Mohammed Ata: Jinsi mtu huyu alivyotekeleza shambulizi la 9/11

Chanzo cha picha, Getty Images
Septemba 11, 2001 ilianza kama siku ya kawaida. Lakini kufikia saa nne asubuhi, siku hii ilikuwa imegeuka kuwa shambulio hatari zaidi la kigaidi katika historia ya ulimwengu na shambulio baya zaidi kwa Amerika baada ya Bandari ya Pearl.
Wakati ndege mbili zilipopiga minara miwili ya Kituo cha Biashara Ulimwenguni huko New York, watu 2606 waliuawa katika shambulio hili.
Watu wengine 206 waliuawa katika shambulio la Pentagon na 40 zaidi katika jaribio la utekaji nyara wa ndege huko Pennsylvania. Majina ya jumla ya watu 2983 ambao walipoteza uhai wao katika mashambulio haya yameandikwa katika jengo la kumbukumbu ya 9/11 lililojengwa huko New York.
Hili halikuwa shambulio la kwanza la kigaidi kwenye Kituo cha Biashara Ulimwenguni mwaka 1993.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika kitabu mashuhuri The Only Plane in the Sky, the Oral History of 9/11, Garrett M. Graf anaandika, "Zaidi ya watoto 3000 walipoteza wazazi wao katika shambulio la 9/11. Kati ya hao, karibu watoto 100 walizaliwa miezi kadhaa baada ya mashambulio na hawakupata nafasi ya kuwaona baba zao.

Chanzo cha picha, AVID READER PRESS/SIMON & SCHUSTER
Anaandika, "Mshtuko uliosababishwa na tukio hilo bado haujafutwa kutoka kwenye kumbukumbu ya kila Mmarekani. Tukio hili lilitokea katika eneo ambalo lilionekana kuwa mahali salama zaidi duniani."
Wosia wa Ata Mohammed
Mnamo Septemba 11 mwaka 2001, Mohammed Atta alifungua macho yake saa kumi alfajiri katika chumba namba 233 cha Hoteli ya Comfort Inn huko Portland, Maine.
Mara tu alipoamka, akampigia simu mwenzake Abdul Aziz Al Omari, ambaye alikuwa akikaa katika hoteli moja. Kisha alioga. Alivaa shati yake la bluu na suruali nyeusi. Kisha akafungua wosia wake kwenye kompyuta yake ndogo ambayo alikuwa ameandika mwezi Aprili mwaka 1996.
Vitu viwili katika wosia vilikuwa vya kushangaza kidogo. Martin Amis anaandika katika kitabu chake 'The Plain Plain', "Ata aliandika katika wosia wake, sitaki watu wapige kelele kwenye mazishi yangu, kwa sababu Mungu anataka niwe kimya kabisa kwenye hafla kama hiyo. Mtu atakayeuosha mwili wangu baada ya kifo avae glavu na asiguse sehemu zangu za siri. Pia sitaki mjamzito yeyote au mtu ambaye si msafi kuniaga siku ya mwisho. "
Hakuna maagizo yoyote aliyoyatoa ambayo yangeweza kutekelezwa kwani hakuna mtu aliyemuaga na hakuna mtu aliyemuosha au kugusa sehemu zake za siri.
William Arkin, mwandishi wa 'On That Day the Definitive Time Line' anaandika, "Atta na mwenzie wake walitoka saa 5:33 jioni. Vyumba vililipiwa kwa kadi ya malipo ya ATM ilitumia kutoa pesa, kula pizza, na kufanya manunuzi huko Walmart . FBI inaamini Ata pia alitembelea Kituo cha Biashara Ulimwenguni siku hiyohiyo akiwa ndani ya gari lake. "

Chanzo cha picha, Getty Images
Mashine za ukaguzi hazikubaini chochote
Baada ya kutoka nje ya hoteli hiyo, Ata na mwenzake Abdul Aziz Al Omari walipanda gari la kukodisha la Nissan Altima la bluu na kufika kwenye maegesho ya uwanja wa ndege ndani ya dakika saba. Wakati wa kuingia kwenye maegesho, usalama wa uwanja wa ndege ulipiga picha yake. Ata na mwenzake walikaguliwa na maafisa usalama saa 11:45 jioni.
Ata alikuwa amebeba begi jeusi, na mkononi mwa Amari kulikuwa na kamera au kitu kama kifaa cha kurekodia ambacho alikuwa amekishika kwa mikono miwili. mashine za ukaguzi hazikugundua chochote kutoka kwao

