Urusi na Ukraine : Kiongozi wa Urusi anavyojifananisha na Mfalme wa karne ya 18 Peter the Great

Chanzo cha picha, Universal History Archive/Getty Images
Mapenzi ya Vladimir Putin kwa Peter the Great yanafahamika vyema, lakini kwa sasa anaonekana binafsi ana mawazo ya "Ukuu"-mwenyewe
Amejifananisha wazi binafsi na Mfalme wa Urusi, akifananisha uvamizi wa Urusi nchini Ukraine unaoendelea sasa na vita vya kupanua maeno ya Urusi vya Mfarme Peter yapata karne tatu zilizopita, na kuelezea kauli yake kwamba vita vyake ni vya kukomboa ardhi iliyonyakuliwa.
Matamanio ya Bw Putin ya iujenzi wa himaya yanaonyesha uovu kwa Ukraine na yamewakera majirani wake , pamoja na Estonia, ambayo imezitaja kauli zake kama "zisizokubalika kabisa."
Rais wa Urusi alikuwa akifanya mazungumzo na wanasayansi vijana na wajasiliamali alipoitoa kauli hiyo. Kabla ya kuzungumza na wataalamu wa masuala ya teknolojia ya mawasiliano na watengenezaji wa teknolojia, alizungumzia kuhusu siasa na mamlaka: mapambano mapya anayoyaona kwa ajili ya kutawala siasa za eneo la kijiografia. Katika hilo aliieleza hadhira iliyochaguliwa kwamba Peter ni mtu ambaye amekuwa akiiga mfano wake.
"Unaweza kufikiria alikuwa akipigana na Sweden, kuchukua ardhi zao," Bw Putin alisema, akizungumzia Vita vya Kaskazini ambavyo Mfalme Peter alivianzisha katika karne ya 18 alipokuwa akianzisha himaya mpya ya Urusi .
" Lakini hakunyakua lolote ; alichukua kilichokuwa chake!"alisema, akidai Slavs walikuwa wameishi katika eneo hilo kwa karne kadhaa.
"Inaonekana imetupata sisi pia , kujirejeshea kilicho chetu na kukiimarisha," alisema Bw Putin, katika kauli ambayo ilimuacha kila mtu akitambua kuwa alikuwa anamaanisha Ukraine na malengo yake pale.
Utawala wa Peter alisema Putin ulikuwa uthibitisho kwamba kupanuliwa kwa Urusi kumeiimarisha.

Chanzo cha picha, EPA
Bw Putin alizungumzia kuhusu Peter the Great kama mtu wa mfano wakati wa mkutano
Bw Putin amekuwa akitumia hali ya nyuma ya Urusi sana hivi karibuni, na kuifananisha mara kwa mara na malengo yake ya sasa. Miezi kadhaa kabla ya kuishambulia Ukraine , aliandika Makala kubwa ambamo alidai kuwa nchi yake na haki ya kihistoria ya kuwepo.
Wakati Urusi ilipovamia majirani wake tarehe 24 Februari , Putin alitoa madai ya Uongo kuwa ilikuwa ni "operesheni maalum" ambayo ilikuwa ifanyike katika jimbo la Donbas kwa lengo ya "kuondoa Unazi" nchini Ukraine na kupunguza tisho kwa Urusi.
Lakini hata alipokuwa akitamka matamshi hayo, vikosi vyake vilikuwa vikielekea katika mji mkuu Kyiv na kushambulia kwa mabomu ya ardhini maeneo ya mbali magharibi mwa Ukraine . Siku 100 baadaye, moja ya tano ya maeneo ya Ukraine yanadhibitiwa na jeshi la Urusi, huku utawala uliowekwa na Urusi ukizungumzia kuhusu kuendeshwa kwa kura ya maoni juu ya kujiunga na Urusi.
Na sasa Putin anahisi kuwa mwenye ujasiri wa kutosha kukiri juu ya "operesheni" kwamba ni uvamizi halisi.
Anaonekana kukiri kuwa nchini za Magharibi zitakubali kwamba vikosi vyake vinapigana kupata ardhi.
Unaweza pia kutazama:













