Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mji wa Colombia ambao polisi hawathubutu kuondoka kwenye vituo vyao
Watu hawaongezi chumvi wanaposema kwamba "Polisi wanaishi kama wako jela" mjini Tibú, manispaa iliyopo mpaka wa Colombia na Venezuela.
Maafisa hapa hawawezi kwenda kwenye mgahawa hata wanapokua mapumzikoni, baadhi ya wafanyabiashara wanawakataza kununua chakula na familia zao zikijaribu kuwanunulia, pia zinashambuliwa, kutishiwa na mara nyingine hata kuuawa.
Vituo vya polisi vimezingirwa na nyaya maalum za kutoa ulinzi, dirisha zimefungwa kwa kutumia simiti au matofali, kuta zenye zilizotobolewa kwa risasi zinaashiria makabliano ya hivi karibuni.
Wanaume hao waliovalia sare wanaishi kula siku kulinda kambi yao kupitia matundu madogo yaliyowekwa katika maeneo maalum. Wanatamani kuondoka eneo hilo ambalo, kulingana na wataalamu wa mantiki ya polisi, wangeweza tu kupewa kama matokeo ya adhabu.
"Hii ni jehanamu, hatuwezi kwenda nje," afisa mmoja anasema. "Hii ni historia ya kifo kilichotabiriwa," asema mwingine. Na mwingine: "Kwangu mimi kipaumbele hapa ni kumaliza kipindi nilichopewa na, bila shaka, kutoka nje na hai wangu."
Tibú ni njia kuu ya kuelekea Catatumbo, eneo kubwa jangwani, milima na ardhi yenye unyevunyevu inatumiwa kwa pamoja kati ya Colombia na Venezuela ambapo uzalishaji wa Cocaine unashamiri upya na vikundi vilivyojihami vimegawanyika na kuongezeka.
Mwezi mmoja uliopita, mauaji ya vijana wawili wa Venezuela ambao walipatikana wakiiba suruali yalifanya taifa kuweka kipaumbele chake katika manispaa hii yenye wakazi 40,000.
Hofu iliyokuwa ikiishi hapa wakati mbaya zaidi wa vita, miaka ya 1990, inaonekana kuibuka tena huku ulanguzi wa dawa za kulevya ukijiibua tena na mkataba wa amani uliyotiwa saini kati ya Serikali na waasi mwaka 2016 ukianza kuonyesha nyufa zake.
Katika ziara yake katika eneo hilo, BBC Mundo alizungumza kwa sharti la kutotaja majina ya polisi kadhaa, lakini mazungumzo rasmi na kamanda mwanadamizi hayakuweza kukamilika licha ya majaribio kadhaa.
"Epuka polisi"
Katika mitaa inayozunguka kituo cha Tibú kulikuwa na maduka, mikahawa na eneo dogo la kujivinjari ambapo madanguro na wacheza densi huwaburudisha wenyeji .
Kila kitu ambacho kina harufu ya tombo (polisi) kinapaswa kuepukwa," anasema jirani wa mji huo ambaye aliacha nyumba yake na biashara yake, na kuhamia mji mwingine.
Jirani mwingine, ambaye utambulisho wake umebanwa kwa sababu ya kiusalama, anadai kutishiwa kwa sababu ya uhusiano wa familia yake na polisi.
Walimpa onyo la mwisho, akaamua kuuza alichoweza na, kwa msaada wa jamii, akafanikiwa kuondoka.
Sasa, kutoka mbali, anajaribu kukodisha nafasi mbele ya kituo, lakini "nyumba hiyo sasa haifai chochote," anacheka.
"Walituambia: 'Ikiwa hutaondoka, basi yeyote atakayekufa na afilie mbali kwa sababu tutashambulia kituo cha polisi kwa bomu," anaongeza.
Maafisa wa polisi ndani ya kituo wanahisi kuwa vitani, lakini wakiwa na ulinzi na silaha za kituo kingine: "Hapa lazima kuwe na wilaya maalum, kituo ambacho kinaweza kutawala na kuwa Serikali, kwani bila hivyo ni vigumu sana ", wanadai.
"Tunapaswa kukarabati vituo hivi na kujihami kupitia vikosi maalum vya serikali, bila shaka hiyo ni ghali sana."
Afisa mmoja alipoombwa kuelezea kwa nini iwe hivyo katika nchi ambayo inatumia hela zaidi katika ulinzi kuliko nchi nyingine yoyote ya Amerika Kusini, alijibu kwa ukimya usio wa kawaida, kufungua mikono yake kana kwamba anasingizia kitu na kuhitimisha: "Sijui, ukweli ni kwamba, sina maelezo. Kwa hilo".
Ukarabati mdogo unaendelea katika sehemu moja ya jengo hilo, lakini wafanyikazi na vifaa vya ujenzi vililazimika kuletwa kutoka mkoa mwingine wa nchi kwa sababu eneo lolote linalojihusisha na polisi liko hatarini.
Ndivyo ilivyo kwa chakula, ambacho lazima walete kutoka jiji kuu la karibu zaidi, Cúcuta, na kukipika wenyewe.
Doria za hapa na pale zinafanywa na wanajeshi tu wanaotumia zana kali za kivita kuoa ulinzi kwa polisi wa kawaida. "Tunatumia dakika 15 tu kufanya shughuli zetu na vituoni kurejea kwa sababu hatari ya mashambulizi inatukodolea macho," wanaeleza.
Na hiyo ndio sababu ni nadra sana kwa maafisa wa polisi kutoka nje ya vituo vyao katika mji huu. Hali ambayo imezua ghadhabu ya kitaifa kuhusiana na kisa cha vijana wa Venezuela, ambao kwanza walihifadhii na wakazi ,ambao baadaye walipiga simu polisi mara 12 lakini wito wao haukuitikiwa.
Vijana hao yadaiwa walichukuliwa na watu waliokuwa kwenye piki piki ambao waliwaua na kutupa miili yao kkando ya barabara ikiwa imeandikwa maneno ''ni wezi''.
Pia polisi hawatoki nje ya vituo vyao kwa sababu kulingana na maafisa, baadhi ya malalamiko ni njama inayotumiwa kuwavizia na kuwashambulia.
Huwezi kufanya kazi yako hapa, unahisi kama umefungiwa na kila wakati una hofu ya kushambuliwa (...) Familia yangu inaishi kwa wasi wasi na roho mkononi," anasema mwanamume aliyevaa sare.