Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Joyce Msuya:Mtanzania ateuliwa kuwa Naibu Mratibu wa Misaada ya Dharura (UNOCHA)
Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres amteua Mtanzania Joyce Msuya kuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa Masuala ya Kibinadamu na Naibu Mratibu wa Misaada ya Dharura (UNOCHA).
Kabla ya uteuzi, Bi. Msuya alikuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).
Anamrithi Ursula Mueller wa Ujerumani ambaye Katibu Mkuu amemshukuru sana kwa uongozi wake na utumishi wake wa kujitolea wakati wa uongozi wake.
Msuya ana Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Mikrobiolojia na Kinga kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa, Canada, na Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Biokemia na Kinga kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde, Scotland.
Joyce Msuya amewahi kuwa Katibu Mkuu Msaidizi na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira mjini Nairobi, Kenya.
Akiwa katika wadhifa wake wa awali aliwajibika kwa bajeti ya dola za Marekani milioni 455 na miradi na oparesheni yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 1, iliyotolewa kupitia wafanyakazi 2,500 katika ofisi 41 na makao makuu.
Pia aliongoza mkakati na uendeshaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa katika Amerika ya Kusini na Afrika, likishughulikia sekta ya viwanda, biashara ya kilimo na huduma.
Bi Msuya ameolewa na ana watoto watatu.