Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi na Ukraine: Ushindi kwa Ukraine au kushindwa kwa Putin? Jinsi nchi za Magharibi zinavyoelezea kuhusu malengo ya vita
Matarajio ya vita vya muda mrefu yamefichua mgawanyiko miongoni mwa viongozi wa Ulaya na wataalamu. Wanaungana katika kuiunga mkono Ukraine, lakini wanatofautiana kuhusu malengo yao: Kuisaidia Ukraine kushinda-au watafute makubaliano ya mapema, hata kwa gharama ya makubaliano na Urusi.
Kwa kipindi cha wiki chache zilizopita, Urusi imepeleka vikosi vingi matia maeneo ya vita nchini Ukraine na imekuwa ikionga mbele kuelekea Donbass, ikitishia kuzingira makundi makubwa ya wanajeshi wa Ukraine katikamaeneo ya Severodonetsk na Lysichansk.
Kulingana na maafisa wa Ukraine, katika baadhi ya maeneo, vikosi vya Urusi vimeweza kuwa na vikosi vingi.
Lakini la muhimu hasa ni mapigano katika ambapo makombora na silaha nyingine nzito zinatumika. Hatahivyo washirika wa Kyiv wanachelewa kutoa silaha za kisasa kwa kuogopa jibu la Kremrin, na kuna kutoelewana miongoni mwa umma kuhusu malengo na vita.
Kuna miito katika Ulaya na Marekani inayotaka kufikiwa haraka kwa mkataba, hata kama itamaanisha kufikiwa kwa makubaliano ya kieneo kutoka Ukraine. Kambi hii katika katika umma inapinga wale wanaotaka ushindi wa Ukaraine na ukombozi wa maeneo yake.
Katika Kyiv, miito ya kutaka mazungumzo na Moscow haraka iwezekanavyo ilijibiwa kwa hasira, na wakati mwingine kwa hata lugha chafu. Maafisa wa Ukraine wanasema kwamba kumaliza vita haraka iwezekanavyo, Marekani na Ulaya lazima waiwekee vikwazo Moscow na kuharakisha usambazaji wa silaha kwa Ukraine, na mwanzo yapelekwe mifumo ya kufyatua makombora mengi kwa wakati mmoja.
Kushindwa kwa Putin au ushindi wa Ukraine?
Maafisa wa Marekani, Uingereza, Uingereza, Poland na wajumbe wa Muungano wa Ulaya wanaunga mkono Ukraine katika juhudi za kuikomboa ardhi yake, halafu katika Ulaya mashariki wanazungumzia kuhusu kumalizika kwa vita.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na waziri mkuu wa Italia Mario Draghi wamekwishazungumzia kuunga mkono mkataba wa mapema na Urusi. Viongozi hawa wamesalia kuwa na msimamo kwamba mataifa ya Magharibi mwanzoni kabisa mwa vita- walilaani uvamizi wa Urusi na walikuwa na hamu ya kuiadhibu Urusi kwa vikwazo vya kiuchum.i
Hatahivyo, haijafahamika bado, ni mifumo mingapi ya aina hiyo itahamishiwa katika siku za hivi karibuni zijazo, limeandika jarida la Wall Street, , ambalo pia lilibaini kuhusu mipango ya usamabazaji wa makombora ya MLRS kwa Ukraine.
London na Warsaw wanashirikiana na Kyiv katika kudai silaha mpya. Rais wa Poland Andrzej Duda hata aliishutumu Ujerumani kwa kuchelewa kufanya hivyo.
Bunge la Ujerumani Bundestag lilipigia kura kusambazwa kwa silaha nzito kwa Ukrainbe mwishoni mwa mwezi Aprili. Wakati huo Berlin iliahidi kuhamisha mifumo ya kuzuia makombora ya anga aina ya 50 Gepard -lakini mwezi mmoja baadaye ilithibitisha kuwa atazituma katika mwezi wa Julai.
"Kujitolea kwa muda mrefu"
Uongozi wa Urusi kwa sasa unazungumzia uwezekano wavita vya muda mrefu. Katika mwanzoni mwa uvamizi, mkuu wa jeshi la ulinzi la Urusi -National Guard, Viktor Zolotov, ambaye wanajeshi anaowaongoza wanapigana Ukraine, alikiri kuwa operesheni maalumu "haitakuwa haraka kama ambavyo tungependa iwe."
Lakini sasa Urusi inasema sema hakuna haja ya kuharakisha vita. "Hatukimbizani na nyakati. Unazi lazima umalizwe kwa 100%, au utapandisha tena kicha chake katika miaka michache ijayo, na kuwa hata kwa katika mfumo mbaya zaidi, "alisema Nikolai Patrushev, mkuu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Urusi.
Putin bado anajaribu kuteka maeneo mapya katika Ukraine katika Ukraine na anaendelea n ani sharti la makubaliano ambalo Kyiv haiwezi kulikubali, anasema Mwanahistoria wa kijeshi wa Uingereza Sir Lawrence Friedman.
"Sasa ni busara kutarajia kwamba hii sio dharura ya muda mfupi, bali ni vita vya muda mrefu kwa nchi ambazo zinaiunga mkono Ukraine; kwamba hakuna diplomasia rahisi, na kwamba Ukraine itaendelea kupigana hadi itakaporejesha tena maeneo yake ," aliandika Friedman.
Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine