Vita vya Ukraine: Je, mzozo huo unagharimu uchumi wa Urusi kwa kiasi gani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Vita vinaweza kushindwa kudhibitiwa ikiwa mambo hayatoenda kama yalivyopangwa
Ijapokuwa ni vigumu kujua kile Vladimir Putin alichokuwa anafikiria wakati alipoongoza Urusi kuvamia Ukraine Februari 24, wengi wanaamini kwamba alikuwa akitarajia ushindi wa haraka katika muda wa siku chache.
Ndani ya mwezi mmoja, mzozo huo umekua na kuwa vita vya uhasama, ambapo Urusi inatumia mbinu za kikatili kupunguza upinzani wa Ukraine, kulingana na wachambuzi wa kijeshi wa Marekani Benjamin Johnson, Tyson Wetzel na J.B. Barranco.
Wakiandikia Baraza la Atlantiki, walisema: "Tunatathmini kwamba kuna uwezekano Urusi itaingia katika vita vya mvutano, ikikabiliwa na njaa Ukrainia ya vifaa, kuzuia ufikiaji wa Bahari Nyeusi, na hatimaye kusababisha njaa kwani wakulima wa Ukraine hawawezi kutunza mavuno yao. "
Lakini vita vya muda mrefu pia vitakuja kwa bei kubwa kwa Urusi. Swali ni: kiasi gani?
'Gharama ya biashara'

Chanzo cha picha, Getty Images
Ed Arnold, Mtafiti Mshiriki wa Usalama wa Ulaya katika taasisi ya Uingereza ya Huduma za Kifalme (RUSI), ameambia BBC kwamba "kuendeleza operesheni za kijeshi ni biashara ya gharama kubwa, haswa wakati wanajeshi wako mbali na kambi kuu."
"Lazima uhifadhi kiasi kikubwa cha risasi na mafuta ili kuhamasisha mashine ya vita na chakula cha kuwalisha wanajeshi."
Kuna ushahidi mwingi wa kuashiria matatizo ya vifaa vya Urusi katika vita na Ukraine - dhahiri zaidi, kuongezeka kwa magari ya jeshi la Urusi yaliyotelekezwa uwanjani baada ya kuharibika.
"Hawakuwa tayari kwa sababu walidhani operesheni hii ingeendelea kwa siku kadhaa," Arnold anasema.

Chanzo cha picha, Getty Images
James Stavridis, amiri mstaafu wa Jeshi la Wanamaji la Marekani na mkuu wa Chuo cha Sheria na Diplomasia cha The Fletcher katika Chuo Kikuu cha Tufts, anasema gharama zinaongezeka huku vyanzo vya fedha vya Urusi vikipungua.
Ingawa nchi inashikilia moja ya akiba kubwa zaidi ya fedha za kigeni duniani (karibu $600bn), kiasi kikubwa cha fedha hizi sasa kimefungwa katika benki za Magharibi kwa sababu ya vikwazo vya kiuchumi.
Vita inagharimu Urusi kiasi gani?
Kulinganana Kituo cha Kufufua Uchumi, kundi la wanauchumi na washauri wa serikali ya Ukraine, siku 23 za kwanza za uvamizi huo zimeigharimu Urusi angalau $19.9bn katika matumizi ya moja kwa moja ya kijeshi.
Wanakadiria kuwa Kremlin imepoteza $9bn katika vifaa vya kijeshi vilivyoharibiwa.
Kiasi hiki cha fidha lazima kiongerezwa gharama ya kurusha makombora ya meli na upotevu wa Pato jumla la Taifa (GDP) katika kipindi cha miaka 40 ijayo (kwa kuzingatia hasara ya kupoteza wafanyakazi).

Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo Machi 19 1Ukraine ilidai kuwa zaidi ya wanajeshi 14,400 wa Urusiwameuawa katika vita kufikia wakati huo.
Jumla ya gharama pia itahitaji kujumuisha gharama za uokoaji, matibabu ya askari waliojeruhiwa, matumizi ya risasi, mafuta, vipuri, chakula cha wanajeshi, na kadhalika.
Makadirio haya yahajathibitishwa kikamilifu. Wataalamu walioshauriwa na BBC walikuwa waangalifu kutokana na hali ya kutokuwa na uhakika, ingawa wanakubali kwamba kuendesha mashine ya vita ni ghali sana.
Urusi itaishiwa lini na pesa?