Chanzo cha picha, Getty Images
William Arkin anaandika, "Saa sita kamili Ata na mwenzake walipanda ndege ya US Airways namba 5930. Kulikuwa na abiria wanane tu kwenye ndege hiyo iliyo na uwezo wa kubeba abiria 19.
Ata alipewa kiti katika safu ya nambari 9. Yeye na Al Omari ndio walikuwa abiria wa mwisho kupanda ndege hiyo.
Katika dakika 45 alifika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Boston Logan, kutoka mahali alipopanda Ndege ya Nambari 11 ya AA iliyokuwa ikielekea Los Angeles.
Mbali na abiria 81, wahudumu 9 walikuwa ndani ya ndege hiyo. Ndege hiyo ya Boeing 767 ilipangiwa kuruka saa 1.59 jioni.

Chanzo cha picha, Getty Images
Akiwa mtoto, alikuwa na aibu na mtiifu
Ata alizaliwa mnamo Septemba 1 mwaka 1968 huko Kafr El Sheikh, Misri. Familia yake na marafiki wanasema kwamba alikuwa na aibu sana akiwa mtoto.
Katika makala ya Septemba 30, 2001 katika jarida la Time lililoitwa 'Ata'az Odessey', John Claude anaandika, "baba wa Ata anasema kwamba akiwa mtoto alikuwa anapenda kucheza chess na alichukia michezo ya vurugu.
Alikuwa urefu wa futi 5 na inchi 7 na alikuwa mwembamba sana hivi kiasi cha baba yake kumuita 'Bulbul'. "
"Baada ya kupata shahada ya kwanza ya uhandisi wa usanifu kutoka Chuo Kikuu cha Cairo, alihamia Hamburg, Ujerumani kwa masomo zaidi. Kuanzia katikati ya miaka ya 90, Ata mara nyingi alikuwa akikosekana chuoni kwa muda mrefu. Sababu ya hili alikuwa akisema kwamba alikuwa amekwenda Saudi Arabia kutekeleza Hija. Aliporudi, alikuwa amefuga ndevu.
Vyanzo vya ujasusi vya Ujerumani vinaamini kuwa wakati huu Ata alikuwa amewasiliana na watu wanaohusishwa na shughuli za kigaidi.
Mafunzo ya kurusha ndege
Terry McDormatt anaandika katika kitabu chake 'Perfect Soldiers Who They Were Why They Did It', "Baada ya kurudi , Ata aliomba pasi mpya ingawa hati yake ya kusafiria ya zamani ilikuwa haijaisha muda.
Ilikuwa kawaida kufanya hivyo katikati kwa sababu kwa kuharibu pasi ya zamani, walitaka kuharibu ushahidi wa wapi walikuwa wameenda. "
Aliwasili Newark mnamo Juni 3 mwaka 2000 kutoka Prague kwa visa ya miezi sita ya utalii, na ndani ya mwezi mmoja, pamoja na wenzake, walikuwa wameanza mazoezi ya kurusha ndege katika chuo cha usafirishaji wa anga, Huffman Aviation International huko Venice.
Pamoja walilipa shule ya Huffman karibu $ 40,000 kwa mafunzo haya ya miezi minne. Mnamo Desemba 21, 2000, Ata na mwenzake, Al Shehi, walipokea leseni yao ya majaribio.
John Claude aliandika kwenye jarida la Time, "Kulikuwa na uhamishaji wa pesa wa namna mbili kwa akaunti ya Ata siku 10 kabla ya Septemba 11. Mnamo Septemba 7, Ata na mwenzake Al Sheahi na mtu mwingine huko Oyster Bar na Grill huko Hollywood, Fla. Ata alikuwa mtu tu kati ya wale watatu ambao hawakunywa pombe. Badala yake, waliendelea kunywa maji ya matunda. "

