LHRC yataka uwazi zaidi katika suala la Loliondo

Maelezo ya sauti, LHRC yataka uwazi zaidi katika suala la Loliondo
Iliyochapishwa

Kituo cha Sheria na haki za binadamu nchini Tanzania, LHRC kinataka uwazi zaidi katika mzozo wa Loliondo kaskazini mwa nchi hiyo, uliosababisha kifo cha polisi mmoja mwishoni mwa wiki.

Katika taarifa yake, iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho , Fulgence Massawe, mbali na kulaani matukio ya ukiukwaji ya haki za binadamu kwenye zoezi la kuweka mipaka Loliondo, hatua za kisheria zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya waliotoa uhai wa polisi huyo.

Jana msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, alisisitiza hali ni shwari Loliondo, na kilichotokea mpaka kusababisha mauaji ni wananchi kuwafuata Polisi na si Polisi kuwafuata wananchi, wakati wa zoezi la kuweka mpaka, kilometa 8, kutoka kwenye makazi ya watu.

Mwandisi wa BBC, Yusuph Mazimu amezungumza na Massawe na kwanz alimuuliza kama watetezi wa binadamu wameona nini Loliondo kiasi cha kuja na tamko la kulaani kinachoendelea.