China Eastern: Ndege iliyokuwa na watu 132 yaanguka katika milima ya Guangxi

Rescuers at the site

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Televisheni ta kitaifa ilinyesha waokoaji wakikimbilia eneo la ajali
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Ndege ya abiria ya China iliyokuwa na watu 132 imeanguka katika eneo lenye msitu kusini mwa China.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737 ilikuwa safarini kutoka Kunming kuelekea Guangzhou wakati ilipoanguka katika mkoa wa Guangxi na kushika moto.

Inahofia hakuna manusura, lakini idadi ya waliojeruhiwa au kilichosababisha ajali hiyo bado haijulikani.

Mashirika ya ndege ya China kwa ujumla yana rekodi nzuri ya usalama: ajali kuu ya mwisho ilitokea miaka 12 iliyopita.

Kifaa cha kufuatilia safari ya ndege kinaashiria ndege hiyo ilipoteza mwelekeo wa kwenda juu na kuanguka chini.

Zaidi ya wahudumu 600 wa dharura wanasemekana kuwa katika eneo la ajali. Wazima moto walifika eneo la tukio kwanza na kufanikiwa kuzima moto katika vilima uliosababishwa na ajali hiyo.

Picha zilizopigwa na wanakijiji wa eneo hilo na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ya China - na vituo vya habari vya serikali - zilionyesha moto na moshi kutoka kwa ajali hiyo, na vifusi vya ndege chini.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Viwango vya usalama wa anga na usafiri wa anga nchini China vimeimarika sana katika miongo ya hivi karibuni kufuatia mfululizo wa ajali katika miaka ya 1990 na ajali kama hizi sasa ni nadra sana.

Mara ya mwisho ajali kubwa ya ndege kutokea nchini humo ilikuwa Agosti 2010, wakati ndege kutoka Harbin ilipoanguka kaskazini-mashariki mwa Yichun kutokana na hali mbaya ya hewa, na kuua watu 42.

China imetoa nambari ya simu ya dharura kwa watu wanaotafuta habari kuhusu wale waliokuwa kwenye ndege. Imeweka nembo ya kijivu kwenye akaunti yake ya Weibo na pia kubadilisha tovuti yake kuwa nyeusi na nyeupe kama ishara ya maombolezo.

Ndege hiyo inalomilikiwa na serikali ni mojawapo ya mashirika matatu makubwa ya ndege ya China, ikiwa ni pamoja China Southern na Air China.

Mamlaka ya Usafiri wa anga nchini China imesema pia umetuma wachunguzi wake kwenye eneo la tukio.

Ndege hiyo yenye nambari ya usajili MU5735 iliondoka Kunming saa 13:11 saa za huko (05:11 GMT) na ilitarajiwa kufika Guangzhou saa 15:05.

Picha ya maktaba ya China Eastern Airlines Boeing 737-800

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Picha ya maktaba ya China Eastern Airlines Boeing 737-800

Maeneo ya ufuatiliaji wa ndege yanaripoti kuwa ndege hiyo ilikuwa angani kwa zaidi ya saa moja, na ilikuwa inakaribia mwisho wa safari yake ilipoanguka huko Wuzhou, eneo lenye milima, lenye hali ya hewa mchanganyiko wakati huu wa mwaka China inapoingia katika msimu wake wa mafuriko ya kila mwaka.

Ijapokuwa hali ya hewa ilikuwa ya mawingu mwonekano wake uliripotiwa kuwa mzuri wakati wa ajali hiyo.

Ndege hiyo ilishuka maelfu ya mita ndani ya dakika tatu, data ya kufuatilia ndege ilionyesha.

map of flight path