Hijra: Mateso ya watu wenye jinsia ya tatu huanzia kwenye familia zao wenyewe

তৃতীয় লিঙ্গের মানুষেরা পরিবারেই সবচেয়ে বেশি নিগৃহীত হন

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watu wa jinsia ya tatu (waliobadili jinsia)huteswa na familia
Iliyochapishwa

"Familia yangu ilifikiria nilikuwa namashetani. Ndio maana nina tabia kama za msichana. Kabiraji amekuwa akifanyiwa ukatili wa kimwili katika maeneo mengi."

Maneno haya yalizungumzwa na Shammi wa Dhamrai anayeishi karibu na Dhaka. Kwa sasa amebadilisha jinsia yake na kuwa mwanamke.

Ingawa utambulisho wa jinsia yake ni wa kiume kwa kuzaliwa, wakati alipofikia umri wa kubalehe aligundua kuwa alikuwa tofauti na wanafunzi wenzake wa kiume.

Shammi anasema alipenda kuvaa mavazi ya wasichana, kufanya kazi za nyumbani na kuwa na wasichana tangu alipokuwa mdogo.

Matokeo yake, alikuwa akisengenywa, kupigwa na hata akapewa hirizi na wazazi wake Shammi walimuona kama mgonjwa.

"Walihakikisha sitoki nje ya nyumba na kuzungumza na mtu yeyote. Kawasababu nilipozungumza na watu walisema mimi ni mtu aliyebadili jinsia yake. Wazazi wang una ndugu zangu walianza kunilaumu kila wakati ."

''Sijui mimi ni nani, Kwanini nipo, sijui ninalopaswa kufanya sasa hivi, Sijui niende kwa nani, Nina mtu yeyote duniani, niko peke yangu duniani, kuna mtu mwingine saw ana mimi ?" Nilikwua nakula kwa uvivu. Wakati mmoja nilijaribu kujiua, "alisema Shammi.

Shammi anasema alikuwa na umri wa miaka 13/14 wakati huo. Masomo yake yaliishia darasa la saba kutokana na utambulisho wake wa jinsia.

Wakati huu alifahamiana na mtu mwingine wa jinsia ya tatu kama yeye. Wakati huo alimchukua Sammi katika nyumba ya hijra.

Shammi anasema familia yake ilifurahi alipoondoka nyumbani.

Familia yake haikuwa bado imemkubwali. Tanisha Yasmin Chaiti wa Rajbari kwa sasa amekuwa mwanamke. Alizaliwa kama mwanaume.

নিজের লিঙ্গ পরিচয় তাদের কে বোঝানোর জন্য রীতিমত যুদ্ধ করতে হয় পরিবারের সঙ্গে

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Walipambana na familia zao zionyeshe utambulisho wao wa jinsia

Tanisha Yasmin Chaiti alisema, "Nilipokuwa darasa la saba, nilimwambia mama yangu, Mimi sio mtoto wako wa kiume.

Ninataka kuwa msichana. Mama yangu alilia tu kwa siku saba na usiku mara saba. Halafu familia yangu na ndugu zangu wakaanza kuniambia. Ninavaa kama mtu aliyebadili jinsia. "

Kwanini familia haikukubali?

Watu wenye jinsia ya tatu (waliobadili jinsia) ambao wanafahamika kama hijtas katika jamii ya Bangradesh huchukiwa na kuchukiwa kwanza ndani ya familia zao wenyewe.

Wanalazimika kupambana na familia zao kuonyesha utambulisho wa jinsia yao.

Jamaa wa familia zao hawawezi kukubali kamwe kwamba mtoto aliyezaliwa kuwa mwanaume au mwanamke mwenye utambulisho wa jinsia hiyo anaweza kuwa na tabia kama mtu wa jinsia tofauti na muonekano wake baada ya umri fulani.

