Filicudi na Stromboli: Kwanini wapendanao huenda 'kuhiji' katika visiwa hivi vya Italia

Chanzo cha picha, Getty Images
Filicudi na Stromboli ni visiwa vyenye mandhari ya kuvutia, vikipatikana katika katika bahari ya Pacific katika taifa la Ulaya ya Italia.
Visiwa hivi viwili vimeundwa na vilima vya volcano na wakati mwingine hupata milipuko midogo lakini milipuko haitokei kwenye vilima vyote.
Harugu ya mimea Cestrum nocturnum yenye manukato ya kuvutia iliyotanda kwenye visiwa hivi inasemekana kuwasaidia watu kupumzika, kukabiliana na msongo wa mawazo na kupunguza hali ya mchoko na wasi wasi wanaokuwa nao katika pilikapilika za maisha ya kila siku.

Chanzo cha picha, Getty Images
Unapotembelea visiwa hivi harufu ya mimea ya maua ya jasmini inayotoa harufu ya kuvutia husasan nyakati za usiku
Wenyeji wa visiwa hivi vinavyopatikana katika katika Sicily, wamekuwa wakiwaelezea waandishi wa habari kuwa sio visiwa vya kawaida, kwani huchochea msisimuka wa mapenzi hususan kwa wapendanao wanapovitembele kujivinjari kwa mapumziko.
Wanasema wanajivunia kuwa katika visiwa hivyo wanavyoviita "mtoto wa volkano," na wanajivunia nguvu za mmea, ambao wanasema unaongeza nguvu za kiume. Mara nyingi hupenda kutoa mzaha kwamba kisiwa chao "kila wakati kina joto."
Unapotembelea visiwa vya Stromboli and Filicudi tarajia kuendeshwa kwenye mawimbi masafi yanayong'ara ya rangi ya blu yenye mvuto.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wavuvi wenyeji wa visiwa hivi wanafahamika kwa kuwatembeza wenzi wanaovitembelea hadi kwenye "mapango ya uzazi."
Na kama wewe ni mwanamke au msichana ambaye hujapata mchumba, wavuvi katika visiwa hivi basi watakutembeza kwenye boti hadi kwenye miamba yenye maumbile yasiyo ya kawaida ambayo inasemekana unapoyagusa hukupatia bahati katika kutafuta mpenzi.
Ni eneo lenye asili isiyo ya kawaida. Kuna kijiji kimoja tu uvuvi, Pecorini a Mare, chenye nyumba ziliopakwa rangi, bandari mbili ndogo na barabara moja pekee inayozunguka kisiwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Tangu nyakati za kale kulikuwa na Imani kwamba mmea wa cestrum nocturnum ambao ni wa spishi ya Jasmini umekuwa ukichukuliwa kama mmea unaoleta msisimko wa hisia za kujamiiana na wenyeji wanasema ''Wapenzi wanaokutana kwenye visiwa hivi ambao hawajapata wenzi wao huishia kupendana na kusherehekea harusi yao au kuzaliwa kwa mtoto''
Cestrum nocturnum, mmea unaomea maua ya kijani na meupe, ambayo huchanua wakati jua linapochomoza, ambao hutoa harufu inayoamsha ari ya ngpno, unaomea katika kisiwa cha Stromboli, pia umeibua tetesi kuwa husaidia wenzi kupata ujauzito.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kulingana na taarifa ya CNN, visiwa hivyo vimekuwa maeneo ya'' hija ya ngono'', kulinga na wenyeji kwasababu ya''uwezo wa kuamsha ari ya ngono'' , pamoja na kutoa mazingira ambayo "huwatia wenzi kukutana kimwili ."
"Wanandoa waliooana haribuni wanaotaka kupata mtoto wanasemekana kutembelea kwenye visiwa hivyo kwa wingi kutoka maeneo mbali mbali ya dunia ili kupata mtoto, huku vijana wa kike wenye matumaini ya kupata mchumba wakifika huko kufanya maombi ya kimya kimya mbele ya miamba yenye maumbile ya ajabu ."

Chanzo cha picha, Getty Images
Wavuvi huwawatembeza wageni wageni ndani ya mitumbwi na kuwapeleka kwenye maeneo maarufu ya bahari, ikiwa ni pamoja na ''pango la wapenzi'' ambapo inasemekana wapenzi wanapoingia ndani ya pango hilo, wanakuwa na uwezekano mkubwa wa kupata ujauzito.
Visiwa hivi pia huwavutia mashabiki wa kupanda miamba na ni makao ya mijusi nyoka wa kipekee ambao huwavutia sana wageni wanaovitembelea.
Hizi ni baadhi ya picha za kuvutia za visiwa vya visiwa vya ''hija ya wapenzi'' vya Italia.

Chanzo cha picha, Getty Images












