Vita vya Afghanistan: Fahamu matukio makuu ya Afghanistan tangu shambulio la balozi za Tanzania na Kenya

Chanzo cha picha, AFP
Hatimaye kundi la wapiganaji wa Taliban limefanikiwa kuuteka mji mkuu wa Kabul - mji mkuu wa taifa la Afghanistan kufuatia kuondoka kwa majeshi ya Marekani nchini humo.
Wapiganaji hao waliwasili katika mji mkuu wa Kabul na kulazimisha utawala uliokuwepo kutoroka.
Lakini je uhasama kati ya majeshi ya Marekani na wapiganaji wa Taliban ulianzia wapi?
Huu hapa msusuru wa matokeo makubwa ya Afghanistan kuanzia mwaka 1998.
1998: Baada ya shambulio la al- Qaeda katika ubalozi wa Marekani mjini na Nairobi na Dar es Salaam, serikali ya taifa hilo ilianza harakati za kumsaka kiongozi wa kundi la al Qaeda Osama bin Laden.
2000: Katika upelelezi wake Marekani ilibaini kwamba kiongozi huyo wa al Qaeda alikuwa mafichoni nchini Afghanistan na hivyo basi ikaliomba kundi la Taliban ambalo wakati huo ndilo lililokuwa likiongoza taifa la Afghanistan kumpeana kiongozi huyo. Taliban lilikataa katakata kufanya hivyo na kupuuzilia mbali onyo lililotolewa na Marekani na mshirika wake Uingereza dhidi ya utawala wake.
2001: Majeshi ya Taliban yalifurushwa nchini humo na muungano wa, majeshi ya Kaskazini { Northern Alliance} yalioshirikiana na majeshi ya Marekani. Baada ya Taliban kutoroka , Osama bin laden alijificha katika milima ya Tola bora .
Septemba. 11, 2001: Watekaji wa ndege walizielekeza ndege nne za kibiashara na kugonga majumba mawili marefu ya kibiashara nchini Marekani mjini New York, na lile la Pentagon nje ya mji wa Washington D.C. na katika uwanja mmoja wa Pennsylvania, na kuuwa maelfu ya watu. Siku chache baadaye, maafisa wa Marekani walisema kwamba Osama bin Laden, raia wa Saudia aliyekwenda mafichoni ndiye aliyekuwa mshukiwa mkuu wa shambulio hilo.
Desemba. 22, 2001: Hamid Karzai, mwandani wa majeshi hayo aapishwa kuwa kaimu kiongozi wa Afghanistan. Karzai aungwa mkono na Marekani na baada ya miezi michache atangazwa kuwa rais rais wa serikali ya miezi 6.
2007: Serikali ya Afghan na Majeshi ya NATO yathibitisha kwamba kamanda wa Taliban Mullah Dadullah ameuawa wakati wa operesheni ilioongozwa na Marekani kusini mwa Afghanistan.
2009: Rais Obama atangaza mikakati mipya ya vita vya Afghanistan ambayo itaongeza wanajeshi zaidi ya wale 17,000 nchini humo ili kuwafunza wanajeshi wa taifa hilo katika vita dhidi ya kukabiliana na wapiganaji wa Taliban .
2011: Wanajeshi wa Marekani wateka ardhi ya nyumba moja huko Abbottabad, Pakistan, na kumuua kiongozi wa kundi la al-Qaida leader Osama bin Laden tarehe 2 mwezi Mei.
2012: Rais Karzai avitaka vikosi vya Marekani kuondoka Afghanistan na kurudi katika kambi zake baada ya wanajeshi wa Marekani kuwaua raia 16 ndani ya nyumba zao.
2014: Ashraf Ghani ataganzwa kuwa rais mpya wa Afghanistan mnamo mwezi Septemba baada kupiga kura kwa mara ya pili na serikali ya kugawanyana mamlaka kati ya na mpinzani wake Abdullah Abdullah yabuniwa . Mwezi Disemba vikosi vya Nato vyaondoka vile vya Marekani vyasalia nyuma kuwafunza wanajeshi wa Afghnaistan.
2021: Muda mfupi baada ya kuapishwa kuwa rais mpya wa Marekani , Joe Biden atangaza kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.
2021: Mei Mosi - Vikosi vya Marekani vyajiondoa katika kambi kubwa ya Afghanistan ya Kandahar, ambao ndio mji wa pili kwa ukubwa. Wapiganaji wa Taliban waingia na kuiteka wilaya za Wardak karibu na Kabul kabla ya kuingia mji mkuu wa Kabul huku rais wa taifa hilo akitoroka ..













