Vita ya Ukraine: Fahamu eneo analoishi Rais wa Ukraine

w
Iliyochapishwa

Tangu vita hivi kuanza, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky hajaondoka katika mji mkuu wa nchi hiyo Kyviv.

Mbali na kuwindwa na vikosi vya Urusi na kupewa kifadhi maeneo mbalimbali lakini aliapa kutoondoka Ukraine.

Waandishi wa BBC walifika hadi eneo analokaa kwa sasa. Na wanasimulia jinsi jengo hilo lilivyo na hali ya ulinzi.

Askari katika kituo cha ukaguzi walichunguza pasipoti zetu, kisha wakatupungia mkono. Tulikuwa ndani ya uwanja wa jengo lililokuwa likitumika kama makao makuu ya upinzani dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Waya wenye silaha zenye ncha kali umezunguka ukuta wa eneo hilo. Wanajeshi wenye silaha nyingi walikuwa kila mahali - mtu ambaye nilikuwa karibu kukutana naye ni mtu anayewindwa kwa hali na mali.

Kremlin ingependa kuona Volodymyr Zelensky akifa na serikali yake ikibadilishwa na kuwekwa kiongozi ambaye atakua anasikiliza matakwa ya Moscow. Lakini kwa muda wa siku 50 za vita hivi, upinzani wa Kiukreni umeshangaza ulimwengu.

Tulipitisha vifaa vyetu kupitia seti mbili za vigunduzi vya chuma na kuingizwa ndani. Kisha tukapita kwenye korido ndefu, ilikua imezingirwa na mifuko ya michanga ambayo huzuia risasi kupita. Shimo kidogo liliachwa kwenye rundo karibu na juu, ambalo mdomo wa bunduki ya kushambulia unaweza kutoshea.

Msaidizi wa Rais alituongoza hadi kwenye mlango uliokuwa na sahani ya shaba juu yake, ulikua na maneno yalisomeka chumba maalum kwa lugha ya Kiukreni.

Ndani, chumba hicho kinaonekana cha kisasa.

w
Maelezo ya picha, BBC ilipata nafasi ya kufanya mahojiano maalum na Zelensky

Lakini kulikuwa na tatizo. Kuhoji watu walioketi kwenye viti vya magurudumu inaweza kuwa ngumu, kwasababu mara nyingi hugeuka na kiti wakati wa mahojiano.

Kwa hiyo tukamwomba msaidizi wa rais viti visivyo na magurudumu. "Umm," akasema, "nitaangalia."

Alitoka katika Chumba hichi na kurudi akiwa na viti viwili vya kizamani, vyote vilivyokuwa vya rangi ya kahawia na viti vyenye muundo. "Hiyo itasaidia," akasema. Lakini niliweza kumwona mkuu wa wafanyakazi wa rais akikunja midomo.

"Hapana, hiyo haitafanya," alisema. "Kiti kinaonekana kuwa cha kizamani sana katika chumba hiki cha kompyuta za kisasa. Tunajaribu kutayarisha picha ya kisasa hapa." Na pamoja na hayo, viti viwili vya kisasa zaidi vilitolewa - bila magurudumu.

w

Majadiliano juu ya viti yalionyesha mengi kwangu kuhusu Ukraine ya kisasa. Tangu mwisho wa Vita Baridi, idadi kubwa ya vijana imeegemea Magharibi kwa ushawishi wake. Ndege za bei nafuu za Ryanair kwenda Ulaya Magharibi zilifungua ushirikiano zaidi.

Utawala huu ulitaka tujue kwamba hawakuwa na mlolongo mrefu wa masharti, walikua tofauti na tayari kuzungumza.

Kisha nikasikia hatua kadhaa zikishuka kwenye ukumbi. Askari wawili waliingia ndani ya chumba hicho na nyuma yao alikuwepo raisi.

Wakati tunasalimia, msaidizi alimpa simu. Juu yake kulikuwa na meseji kutoka Ufaransa. "Ni Emmanuel?" aliuliza msaidizi? "Ndiyo," jibu lilikuja.

"Tuna uhusiano mzuri na ananipigia simu kila wakati," rais ananiambia. "Unajali nimpigie simu haraka?"

"Hapana sijali," nikamjibu, nikishangaa kwamba aliniuliza ikiwa anaweza kumpigia simu rais wa Ufaransa mara moja au amjaribu baadaye.

Lakini hiyo ni sehemu ya kipimo cha Volodymyr Zelensky, urafiki na haiba ambayo huja kwa kawaida.

Walakini, kulikuwa na nyakati katika saa iliyofuata ambapo niliweza kusema kwamba alikuwa na hasira na kukasirika: alipokumbuka kutembelea mji wa Bucha, takriban kilomita 25 (maili 16) kaskazini-magharibi mwa Kyiv ya kati, ambayo majeshi ya Urusi yalikuwa yamekatia kwa wiki kadhaa.

Baada Urusi kujiondoa, kaburi la pamoja liligunduliwa karibu na kanisa na kulikuwa na miili imelala barabarani.

Nilimuuliza kuwa je anaweza kukaa meza moja na Urusi?

"Dirisha la fursa ya mazungumzo linapungua," alijibu, akionesha ukatili huko Bucha na Borodyanka.

Bwana Zelensky, bila shaka, ni mcheshi na mwigizaji wa zamani. Lakini wakati wa saa niliyokuwa naye, nilimwona mtu akiwa amechoka kiakili na mwenye maumivu makali kuhusu jinsi watu wake wanavyotendewa.

Mtu ambaye amefananishwa na aliyekua waziri mkuu wa Uingereza Churchill na ambaye wengi watamkumbuka kwa uongozi wake katika siku za giza za vita.

Unaweza pia kusoma