Maisha yangu kama mtu mwenye jinsia mbili: “Nikiwa na umri wa 12 nilikuwa na ndevu na nilipata hedhi”

Iliyochapishwa

Wakati Alec Butler alizaliwa mwaka 1959 waliamini yeye alikuwa ni msichana. Lakini alipoendelea kukua aligundua kuwa hakuwa mvulana wala msichana.

Nilipokuwa na umri wa miaka 12, ndevu zangu zilianza kumea na wakati huo huo nilikuwa napata hedhi zangu.

Kwangu ni kitu kilichonichanganya na wazazi wangu waliogopa sana. Walinipeleka kwa madaktari kadhaa lakini hakuna mtu alifahamu kuhusu hali hii kwenye mji mdogo niliokuwa naishi nchini Canada.

Daktari mmoja alisema: "Tutamuweka kwa taasisi ya masuala ya akili hadi ajifunze kuvaa kama msichana.

Lakini kwa umri wa miaka 12 hata wale wasichana waliokamilika hawahitajiki kufanya hilo.

Kwa bahati nzuri wazazi wangu walikasirika na wakasema, "hatuwezi kufanya hivyo. Tunakupenda na utachagua kile ungependa uwe." Na sio watoto wote wenye jinsia mbili wana bahati kama hiyo.

Familia yangu ilinisaidia sana na ikanikubali vile nilikuwa lakini kitu kigumu zaidi kilikuwa ni shule na kwenye jamii.

Hakuna mtu aliyeelewa wakati huo kuwa msichana anaweza kuvaa suruali ndefu.

Nilihisi na shinikizo za kupata homoni ili niwe msichana zaidi lakini kwa wakati huo pia nilitaka niwe na umbo la kiume, nilitaka niwe mvulana.

Nilishikwa na wasiwasi kwamba watu wataniona kama mtu asiye na akili timamu kwa hivyo nikajaribu kwa kila njia nisijipate kwenye matatizo mengi.

Lakini kwa mwili kama wangu ilikuwa ni vugumu.

Nilikuwa na matatizo kwa sababu nilipenda kuwa msichana. Lakini iligeuka kuwa vibaya kwa sababu nilikuwa na jinsia mbili na wala sikuwa mvulana.

Wakaniita mpenzi wa jinsia moja na kunikemea: "Wewe ni mgonjwa!" na tena, wakaniandikia vijikaratasi darasani na ujumbe kama "mbona hujiui?"

Wakati huo tuliishi kwenye kambi ya jeshi mashariki mwa Canada, kwa sababu baba yangu alikuwa jeshini lakini alikuwa na wasi wasi kutokana na hali yangu na hivyo aliomba astaafu mapema ndipo tukahamia kisiwa cha Cape Breton huko Nova Scotia.

Lakini hali ilikuwa mbaya kwa njia nyingi kwa sababu tulitengwa na kuzungukwa na watu wasiolewa.

Maisha magumu

Nilipomaliza shule ya upili mwaka 1978, ilikuwa vigumu kwangu kupata ajira.

Nilihama kwenda Toronto ambapo nilionekana kuwa mpenzi wa jinsia moja.

Nilitaka nipate msaada na nihisi kukubalika katika jamii. Sikumfahamu mtu yeyote mwenye jinsia mbili hata sikufahamu jina hilo.

Maisha hayakuwa rahisi

Walinitishia maisha mitandaoni na kunirushia vitu. Mtu mmoja akajaribu kiniingiza ndani ya gari kwa nguvu. Kwenye gwaride la watu wapenzi wa jinsia moja, wanaume walizunguka na kutishia kunivua nguo zangu. Kilikuwa kitu kibaya.

Kuna wapenzi wa jinsia moja wengi walionichukia na moja ya sababu ambazo kwa sawa ninajitambua zaidi kama mwanamume ni kwa sababu ya chuki hizo.

Mpenzi wa jinsia moja nilie na ndevu

Lakini nilifanikiwa kuzalisha kazi zangu kwa sasa (Alec ni muandishi na mtengeneza filamu).

Mwanzo wa miaka ya 1990 niliwatunza baadhi ya marafiki waliokuwa wanakufa kutokana na ugonjwa wa ukimwi. Wakati huo nilikuwa na kazi nyingi.

Sikutaka watu wajue nilikuwa na ndevu lakini sikuwa na muda wa kunyoa. Marafiki zangu wakasema, uko na ndevu, inaonekana vizuri sana, unahitaji kuziacha zimee.

Kwa hivyo wakati marafiki zangu walifariki niliacha ndevu zangu zikakua kwa kuwakumbuka. Lakini sasa nina matatizo tena.

Mambo hayaniendei vizuri wakati ninafika kwa baa za wapenzi wa jinsia moja , hawaelewi ni kipi ninafanya huko, lakini ninaweza kuwalezea kuwa mimi pia ni mpenzi wa jinsia moja licha kuwa nina ndevu.

Mtu aliyebadilishia jinsia

Miaka ya 1990 nilijua kuwa sikuwa mwanaume wala mwanamke.

Siku moja mtu fulani ambaye alikuwa amenijua kwa miaka mingi aliniambia kuna uwezekano kuwa wewe una jinsia mbili na nikauliza hicho ni kitu gani?

Kwa hivyo nikafanya utafiti mkubwa nikagundua maana yake ni nini

Kisha nikakumbuka mambo mama yangu aliniambia kuhusu wakati alikuwa amebeba mimba yangu.

Alikunywa dawa fulani ambayo niligundua kuwa inaweza kusababisa hali yangu na nafikiri hicho ndicho kilitokea. Mapema miaka ya 1990 nikabadilisha jina langu kuwa Alec.

Sio mwanamume wala mwanamke

Ni vigumu kwa watu kuelewa suala la kutokuwa mwanamke au mwanamume na hata watu kama hao.

Watu wengi hufikiria kuchagua kuwa wanaume au wanawake ni rahisi.

Haikuwa na maana kwangu kama wangesema mimi ni mvulana au msichana

Na ujumbe ambao ningependa kutoa kwa watu kama hawa ni wajivunie jinsi walivyo.