হিজড়া জনগোষ্ঠীর অধিকার নিয়ে আন্দোলনকারীরা বলেছেন,যেসব অভিযোগ তারা পান, তার বড় অংশই হিজড়াদের বাবা-মায়ের সম্পত্তির ভাগ না পাওয়ার বিষয়ে।

Chanzo cha picha, ALLISON JOYCE

Maelezo ya picha, Wanaomuunga mkono wamekuwa wakifanya juhudi za kuhakikisha maelezo yake yanapatikana katika mtandao

Shinikizo la jamii la kutowaheshimu jamaa wa familia huwaathiri. Wengi hawawezi kupuuza shinikizo hilo.

Mwanaume mmoja kwa jina Nazrul Islam anasema wakati kaka yake alipoanza kuwa na tabia kama za kisichana, familia yake karibu familia yake itengwe kwenye nyumba moja kijijini.

Bw Islam anasema, "Watu katika Kijiji walikuwa wakiniita mimi, na baba yangu na kusema, mvulana wenu ni mchafu, kwanini mnakaa naye nyumbani?

"Wafanyakazi wanaofanya kazi na mke wangu walikuwa wakimuita kwa kutumia maneno makali. Lakini mama yangu ndiye aliyeumia zaidi. Watu wa kijijini kwetu walikuwa wanakuja kuchungulia nyumbani kwetu. Wakati kaka yangu alipoondoka nyumbani akiwa na umri wa miaka 16/17 hakuna aliyemzuwia.

তৃতীয় লিঙ্গ কোন ব্যাধি না, বলছে ডব্লিউএইচও

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Shirika la afya la Umoja wa Mataifa -WHO, lilisema kuwa jinsia ya tatu sio hitilafu ya kimaumbile

Mabadiliko ya kiakili au ya kimwili?

Taslima Yasmin, mwalimu wa sheria katika Chuo kikuu cha Dhaka University ambaye alifanya utafiti kuwahusu watu wa jinsia ya tatu-waliobadili jinsia , alisema yanawez kusababishwa na sababu za kiakili na kimwili.

Taslima Yasmin anasema: " Mara nyingi huwa wanakuwa ni wanaume kibaiolojia lakini wao wanajifikiria kama wanawake. Kwahiyo jinsi mwanamke anavyoonekana katika jamii , hujionyesha hivyo. Katika akili zao hujihisi wanawake kabisa . "

"Kando na hilo, kuna watu ambao utambulisho wao hawajihisi kuwa ni watu wa jinsia ya kiume wala ya kike. Kuan watu tunaowaita wenye jinsia zinazoingiliana. Ni mchanganyiko wa viungo vya jinsia vya kike na kiume , "alisema.

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa -WHO, lilisema kuwa jinsia ya tatu sio kasoro ya kimaumbile.

Unaweza pia kusoma:

Watu wenye jinsia ya tatu ni akina nani?

Kuna mkanganyiko kuhusu ni watu gani wenye jinsia ya tatu katika Bangladesh.

Kwa kawaida wakati mvulana anapokuwa na tabia za kike au anapobadilika na kuwa msichana huwa anajumuishwa katika kundi la waliobadili jinsia au jinsia ya tatu.

Lakini wale wanaopigania haki zao wanasema huenda hawakuzaliwa na jinsia ya kiume, ya kike au jinsia yoyote ile.

Hatahivyo, haiku wazi katika Bangladesh ni nani anayefaa kuwa mtu mwenye jinsia ya tatu, Taslima Yasmin.

Iwe jinsia ya tatu, aliyebadili jinsi au utambulisho wa jinsia yoyote ile,ukweli ni kwamba tabia zao ni kinyume na mienendo iliyozoeleka katika jamii sawa na ile ya wanawake na wanaume.

Mashirika mbali mbali yanapigania haki zao nab ado kuna mkanganyiko katika jukwaa la serikali la uundwaji wa sera.

Hatahivyo jambo la kwanza kabisa, iwapo watapewa usaidizi kamili kutoka kwa familia, basi maisha yao yanaweza kuwa rahisi zaidi.