Chanzo cha picha, Getty Images
Inategemea jinsi vikwazo vya kiuchumi vya Magharibi vitakavyoendelea kuwa.
Kimsingi, inategemea pia ikiwa nchi za Ulaya zinaweza kumudu kupiga marufuku uagizaji wa gesi ya Urusi. Hii ni changamoto kubwa kwani Urusi inasambaza takriban 40% ya uagizaji wa gesi asilia wa EU.
Haijulikani pia ikiwa kutengwa kwa benki kadhaa za Urusi kutoka kwa mfumo wa malipo wa SWIFT, unaowezesha uhamishaji wa pesa za kimataifa, hatimaye kutapanuliwa, na kumwacha Putin bila njia mbadala ya kupokea malipo ya fedha za kigeni.
Hatimaye, jinsi rasilimali za Urusi zinaweza kuenea pia inategemea washirika wake, na moja hasa.
Nafasi ya China

Chanzo cha picha, Getty Images
Wataalamu wamesisitiza uwezo wa China kuingilia kati mzozo huo lakini hakuna maafikiano yaliyofikiwa kuhusu ni jukumu gani inakusudia kuchukua katika vita hivyo.
China imeelezea wasiwasi wake kuhusu vita hivyo lakini imeendelea kuichukulia kama "oparesheni ya kijeshi"
Na naibu waziri wa mambo ya kigeni Le Yucheng Machi 19 alisema kwamba vikwazo vya magharibi "vinaendelea kughadhabisha".
Aliongeza kuwa hatua hizo ni za upande mmoja na zinawanyima raia wa Urusi mali ya kigeni "bila sababu".
"Historia imethibitisha mara kwa mara kwamba vikwazo haviwezi kutatua matatizo. Vikwazo vitadhuru tu watu wa kawaida, kuathiri mfumo wa kiuchumi na kifedha ... na kuathiri zaidi uchumi wa dunia," Le alisema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Renaud Foucart, senior lecturer at Lancaster University in the UK, argues that China could prove vital for Russia, given the latter's "dire" long-term prospects.
"Ikiwa vikwazo vitadumishwa, Urusi itatengwa na washirika wake wakuu wa biashara, isipokuwa Uchina na Belarusi," Foucart anasema.
Maxim Mironov, profesa katika Shule ya Biashara ya IE, nchini Uhispania, anasema utegemezi huu hauwezi kutiwa chumvi.
"China itanunua rasilimali kutoka Urusi kwa bei ya chini sana na kuuza bidhaa kwa Urusi kwa bei ya juu," aliambia BBC.
"China itaichukulia Urusi kama koloni lake. China itakuwa mshindi pekee katika vita hivi."
Uchumi kusambaratika

Chanzo cha picha, Getty Images
Moscow inasisitiza kwamba vikwazo vya Magharibi haviwezi kutenga nchi kubwa kama Urusi.
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov mnamo Machi 5 aliwaambia waandishi wa habari: "Dunia ni kubwa sana kwa Uropa na Amerika kutenganisha nchi fulani, haswa jimbo kubwa kama Urusi."
Lakini sarafu Urusi rouble, imeporomoka, soko la hisa limebaki kufungwa kwa kiasi kikubwa, mfumuko wa bei tayari umeshamiri na viwango vya riba vimeongezeka maradufu. Zaidi ya makampuni 400 ya kigeni yameondoka nchini.
Baadhi ya makadirio yanaonyesha kuwa uchumi unaweza kurudisha nyuma kwa 7% hadi 15% mwaka huu na kuna hofu kwamba serikali ya Urusi inaweza kutolipa deni lake.
"Sekta ya Urusi inasimama," anasema Mironov.

Chanzo cha picha, Getty Images
Foucart anasema mambo mawili yataamua kwa kiasi kikubwa ikiwa gharama ya vita itakuwa kubwa sana kwa Putin katika wiki zijazo.
Ya kwanza ni ikiwa tasnia ya kijeshi na ulinzi ya Urusi inaweza kuendelea bila uagizaji wa kiteknolojia kutoka Magharibi.
Na ya pili, ikiwa athari za vikwazo zitatosha kubadilisha maoni ya umma ya ndani dhidi ya mtu huko Kremlin.
Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine












