Chelsea v Man City: Nini atakachofanya Pep Guardiola kujaribu kushinda dhidi ya Thomas Tuchel?

Chanzo cha picha, BBC Sport
Ni mmoja wa makocha wawili waliomchachafya Pep Guardiola katika mechi tatu mfululizo - itakuwaje kama Thomas Tuchel atafanikiwa kupata ushindi mwingine wa nne mfululizo akiwa na Chelsea dhidi ya Manchester City Jumamosi hii?
Meneja huyo wa Chelsea hakuwahi kumfunga Guardiola wakati wote wakiwa wanafundisha nchini Ujerumani lakini akifuata nyayo za Jurgen Klopp punde tu mara baada ya kuwasili Stamford Bridge amefanikiwa kumfunga mara tatu mfululizo katika mashindano matatu tofauti katika kipindi cha wiki sita tu mwishoni mwa msimu uliopita.
Ushindi wa mwisho wa Tuchel ulikuwa kwenye fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya, yakiwa ni moja ya mafanikio makubwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Je Guardiola anapaswa kufanya nini kumkabili Tuchel?
"Hicho ndicho kila mtu anazungumzia pale City," anasema kiungo wa zamani Michael Brown.
"Nilikuwa kazini katika mechi waliyoshinda ya Carabao Cup dhidi ya Wycombe pale Etihad siku ya Jumatano, kuanzia mashabiki, wachezaji wengine wa zamani na watu wengine kwa ujumla, wote walikuwa wanasema' Pep atafanya nini mwishoni mwa wiki na je atafanya kitu cha tofauti?
"Inaonyesha namna walivyo yeye na klabu yake, kila mtu anatazamia Pep kupoteza mechi- yoyote anayeshinda basi hiyo ni habari kubwa.
"Ni mmoja wa makocha duniani, ambaye kama akifungwa, kila mtu atatafuta hata vitu vidogo kuangalia kwa nini amefungwza."
'Mafundi wawili wa mbinu kwenye soka
Tuchel na Guardiola, ni wakali wa mbinu katika uwanja, wanapenda kucheza mpira wa kumiliki na wa kasi, wana wachezaji bora kwenye vikosi vyao, na kuufanya mchezo wa Jumamosi kuwa wa kipekee.
"Kitu kinachosisimua ni kwamba Tuchel msimu huu ameachana na mfumo wa 3-4-3 ulioisaidia Chelsea kufika fainali na kutwaa ligi ya mabingwa Ulaya ," anasema mchezaji wa zamani wa Chelsea Pat Nevin.
"Wanaonekana kutumia zaidi kwa sasa 3-5-2 , ambapo Kai Havertz au Timo Werner akicheza karibu na Romelu Lukaku. Mtumo huu unafanya vyema kwenye viungo kukiwa na N'Golo Kante, Jorginho na Mateo Kovacic.
"Tuchel na Guardiola kwakweli ni watalaam wa mbinu za mchezo kwa sasa linapokuja suala la kuusoma mchezo.
"Kwa sasa maamuzi anayofanya Tuchel yanamlipa na anaonekana ynaonekana kuleta utofauti kwa haraka. Dhidi ya Spurs mwishoni mwa wiki alimuingiza N'Golo Kante wakati wa mapumziko jambo lililobadilisha kila kitu
"Kwa sasa anakwenda kupambana na Pep tena mchezo mwingine mkubwa," anasema Pat Nevin.

Chanzo cha picha, Getty Images
Nini atakachofanya Guardiola ?
Mfumo wake wa kutotumia mshambuliaji halisi wa kati huenda Guardiola akautumia jumamosi lakini alifanya tofauti kila alipokutana na Tuchel msimu uliopita, lakini bila mafanikio.
Ingawa aliwapumzisha wachezaji kadhaa kwenye nusu fainali ya FA Cup na kubadioli mfumo wake kutoka 4-3-3 kwenda 3-5-2 walipokutana tena kwenye ligi, lakini hali ilikuwa mbaya zaidi huko Porto, kwenye ligi ya mabingwa Ulaya.
Akijaribu kutafuta namna ya kushinda Chelsea imekuwa ikimpa wakati mgumu Guardiola ambaye aliamua kutotumia kiungo wa ulinzi kwenye fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Pep alitumia akili kule Ureno akitaka kutawala mchezo kwa kumiliki sana mpirana kuwafanya viungo wake wacheza zaidi sehemu ya mbele," anasema Brown.
"Ndiyo maana hakutaka kucheza na kiungo mzuiaji, kwa sababu alifikiri Ilkay Gundogan anaweza kusogea mbele pia, lakini mambo hayakwenda sawa, - mipira ya haraka ya Chelsea iulikuwa bora zaidi.
"Kwa kuwa ugenini Jumamosi hii, anaweza kufikiria kucheza na kiungo mzuiaji, anaweza kuwa Fernandinho ama Rodri.
"Mbele anaweza kumtumia Ferran Torres kama mshambuliaji akitarajia kusumbuana na mabeki wa Chelsea..
"Angalia eneo la mabeki John Stones na Aymeric Laporte wote ni majeruhi. Kumchezesha yoyote ni kucheza patapotea, kwa hivyo kusalia na mabeki wanne inaweza kuwa jambo jema kwa Pep.
"Anajua pia kuwa City ina mechi ngumu wiki hii - watakutana na Paris St-Germain Jumanne Tuesday baadae Jumapili ijayo weatawavaa Liverpool.
"Hili linaweeza kuathiri uchaguzi wake wa kikosi, lakini nafikiri atajiegemeza zaidi kwenye mchezo huu dhidi ya Chelsea. Anajua utakuwa mgumu, lakini hataihofia Chelsea - City itajitoa kusaka ushindi Jumamosi.














