Sirajuddin Haqqani: Kiongozi wa kundi 'katili' aliyeteuliwa kuwa waziri katika serikali ya Taliban

Chanzo cha picha, FBI
Taliban imetangaza serikali yake ya mpito nchini Afghanstan na kuitangaza Afghanistan 'Milki ya Kiarabu'.
Kama Mulla Mohammad Hassan Akhund ni Waziri Mkuu wa serikali, basi Mulla Abdul Ghani Baradar atakuwa naibu Waziri mkuu, na Mulla Abdul Salam Hanafi ametangazwa kuwa Naibu Waziri Mkuu.
Hatahivyo, mmoja wa watu wanaozungumziwa zaidi ni Sirajuddin Haqqani, kiongozi wa mtandao wa Haqqani.

Ameteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani katika serikali ya Akhund.
Msemaji wa Taliban Zabiullah Mujahid alisema kuwa uteuzi wake ni mpango wa muda. "Tutafanyia kazi mpango wa kuunda serikali yote " alisema.
Baada ya Taliban kuuteka mji mkuu Kabul tarehe 15 Agosti, katika kipindi cha siku chache umeshuhudiwa uundwaji wa serikali ya Taliban.

Kulingana na mwandishi wa BBC Sikandar Kirmani, afisa wa Taliban Ahmadullah Wasim amesema kwamba Afghanistan kwa sasa ni "Milki ya Kiislamu ya Afghanistan."
Msemaji wa Taliban amesema : "Baraza la Shura (baraza la mawaziri ), bado litaangalia suala hili na baadaye litaamua jinsi watu watakavyoshiriki katika serikali hii."
Wapiganaji wa kikabila wa The National Resistance Front wamepinga madai ya Taliban ya uvamizi na kutangaza vita. Siku iliyofuata, Taliban ilitangaza serikali.
Msemaji wa Taliban pia alifanya mkutano na waandishi wa habari Jumatatu. Hata wakati huo, maswali yaliibuka kuhusu waliounda baraza hilo, lakini msemaji huyo alikataa kujibu maswali kuihusu serikali mpya ya Taliban.
Haqqani anayesakwa na Marekani

Chanzo cha picha, FBI
Huyu ni Haqqani yule ambaye kikundi chake kilifanya, mashambulio ya kikatili miaka 20 iliyopita. Ni rais wa kikundi chenye sifa mbaya chenye itikadi kali kinachoitwa Mtandao wa Sirajuddin Haqqani chenye ushirika na Taliban.
Mnamo mwaka 2017, kikundi chake kilifanya shambulio la bomu lililowekwa ndani ya lori ambalo liliwauwa zaidi ya watu 150.
Kikundi hiki pia kina uhusiano wa karibu na al-Qaeda. Marekani imeuorodhesha mtandao wa Haqqani kama "kikundi cha ugaidi."
Kulingana na maelezo ya FBI kuhusu mtandao wa Haqqani, ni kikundi kinachosakwa na shirika hilo.
Haqqani katika kitengo hiki kinatafutwa kuhojiwa kuhusiana na shambulio la 2008 dhidi ya hoteli mjini Kabul.
Shambulio hilo liliwauwa watu sita, akiwemo raia wa Marekani.

Chanzo cha picha, DAUD YARDOST / AFP VIA GETTY IMAGES
Maelezo yake yanasema kuwa mtandao wa Haqqani unaaminiwa kufanya mashambulio dhidi ya vikosi vinavyoongozw na Marekani pamoja na vikosi vya NATO.
Pia inaaminiwa kwamba mtandao wa Haqqani ulitekeleza shambulio la kujitoa muhanga la mwaka 2008 dhidi ya rais wa zamani wa Afghanistan Hamid Karzai.
Mtandao wa Haqqani pia ulilaumiwa kwa mashambulio ya Septemba 2, 2011 dhidi ya ngome za NATO karibu na ubalozi wa Marekani mjini Kabul.
Watu wanane, wakiwemo maafisa wanane wa polisi waliuawa .
Maelezo ya FBI yanasema Haqqani ana urefu wa futi 5 na inchi 7.
Haqqani alisema kuwa anaishi nchini Pakistan na kwamba kikundi chake kinaendesha harakati zake kwenye mpaka kati ya Pakistan na Afghanistan.
Ana umri wa takriban miaka 45.
Mwaka jana, wafuasi wa Haqqani waliandika makala ya gazeti la New York Times, " kila siku kwa zaidi ya miongo minne, watu wa Afghanistan wamekuwa wakipoteza maisha yao ya thamani ."
"Kila mtu hapa amempoteza mpendwa wake . Kila mtu amechoshwa na vita. Ninaamini mauaji haya yanapaswa kukoma."
Marekani pia imevitaka vikosi vinavyoipinga Taliban nchini Afghanistan, na jamii ya kimataifa kutoitambua serikali mpya iliyotangazwa na wanamgambo wa Kiislamu Jumanne.
Wapiganaji wanaoipinga Taliban katika jimbo la Banshir wamesema kuwa serikali mpya ni "haramu".













