiliano baina ya jeshi la Polisi nchini Tanzania na jamii ya wamaasai waishio katika eneo la Loliondo Kaskazini mwa Tanzania wamekimbilia nchini Kenya kupatiwa matibabu katika zahanati na hospitali za karibu
Chanzo cha mgogoro huo ni zoezi linaloendelea la uwekaji alama kwenye eneo la kilomita za mraba 1500 kati ya 4000 za eneo hilo la pori tengefu
Serikali imeeleza nia yake ya kuendelea na zoezi hilo kutokana na umuhimu wake kwa ikolojia na uhifadhi wa Wanyama pori nchini Tanzania
Eagan Salla ametuandalia taarifa ifuatayo