Chanzo cha picha, Getty Images
Mhudumu wa ndege alitoa taarifa kwa simu kuhusu ndege kutekwa nyara
Wakati ndege ya AA 11 ilipopaa, kwa dakika chache zilizofuata, alifuata maagizo kutoka Udhibiti wa Trafiki wa Boston Airroute, lakini baada ya dakika 8.13, wakati Atta na washirika wake walipodhibiti ndege, aliacha kufuata maagizo yao.
William Arkin anaandika, "Kama ilivyoripotiwa na mashuhuda , Ata aliamua kutumia kisu na vurugu kumdhibiti rubani. Saa 2:18 asubuhi, mhudumu wa ndege Betty Ong alipiga simu kwa Shirika la Ndege la Marekani, Kituo cha Uhifadhi cha Kusini Mashariki, akishuku utekaji nyara.
Alisema kwamba anapiga simu akiwa ameketi nyuma ya ndege. Simu hii ya binti ilidumu kwa dakika 25. Alisema kwamba hakuna majibu ya ujumbe wake kutoka kwa chumba cha rubani na kiti nambari 9B katika daraja la wafanyabiashara Lakini Daniel Levine ameketi akiwa amedungwa kisu. "
Levine alihudumu katika jeshi la Israeli kwa miaka michache. Inakisiwa kuwa huenda alijaribu kumzuia mtekaji huyo kukaa mbele yake lakini hakujua kwamba mtekaji nyara mwingine alikuwa amekaa nyuma yake.
Pia alisema kwamba mtu anayeketi kwenye kiti cha 10B kwa sasa yuko ndani ya chumba cha rubani. Saa 2:26 asubuhi, ndege hiyo ghafla ilitengeneza pembe ya digrii 100 na kuelekea New York City. Mhudumu wa ndege Ong aliripoti kwamba ndege hiyo ilikuwa ikipanda na kushuka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ndege iligonga jengo la Kaskazini saa 2.46 asubuhi
William Arkin anaandika zaidi, "Wakati huo huo, Mohammad Ata, akiwa amekaa kwenye kiti cha rubani, alijaribu kuhutubia abiria kupitia mfumo wa intercom ya ndege. Lakini akabonyeza kitufe kisicho sahihi. Kwa hivyo ujumbe wake ulisikika kwenye chumba cha kudhibiti hapo chini. Ong aliendelea Wakati huo huo," Mhudumu mwingine wa ndege, Sweeney, aliripoti kwamba ndege hiyo ilikuwa ikitoa taarifa potofu kwamba kulikuwa na dharura ya kiafya katika daraja la kwanza, kwa hivyo ndege ililazimika kushushwa. Ilikuwa hivyo. "
Wakati huo huo, muhudumu wa ndege hiyo Sweeney alisema, ndege hiyo inashuka kwa kasi. Ninaweza kuona maji. Majengo pia yanaonekana. Baada ya muda akasema tena, "Ee mungu wangu, tumeshuka sana." Wakati huo huo sauti kubwa sana ilisikika na Kituo cha Operesheni cha Marekani kilipoteza mawasiliano naye. "
"Saa 2:46 asubuhi Ndege AA iligonga katika Mnara wa Kaskazini wa Kituo cha Biashara Ulimwenguni kati ya ghorofa ya 93 na 99. Karibu galoni 10,000 za mafuta ya ndege yalitoka kwenye ndege yalimwagika kwenye ghorofa hizo.
Ndege nyingine iligonga jengo la Kusini
Dakika 17 baadaye, saa 3:03 asubuhi, ndege nyingine iliyotekwa nyara, Ndege nambari 175, iligonga Mnara wa Kusini wa Kituo cha biashara Ulimwenguni. Ndani ya saa 1 dakika 42, majengo yote mawili ya ghorofa 110 yaliporomoka.
Ndege nyingine ilipiga mwisho magharibi mwa Pentagon, na kusababisha sehemu ya jengo hilo kuanguka. Jaribio pia lilifanywa kuiteka nyara ndege ya United Airlines nambari 93, lakini abiria waliokuwamo ndani ya ndege hiyo walizuia jaribio hilo. Ndege ilianguka Pennsylvania saa 4.03 asubuhi na kila mtu aliyekuwamo alipoteza maisha.












