Boeing na Airbus zaionya Marekani kuhusu usalama wa 5G

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakuu wa mashirika mawili makubwa ya kutengeneza ndege duniani wametoa wito kwa serikali ya Marekani kusitisha kusambaza huduma mpya za simu za 5G.
Wakuu hao kutoka kampuni mbili kubwa zaidi za kutengeneza ndege duniani wametoa wito kwa serikali ya Marekani kuchelewesha kusambaza huduma mpya za simu za 5G.
Katika barua, wakuu watendaji wa Boeing na Airbus walionya kuwa teknolojia hiyo inaweza "kuwa na athari mbaya kwa sekta ya usafiri wa ngani'
Kumekuwa na wasiwasi kwamba huduma ya C-Band spectrum na 5G wireless inaweza kuingiliana na vifaa vya kielektroniki vya ndege.
Mashirika makubwa ya mawasiliano ya simu nchini Marekani AT&T na Verizon yanatarajiwa kuzindua huduma za 5G tarehe 5 Januari.
"Muingiliano wa 5G unaweza kuathiri vibaya uwezo wa ndege kufanya kazi kwa usalama," walisema wakuu wa Boeing na Airbus Amerika Kusini, Dave Calhoun na Jeffrey Knittel, katika barua ya pamoja kwa Waziri wa Usafiri wa Marekani Pete Buttigieg.
Barua hiyo ilinukuu utafiti wa shirika la biashara la Airlines for America ambao uligundua kuwa ikiwa sheria za Shirika la Usafiri wa Anga (FAA) 5G zingetumika mnamo 2019, takriban ndege 345,000 za abiria na safari 5,400 za mizigo zingekabiliwa na ucheleweshaji, ubadilishaji au kughairiwa.
Sekta ya usafiri wa anga na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA) zimeibua wasiwasi kuhusu uwezekano wa 5G kuvuruga vifaa nyeti vya ndege kama mita za urefu wa redio.
"Airbus na Boeing zimekuwa zikifanya kazi na washikadau wengine wa sekta ya anga nchini Marekani ili kuelewa uwezekano wa 5G kuingiliwa na vifaa vya kupimia sauti vya redio," Airbus ilisema katika taarifa.
"Pendekezo la Usalama wa Anga ili kupunguza hatari zinazoweza kutokea limewasilishwa kwa Idara ya Usafiri ya Marekani ili kuzingatiwa."
Mwezi huu, FAA ilitoa maagizo ya kuonya kwamba 5G inaweza kvuruga utendakazi wa ndege, ikisema kuwa itatoa maelezo zaidi kabla ya tarehe ya kuzindua ya Januari 5.
Mnamo Novemba, AT&T na Verizon zilichelewesha uzinduzi wa kibiashara wa huduma ya wireless ya C-band kwa mwezi mmoja hadi Januari 5 na kuchukua hatua za tahadhari ili kudhibiti uingiliaji.
Mashirika kadhaa ya ndege yamesema kuwa hatua hizo hazikidhi mahitaji, baada ya Boeing na Airbus kusema walitoa pendekezo mbadala ambalo lingezuia usambazaji wa simu za rununu karibu na viwanja vya ndege na maeneo mengine muhimu
Wiki iliyopita, afisa mkuu mtendaji wa shirika la ndege la United Scott Kirby alisema maagizo ya FAA ya 5G yatazuia matumizi ya simu hizo katika takriban viwanja 40 vikubwa zaidi vya ndege nchini Marekani.
Mashirika ya teknolojia ya Marekani yanasema 5G ni slama na kulaumu mashirika ya ndege kwa kutoa taaarifa za kuogogya na za kupotosha kuhusu teknolojia hiyo.















