Janga la covid Uganda: Kumi kati ya watoto wa Fred Ssegawa hawatarudi shuleni tena.

Iliyochapishwa

Hii inatokana na kufungiwa nje ya msomo tangu Machi 2020, kufuatia hatua kali za Uganda za kudhibiti virusi vya corona.

Wawili kati ya watoto wake 12 walikuwa wadogo sana hawakuwa wameanza masomo wakati huo.

Bw Ssegawa ambaye amekuwa mwalimu kwa miaka 20 amepoteza kipato chake kidogo cha karibu dola 40 kwa mwezi.

Alipokuwa na kazi alikuwa na wakati mgumu kuwapeleka watot wake shuleni. Sasa akiwa na umri wa miaka 49 anatumia wakati wake mwingi akifanya kilimo na kuachana na kazi ya kufunza. Anataka kutumia ardhi kidogo aliyo nayo.

Watoto wake watatu walio na umri kati ya miaka 10 na 15 humsaidia kazi za shambani. Wale wakubwa hutafuta pesa jinsi wawezavyo.

Rais Museveni amesisitiza kuwa kufungwa kwa shule kulikuwa na umuhimu wa kuwalinda watu hadi watu wazima wapate chanjo.

Ni kweli kuwa visa vya ugonjwa huo na vifo vimekuwa vya chini lakini anayopitia Bw Ssegawa na famialia yake ni ishara ya athari ambazo zimeibuka kufutia hatua za afya zilizochukuliwa.

Nilipata, mabinti zake wawili na mwanae, wakivuna maharage kwenye shamba lao huko Luweero safari ya umbali wa masaa manne kutoka Kampala.

Maharage hupandwa pamoja na mahindi na mihogo kuweza kuwalisha famili ya watu 14,

"Baadhi ya watoto walikuwa shule za bweni. Hawakuwa wakifanya kazi kama hii awala. Lakini kutokana na hali ilivyo wamelazimika kujifunza," Bw Ssegawa anasema wakati watoto wakisaka kwenye magugu kuvuna maharage.

Wawili kati ya watoto wake wakubwa, wote wa kiume walikuwa wakijiandaa kwa mtihani muhimu wakati shule zilifungwa. Ni mmoja tu alifanikiwa kurudia wakati shule zilifunguliwa kwa muda mwezi oktoba 2020 ili watoto wapate kufanya mitihani.

Afadhali ningekuwa shuleni

Huyo ni Danile, 21, aliyekuwa na mpango wa kijunga na chuo kikuu.

Badala yake anaunda matofali ya kuuza katika sehemu moja ya shamba la familia.

Licha ya kuwa ndoto zake za kupata elimu ya juu sasa zimezimwa, kwa kuuza tofali moja kwa shilingi 80 za Uganda sawa na dola 0.02, Danielea na matumaini ya kuwasaidia wadogo wake kuendelea na masomo.

Lakini kwa sasa, ndugu yake mwenye umri wa miaka 16 Paul hutumia muda wake kuchonga nyanya na vitunguu katika kibanda kimoja kidogo karibu na nyumbani kwao. Hapa anapika chapati na omellete maafuruku kama rolex katika eneo hili.

"Janga liliathiri masomo yangu. Nilikuwa nafanya kazi na kujilipia karop. Sipendi kazi hii afadhali niwe darasani," anasema, akiongeza kuwa hana uhakika atapata pesa za kutosha kumwezesha kurudi shuleni wakati shule zitafunguliwa.

Licha kuwa karo hailipwi kwenye shule za msingi za umma nchini Uganda, Wazazi wanahitajika kulipia sare na mambo mengine muhimu, ambayo ni ghali kwa wengine. Pia kwenye shule nyingi za vijijini, kuna uhaba wa walimu na madarasa kuweza kuwahudumia watoto wote.

Bw Ssegawa anasema inamuuma sana kuona watoto wake wakihangaika.

"Nilitaka watoto wangu wote wamalize shule ya upili. Lakini sidhani hilo litawezekana.

