'Mashambulizi Gaza yamekuwa janga' shirika la madaktari wasio na mipaka limeeleza

Iliyochapishwa

Mashambulizi makubwa ya mabomu Gaza wiki iliyopita yamekuwa "janga" anasema Helen Ottens-Patterson, Mkuu wa misheni huko Gaza kutoka shirika la madaktari wasio na mipaka(MSF).

Anasema barabara, maji, usafi wa mazingira na miundombinu mingine imeharibiwa, na kuwa kikwazo kwa mfumo wa afya.