Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Hapakuwepo na mgusano wa kimwili: Mahakama ya juu zaidi India ‘yawakasirisha wengi' kwa kupinga ukatili wa kingono
Mahakama ya juu zaidi nchini India imebatilisha uamuzi tata wa mahakama kuu wa kufuta kosa la ukatili wa kingono wa mwanaume aliyetuhumiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 12 kwasababu "hapakuwa na mgusano wa mwili -kwa mwili'' na muathiriwa.
Uamuzi huo , uliopitishwa na jaji mwanamke wa mahakama ya juu zaidi katika jimbo la Mumbai mwezi Januari, ulisababisha malalamiko mengi kutoka kwa umma.
Wana harakati na wataalamu wa sheria walisema uamuzi huo utakuwa " mfano hatari" na kuitaka mahakama hiyo ya juu zaidi kuubatilisha.
Wanaharakati wanasema utawavunja moyo watoto na kuwafanya wasiripoti unyanyasaji wanaofanyiwa.
Mahakama ya juu zaidi ilisema nini?
Katika uamuazi wake Alhamisi jopo la Mahakama ya juu zaidi lilisema kuwa mahakama zinapaswa kuangalia katika madhumuni ya kitendo chenyewe cha ngono na wala sio kuangaliwa iwapo kulikuwa na mgusano wa mwili-kwa mwili.
"Kuangalia tu suala la mgusano wa mwili-kwa mwili haiwezi kutafsiri kitendo kilicholengwa , na badala yake inaweza kupotosha uhalisia wa tafsiri ya kipengele ," wavuti wa kisheria wa LiveLaw uliripoti.
Katika maneno makali ya hukumu, majaji walisema kuwa uamuazi wa mahakama kuu ya Mumbai ilikuwa "imehalalisha tabia ya ubakaji bila kuwa makini" na kwamba "lengo la sheria haliwezi kuruhusu mkosaji kukwepa vipengele vya sheria ".
Kesi ilikuwa inahusu nini ?
Mwezi Disemba 2016, mwanaume mwenye umri wa miaka 39-alishutumiwa kwa kumpapasa msichana mwenye umri wa miaka 12. Mama yake msichana huyo alikuwa amedai kuwa alikuwa amemlaghai binti yao kwenda nyumbani kwake ambako aliyaminya matiti yake na kujaribu kumvua suruari yake ya kulalia.
Mhakama ilikuwa imempata na hatia ya ukatili wa kingono kwa mujibu wa sheria na kumhukumu kifungo cha miaka miaka mitatu jela.
Lakini tarehe 12 Januari, Jaji wa mahakama ya juu ya Bombay Pushpa Ganediwala alisisitiza kuwa kuyaminya matiti ya msichana bila kumvua fulana haukuwa unyanyasaji wa kingono kwasababu hapakuwa na mgusano wam wili-kwa mwili na hilo ni kosa dogo la unyanyasaji.
Uamuzi huo ulilaaniwa pakubwa na maombi kadhaa kuwasilishwa katika mahakama ya juu kutaka uamuzi huo ubatilishwe.
Tarehe 27 Januari, Mahakama ya juu zaidi ilitangaza agizo la kuzuwia utekelezwaji wa hukumu hiyo hadi itakapoamua juu ya suala hilo.
Baada ya uamuzi wa Alhamisi, mshitakiwa atatakiwa kutumikia kifongo cha miaka mitatu jela.
Changamoto
Mwanasheria mkuu wa India KK Venugopal, ambaye alikuwa mmoja wa waliowasilisha ombi la kusitishwa kwa uamzi wa awali wa mahakama, alielezea uamuzi wa mahakama kuu kama wa "kushitusha na kushangaza".
Alisema kuwa kama hautabadilishwa, agizo hilo lita "weka mfano hatari ".
Wakati kesi hiyo ilipokuwa ikiendelea, Bw Venugopal alidai kwamba mgusano wa mwili -kwa mwili haukuwa "jambo muhimu" kwa uhalifu wa ukatili wa kingono chini ya sheria ya unyanyasaji wa kingono-Pocso Act.
"Iwapo kesho, mtu atavaa glovu mbili za upausaji na kuutomasa mwili wa mwanamke, hataaadhibiwa kwa unyanyasaji wa kingono kulingana na uamuazi huu.
Huu ni uamuzi wa kushangaza na kushitua ," alinukuliwa na gazeti la Indian Express akisema.
"Mshukiwa alijaribu kuishusha chini salwar [nguo ya chini ya kulalia ] ya msichana n a hata wakati huo dhamana ilitolewa," aliongeza.
Malalamiko
Uamuzi wa mahakama ya juu, uliidhinishwa na jaji mwanamke, ulikosolewa na wanaharakati wa watoto na wajumbe wa makundi ya kiraia ambao waliuelezea kama wa " kuchukiza na usiokubalika".
Wakosoaji walisema kuwa hukumu ilikuwa ina kasoro kwasababu ilikuwa ni ya watoto, ambaomara nyingi hawawezi kujilinda wenyewe.
Kulingana na uchunguzi wa serikali wa mwaka 2007 watoto wawili kati ya watatu wa India walikuwa wamefanyiwa ukatili wa kingono na kwamba 53% kati ya watoto wote waliohusika katika utafiti huo karibu 12,300 waliripoti aina moja au au zaidi ya unyanyasaji wa kingono.
Mwaka jana , rekodi yaa kitaifa za ofisi ya uhalifu ilirekodi makosa 43,000 chini ya sheria ya unyanyasaji wa kingono -Pocso Act - hii ikiwa ni sawa na wastani wa kisa kimoja kwa kila baada ya dakika 12.
Taarifa zaidi kuhusu ukatili wa kingono India:
Wanaharakati wanasema idadi halisi ya watoto wanaobakwa iko juu zaidi kwani visa nyingi vya unyanyasaji ambapo wanyanyasaji huwa ni watu wa familia au watu ambao wanyanyaswaji wanawafahamu, na visa hivyo haviripotiwi.