Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Waliowauwa wataalamu wa Umoja wa Mataifa wahukumiwa kifo DRC
Makumi ya wanamgambo wamehukumiwa kifo katika Jamuhuri ya Kidenokrasi ya Kongo kwa kuhusika katika mauaji ya wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa.
Wataalamu hao Zaida Catalan mwenye uraia wa Sweden na Chile na Mmarekani Michael Sharp walitekwa na kuuawa katika jimbo la Kasai mwaka 2017.
Walikuwa wakichunguza madai ya kuwepo kwa makaburi ya pamoja baada ya kuibuka kwa mapigano baina ya vikosi vya serikali na kikundi cha wanamgambo.
Mkalimani wao, Betu Tshintela,pia aliuawa. Miili yao ilipatikana siku 16 baada ya kutekwa nyara. Catalan alikuwa amekatwa kichwa.
Umoja wa Mataifa ulishitushwa na mauaji hayo na wakati huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema kuwa Umoja huo "ungefanya kila liwezekanalo kuhakikisha haki itendeka".
Unaweza pia kusoma:
Mamia ya watu walikufa katika mzozo katika jimbo la Kasai uliomalizika mwaka 2017. Zaidi ya watu milioni moja walisambaratishwa na mapigano, ambayo yalianza baada ya kiongozi wa kikabila, Kamwina Sapu, kuuawa Agosti 2016.
Hukumu zilizowatia hatiani washitakiwa zilitolewa na mahakama ya kijeshi katika mwisho wa kesi iliyodumu kwa miaka minne.
Kati ya makumi ya washitakiwa, 51, wakiwa ni karibu wanamgambo, walihukumiwa kifo. Lakini kutokana na kwamba Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo imekwisha tangaza usitishwaji wautekelezwaji wa hukumu ya kifo, hukumu hizi huenda zikaishia kuwa kifungo cha maisha gerezani.
Walikabiliwa na mashitaka mbali mbali, kuanzia ugaidi na mauaji na kitendo cha uhalifu wa kivita kwa kukata viungo, limeripoti shirika la habari la AFP.
Kanali Jean de Dieu Mambweni, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela, alihukumiwa kwa kukiuka maagizo. Wengine wawili- mwandishi wa habari na afisa wa polisi waliachiliwa huru.
Zaidi ya vikao 100 vya mahakama vilikaa tangu kesi hiyo ilipoanza kusikizwa Juni 15, 2017 dhidi ya washukiwa waliotuhumiwa kwa mauaji ya wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa.