Fahamu jinsi binadamu walivyopoteza mikia yao

Ushawahi kujiangalia huko nyuma na ukashangaa au kujiuliza mkia wako umeenda wapi? Inaweza kuonekana kama jambo la masihara hivi au swali la kitoto.
Lakini kwa wanasayansi ni jambo muhimu sana. Kama binadamu wanafanana na nyani ukizungumzia kibaiolojia, kwa nini nyani wa mkia na sie binadamu hatuna? "Ni swali zuri," anaunga mkono Bo Xia, mwanafunzi wa baiolojia kutoka shule ya Grossman ya chuo kikuu cha New York, Marekani.
Mkia unaweza kuwa na faida nyingi kwa dunia ya wanyama. Tangu ionekane kwa wanyama walioishi mwanzoni zaidi ya miaka milioni 500 iliyopita, inaelezwa kuwa na kazi nyingi. Kwa samaki mkia unamsaidia kuogelea awapo majini. Kwa ndege inamsaidia kupaa na kwa wanyama mkia inasaidia wakati wa kutembea . Mkia unaweza kutumika kama silaha ya kujilinda, kwa wadudu kama nge. Ama ishara ya onyo kwa baadhi ya nyoka.
Kinachowasumbua wanasayansi ni kwanini wanyama ama viumbe wengine akiwemo nyani anayefanana kibaiolojia na binadamua wana mikia na binadamu hana. Xa amefuatilia kuhusu nyani, sokwe na panya, tabia zao zinaonyesha mapinduzi ya mikia na ukuaji wao. Amegundua panya anakua akiwa na aina mkia wa muundo tofauti, mikia mingine mifupi, mikini haikui kabisa.
Kitedawili cha mkia na miguu

Mwandishi wa vitabu kikiwemo cha 'The Origin of Man 'Charles Darwin, amewahi kugusia kuhusu mapinduzi ya ukuaji wa nyani na sokwe akiuhusisha na ule wa binadamu. Kupitia kitabu chake hicho kuhusu asili ya binadamu kilichochapishwa mwaka 1871, alieleza dhana ya mapinduzi ya ukuaji inayomgusa pia binadamu.
Hata hivyo, binadamu na sokwe, wenye asili inayofanana, wanavinasaba (DNA) vinavyofanana kwa asilimia 98%.
Watu wa kale wa jamii ya sokwe waliokuwepo zaidi ya miaka milioni 20 iliyopita hawakuwa na mikia.
Sokwe anamiguu minne na mkia, binadamu ana miguu miwili bila mkia. Xia anabaki na maswali mengi kuhusu wapi mkia wa binadamu ulipokwenda, ikiwa anafanana vinasaba kibaiolojia na vya sokwe?
Kujua asili ya vizazi ndio jawabu

Xia amekuwa akitafiti kuhusu binadamu na mkia tangu apate majeraha ya mfupa wa chini ya mgongo alipokuwa kwenye taksi (uber) miaka miwili iliyopita.
Anatumia panya kutaka kupata ukweli wa asili ya binadamu na huenda akapata kujua kisayansi mkia wa binadamu ulikwenda wapi. Xia na wenzake wnaangalia mabadiliko ya ukuaji wa panya. Mpaka walichogundua baada ya shughuli zao za kitafiti ni kwamba ukuaji wa mkia wa panya wanaotumika kwneye utafiti huo haukui kama ilivyo mikia wa panya wengine.

Pengine matokeo hayo yanaonyesha umuhimu wa jukumu la mabadiliko kwenye asili ya binadamua. Wanasayansi wanasema kuna vichocheo zaidi ya 30 vinavyohsika kwneye ukuaji wa mkia wa mnyama, watafiti wa Marekani wanauzungumzia kimoja tu.
Xia anasema, binadamu wote wana mfupa wa mkia unaofanana, lakini kwa utafiti waliofanya kwa panya, mifupa hiyo ya mikia kwao inatofautiana kwa ukubwa.
Anachohitima Xia ni kwamba kuna mfululizo wa ukuaji , ulioathiri mabadiliko ya ukuaji wa binadamu miaka milioni 25 iliyopita.















