Pandora Papers: Mwongozo rahisi kuhusu nyaraka zilizovuja

- Author, Na Pandora Papers reporting team
- Nafasi, BBC Panorama
- Iliyochapishwa
Pandora Papers ni uvujaji wa nyaraka karibu milioni 12 ambazo zinafichua utajiri uliofichwa, kuepukana na ushuru na, wakati mwingine, utakatishaji fedha unaofanywa na baadhi ya matajiri na wenye nguvu ulimwenguni.
Zaidi ya waandishi wa habari 600 katika nchi 117 wamekuwa wakitafiti kwa vyanzo 14 kwa miezi, wakipata taarifa ambazo zinachapishwa wiki hii.
Jumuiya ya Kimataifa ya Wanahabari wa Upelelezi (ICIJ) huko Washington DC, ilizipata data hizo, ambayo imekuwa ikifanya kazi na mashirika zaidi ya 140 ya habari kwenye uchunguzi wake mkubwa zaidi ulimwenguni.
BBC Panorama na Guardian wameongoza uchunguzi nchini Uingereza.
Mambo gani yamebainika?
Pandora Papers inahusisha nyaraka milioni6.4, karibu picha milioni tatu, zaidi ya barua pepe milioni moja na zilizokuwa kwenye majedwali karibu nusu milioni.
Taarifa mpaka sasa zinahusisha:
- Matumizi ya pauni milioni 70 ya Mfalme wa Jordan kwenye mali nchini Uingereza na Marekani kupitia kampuni zinazomilikiwa kwa siri
- Uhusika wa siri wa familia inayoongoza Azerbaijan katika mikataba ya mali nchini Uingereza yenye thamani ya zaidi ya pauni milioni 400
- Kushindwa kwa waziri mkuu wa Czech kutangaza kampuni ya uwekezaji ya nje iliyotumika kununua majengo mawili ya kifaransa kwa pauni milioni 12
- Jinsi familia ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta inavyomiliki kwa siri mtandao wa kampuni za nchi zenye nafuu ya ushuru kwa miongo kadhaa.
Nyaraka hizo zinafichua jinsi watu wengine wenye nguvu zaidi ulimwenguni - pamoja na wanasiasa zaidi ya 330 kutoka nchi 90 wanavyotumia kampuni za siri za pwani kuficha utajiri wao.
Lakshmi Kumar kutoka shirika la Think-tank la Marekani alielezea kuwa watu hawa "wanauwezo wa kuingiza pesa, kuzinyonya na kuzificha," mara nyingi kupitia kampuni za siri kuficha utajiri wao.

Nini maana ya kampuni zilizofunguliwa katika maeneo yenye nafuu ya kodi (offshore)
Pandora Papers zinafichua mitandao tata ya kampuni ambazo ziko nje ya mipaka, ambayo mara nyingi hutumika kuficha umiliki wa pesa na mali.
Kwa mfano, mtu anaweza kuwa na mali nchini Uingereza, lakini anamiliki kupitia mlolongo wa kampuni zilizo katika nchi nyingine, au "kampuni zilizofunguliwa katika maeneo yenye nafuu ya kodi.
Nchi ambazo kuna nafuu ya ushuru zina sifa zifuatazo;
- Ni rahisi kuanzisha makampuni
- kuna sheria ambazo huwa vigumu kubaini wamiliki wa makampuni
- Kuna kodi ndogo au hakuna kabisa kodi
Mara nyingi maeneo haya huitwa mahali penye nafuu ya ushuru au mamlaka ya usiri. Hakuna orodha dhahiri ya maeneo yaliyo na nafuu ya ushuru, lakini maeneo maarufu zaidi ni pamoja na Maeneo ya Ng'ambo ya Uingereza kama vile Visiwa vya Cayman na Visiwa vya British Virgin na pia nchi kama Uswizi na Singapore.
Je ni haramu kutumia nchi zenye nafuu ya kodi
Mianya katika sheria inaruhusu watu kisheria kuepuka kulipa ushuru kwa kuhamisha pesa zao au kuanzisha kampuni katika maeneo hayo, lakini mara nyingi huonekana kinyume cha maadili. The UK government says tax avoidance "involves operating within the letter, but not the spirit, of the law".
Pia kuna sababu kadhaa halali ambazo watu wanaweza kutaka kushikilia pesa na mali katika nchi tofauti, kama vile ulinzi dhidi ya kwa mashambulio ya jinai au kujilinda dhidi ya serikali zisizo imara.
Ingawa kuwa na mali za siri katika maeneo hayo sio haramu, kutumia mtandao tata wa kampuni za siri kuzungusha pesa na mali ndio njia nzuri ya kuficha mapato ya uhalifu.
Kumekuwa na wito mara kwa mara kwa wanasiasa kufanya iwe vigumu kukwepa ushuru au kuficha mali, haswa kufuatia uvujaji wa hapo awali kama vile nyaraka za Panama.
Lakini Bw Ryle alisema Nyaraka za Pandora zinaonesha kuwa "watu ambao wanaweza kumaliza usiri katika nchi zenye nafuu ya kodi ... nao wanafaidika nayo. Kwa hivyo hakuna motisha kwao kuimaliza".
Ni namna gani ilivyo rahisi kuficha fedha kwenye maeneo yaliyo na nafuu ya ushuru?
Unachotakiwa kufanya ni kuanzisha kampuni katika moja ya nchi yenye kiasi kikubwa cha usiri. Kampuni hiyo itabaki kuwa jina pekee, bila ofisi au wafanyakazi.
Ni gharama hata hivyo. Kampuni za wataalam hulipwa kuanzisha na kuendesha kampuni za hizo kwa niaba yako. Kampuni hizi zinaweza kutoa anuani na majina ya wakurugenzi waliolipwa, kwa hivyo haiwezi kufichua anayemiliki biashara hiyo.
Kiasi gani cha fedha hufichwa?
Haiwezekani kusema kwa kweli, lakini makadirio yameanzia dola trilioni 5.6 hadi dola trilioni 32, kulingana na ICIJ. Shirika la Fedha Duniani limesema matumizi maeneo yenye nafuu ya ushuru hugharimu serikali ulimwenguni hadi dola bilioni 600 kwa ushuru unaopotea kila mwaka.
Bi Kumar alisema ni mbaya kwa jamii yote: "Uwezo wa kuficha pesa una athari ya moja kwa moja katika maisha yako ... inaathiri elimu ya watoto, huduma za afya, na makazi.''
Je! Uingereza inafanya nini ?
Uingereza imekosolewa kwa kuruhusu mali kumilikiwa na kampuni zisizojulikana nje ya nchi.
Serikali ilichapisha rasimu ya sheria mnamo mwaka 2018 ambayo itahitaji wamiliki wa mali ya Uingereza kutangazwa. Lakini bado inasubiri kuwasilishwa kwa wabunge.
Ripoti ya bunge ya 2019 ilisema mfumo wa Uingereza unavutia watu "kama watatishaji fedha, ambao wanaweza kutaka kutumia mali kuficha pesa haramu".
Ilisema uchunguzi wa jinai mara nyingi "unazuiliwa" kwa sababu polisi hawawezi kuona nani mwishowe anamiliki mali.
Hivi karibuni serikali iliongeza hatari ya utakatishaji fedhakutoka viwango vya "kati" hadi "juu".
Inasema inakabiliana vikali na vitendo vya utakatishaji fedha na sheria kali na ufuatiliaji wa sheria, na kwamba itaanzisha rejista ya kampuni za nje zinazomiliki mali ya Uingereza wakati wa bunge utakaporuhusu.













