Fahamu sababu za wanawake wanaovutiwa zaidi kimapenzi na wanaume wahalifu?

Charles Manson

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Charles Manson
Iliyochapishwa

Kwa jamii nyingi wao ni katili lakini wanawake wengine huwaona wahalifu kama wanaume wazuri na wenye kupendeza, wanaume ambao wanaweza kuwabadilisha na kuwakomboa kupitia upendo wao, au watoto wanyonge ambao wanatakiwa kulindwa.

Mifano ya marafiki hawa wa kawaida wa kiume ni Mmarekani Charles Manson, ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha kwa kuamuru wafuasi wake kuua watu 9 karibu nusu karne iliyopita.

Yasiyojulikana karibu na uhalifu wa kutisha wa Sharon Tate na wengine 6 na dhehebu lililoongozwa na Charles Manson. Raia wa Norway Anders Behring Breivik, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 21 kwa mauaji ya vijana 77 mwaka 2011, na Josef Fritzl, kutoka Austria, alifungwa maisha tangu 2008 kumfungia na kumbaka binti yake mwenyewe kwa miaka 25.

Wakati wakiwa gerezani, wahalifu hawa na wengine mashuhuri wamepokea barua za mapenzi na hata pendekezo la ndoa kutoka kwa wanawake, ambao wengine waliwapenda sana au kuwatamani. Hakuna jibu moja kuelezea jambo hili la kushangaza na linalofanyika kwa wachache, lakini saikolojia ina jina la kuifafanua: hybristophilia, mvuto wa kijinsia kwa watu ambao "walifanya unyama au uhalifu, - kama vile ubakaji, mauaji au Ujambazi wa kutumia silaha ".

Ilikuwa mwanasaikolojia mashuhuri na mtaalam wa jinsia John Money ambaye ndiye aliyeanzisha neno hilo kwa mara ya kwanza miaka ya 1950. Pamoja na hayo alielezea jambo ambalo kwake lilikuwa la kiafya na ambalo liliathiri wanawake hasa wa mahusiano ya jinsia moja.

Kwanini mpenzi mhalifu?

El noruego Anders Behring Breivik, cumple una sentencia de 21 años por el asesinato de 77 jóvenes en 2011.

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Anders Breivik, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 21 kwa mauaji ya vijana 77 mnamo 2011, amejibu mamia ya barua za mwanamke anayejulikana kama "Victoria" ambaye anadai kuwa anampenda.

Kwa mujibu wa mwanasaikolojia Katherine Ramsland,mwandishi wa vitabu kuhusu wauaji katili, aliwahoji wanawake walioolewa na aina hii ya wahalifu na kubaini aina tatu za sababu zilizowasukuma kuvutiwa na aina hii ya watu. Wengi wao, kwa mujibu wa Ramsland, waliamini kuwa kwa mapenzi yao wangeweza kuwabadilisha wanaume hawa 'mashetani' na kuwaokoa.

"Wanavutiwa na wazo kwamba wanaweza kuwaokoa, na kwamba wanaweza kuwaondoa katika ulimwengu waliomo na kuwafanya kuwa wazuri," Torres Cazallas, mwanasaikolojia, mtaalam wa jinsia aliiambia BBC Mundo.

"Wanachanganya mvuto wa kuwaona na unyama kama huo na kwa nguvu kama hiyo na hamu ya kumfanya mwanaume abadilike. Kwa hivyo wamebaki na mtu ambaye ana uwezo wote (wa vurugu) lakini ambaye ataacha kuzitumia kwa sababu ya wao, kwamba wao ni wakombozi wao, "anaelezea.

Charles Manson detenido

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Charles Manson alikana tuhuma zake mpaka hatua za mwisho.

Wanawake, kulingana na Ramsland, wanavutiwa na wahalifu wakiongozwa na sababu ya mapenzi ya mama: wanahisi huruma au hata huruma kwa mtu aliyefungwa gerezani licha ya ukatili uliofanywa.

Kundi la tatu la wanawake, dogo zaidi, kulingana na Ramsland, linataka kupata umaarufu na kuzungumziwa na vyombo vya habari kuhusu mahusiano yao na wahalifu wa jinai mashuhuri, wengine kwa matumaini ya kutia saini kandarasi kwa ajili ya sinema au kitabu.

Charles Manson alikuwa mmoja wa wahalifu maarufu Marekani

Charles Manson

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Charles Manson

Mnamo mwaka 2015, wakati huo Manson alikuwa na umri wa miaka 80 na katika kifungo cha maisha, aliifuta harusi na mchumba wake wa miaka 27, Afton Elaine Burton, baada ya kubaini kuwa alipanga kufaidika na mhalifu huyo hasa kwa faida ambayo angepata kutokana na kuufichua mwili wake hadharani. baada ya kifo chake.

Msichana huyo aliwasiliana na muuaji kwa mara ya kwanza wakati akiwa na umri wa miaka 17, kulingana na jarida la Rolling Stone lililochapishwa mnamo 2013, baada ya kusoma nakala kadhaa ambazo Manson alikuwa amechapisha. Aliamua kuhamia Corcoran, California, mahali ambapo kuna gereza alilokuwa Manson alianza kumtembelea huko tangu mwaka 2007.

Maslahi ya ngono na kuvutiwa na wale wanaofanya uhalifu

Kuna wanawake ambao hupenda mapenzi na wahalifu kwa kuangalia tu picha zao au kusoma juu ya kile walichofanya kwenye vyombo vya habari. Kwanza wanaanza kuwaandikia barua na wengine huwapigia simu, kuwatembelea na hata kushiriki katika utetezi wao au kuwasaidia kifedha.

Wakati mwingine hakuna mawasiliano yoyote : uhusiano ni zaidi ya shauku ya kimapenzi. Katika mazingira mengine wanawake hawa wanaweza pia kuwa washirika wa wapenzi wao katika uhalifu . Jambo muhimu katika uhusiano huu wa kimapenzi, ambao hakuna mawasiliano yoyote ya mwili, ni sababu kuwa wanaume wanatumikia kifungo. Kwa hivyo wanawake wanaweza kukabiliwa na mvuto kwa mwanaume mwenye jeuri wakijua kuwa hawako hatarini kimwili.

Mwanasaikolojia Katherine Ramsland anazungumzia kuhusu jinsi wanavyoweza kuwa "wapenzi wazuri lakini kwa muda mfupi." ''Wengine hujua kuwa waume zao wana hatia, wengine husisitiza kuwa hawana hatia, ingawa kunakuwa na ushahidi wa wazi kuwa walitenda kosa.''

Josef Fritzl, de Austria, encerrado de por vida desde 2008 por el encierro y violación de su propia hija durante 25 años.

Chanzo cha picha, Police Niederoesterreich HO

Maelezo ya picha, Raia wa Austria, Josef Fritzl pia alipokea barua za mapenzi kufuatia kukamatwa kwake na kutiwa hatiani mnamo 2008 kwa kumfunga na kumbaka binti yake mwenyewe kwa miaka 25.

Ingawa waandishi kadhaa wanatoa ufafanuzi wa mvuto huu usio na mantiki, ukweli ni kwamba hakuna tafiti za kisayansi ambazo zinaelezea kwa nini hali hii hutokea zaidi miongoni mwa wanawake kuliko wanaume.