"Ninajua umuhimu wa elimu. Siku hizi, huwezi kupata kazi nzuri bila elimu. Ni huzuni kuona watoto wangu wakiwa hivi," anasema mwalimu huyo wa zamani.

Kumekuwa na masomo kwenye radio na televiseni, pia magazeti na baadhi ya shule zimechapisha masomo, Lakini hayajafiki kila mwanafunzi.

Utafiri wa mwezi Aprili uliofanywa na Forum for African Women Educationalists uligundua kuwa zaiid ya nusu watioto milioni 15, elimu imekwama kabisa huku watoto wa shule za msingi wakiathirika zaidi.

Walio na pesa wana uwezo wa kupata masomo ya mitandaoni na walimu wa nyumbani Lakini kwa Bw Ssegawa ni ndoto.

Maisha yangu yalibadilika wakati nilipata ujauzito

Mpwa wake mwenye umri wa miaka 17 Madina Nalutaaya, anaishi umbali wa safarii ya dakika 30 kwa kutumia gari kutoka kijiji chake Ssegawa.Yeye pia hatarudishwa shuleni.

Alikuwa katika mwaka wa mwisho wa shule ya msingi kabla ya masomo kusimamishwa. Sasa hivi yeye ni mama wa mtoto wa miezi miwili.

"Maisha yangu yalibadilika wakati nilipata ujauzito. Baba ya mtoto wangu alitoroka."

Mamlaka ya mipango ya kitaifa nchini Uganda ilikadiria Agosti kuwa asilimia 30 ya wanafunzi wote nchini Uganda hawatarudi shuleni kutona na mimba za mapema, ndoa za mapema na ajira za watoto.

Data za afya za serikali zimeonyesha kuwa visa vya mimba miongoni mwa wasichana walio na umri wa kati ya miaka 10-14 viliongezeka zaidi ya mara nne kati ya mwezi Machi, wakati shule zilifungwa mara ya kwanza na Septemba 2020.

Mfumo wa elimu nchini Uganda unawaruhusu wasichana waliojifungua kurejea shuleni lakini wengine hukosa msaada nyumbani au hukosa njia za kuwalea watoto wao.

"Nina mtu ninaweza kuachia mtoto wangu lakini sina uwezo wa kutafuta karo yangu, na pesa za mahitaji ya mtoto wangu," anasema Madina.

Serikali ina mipango ya kufungua shule Januari mwakani kwa sharti kuwa wanafunzi walio na umri wa zaidi ya miaka 18 watakuwa wamechanjwa.

Lakini huenda mamlaka zikakumbwa na tatizo.

Kuna baadhi ya walimu kama Ssegawa waliojiunga na kilimo au waliopata kazi nzuri kuwalisha famialia zao, na huenda wasirudi shuleni.

Unaweza pia kusoma:

Bw Ssegawa mwenyewe hana matumaini ya kuendelea kuwa mwalimu na anatumai kuwa siku moja shamba lake litampa kipato.

Majengo ya shule yamedhoofika na karibu shule 4,300 zitabaki zimefungwa kutokana na changamoto za kifedha.

Athari za elimu ndogo

Pia kuna mipango cha kuwalenga watoto walio katika hatari ya kuacha shule au kutoka elimu ya kiufundi kama njia mbadala.

Lakini kuna pia kuna athari za muda mrefu.

Dr Ibrahim Kasirye, mtafiti chuo kikuu cha Makerere anasema kuwa elimu duni hupunguza fursa za kupata kazi nzuri na kusababisha changamoto za kukwepa umaskini.

Hali hii huchangia kuongezeka uhalifu miongoni mwa vijana, kwa sababu vijana hawa ni lazima watafute kupata kuishi, aliiambia BBC.

Kwa Bw Ssegawa anahisi kukosa matumaini.

Akipumzika kivulini na wawato wake baada ya kazi anasema anaumia sana moyoni anapofikiri kuhusu hatma yao.

Anaweka matumaini yake kwa elimu ya bure ya shule za msingi maeneo za vijijini Lakini huenda hilo lisifanyike hivi karibuni.

Unaweza pia kutazama: