Real Madrid: Je Zinedine Zidane anapata heshima yake kwa mafanikio ya kombe la klabu bingwa ?

Chanzo cha picha, Getty Images
Huwezi kushinda mataji matatu ya kombe la klabu bingwa Ulaya , mataji mawili ya Ligi ya La liga na mechi 13 kati ya 14 za muondoano Ulaya iwapo wewe sio mkufunzi mzuri.
Wakati mwanahabari wa Ufaransa Julien laurens alipopokea wasifu (CV) ya ukufunzi ya Zinedine Zidane ni vigumu kukataa.
Licha ya kushinda mataji saba makuu katika kipindi chake cha miaka minne na nusu kama mkufunzi wa Real Madrid, raia huyo wa Ufaransa anaendelea kuonekana na baadhi kama mkufunzi ambaye hana maarifa bali ni mtu mwenye bahati.
Kabla ya mechi ya nusu fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya wakati Real Madrid ikiwa katika sare ya 1-1, BBC inachunguza ni kwanini hajapatiwa heshima licha ya mafanikio yake yote.
Zidane ni miongoni mwa makocha watatu waliofanikiwa kushinda makombe matatu ya Yuropa na matatu ya klabu bingwa katika CV zao lakini wawili wengine Bob Paisley na Carlo Ancelotti hawakushinda mfululizo.
Katika msimu wake kamili wa kwanza akisimamia Rea Mardid, alishinda kombe la La la liga na lile la klabu bingwa Ulaya { Ikiwa ni mara ya mwisho kwa klabu hiyo kufanya hivyo tangu mwaka 1958}, pamoja na ushindi wa kombe la klabu bingwa duniani huku akishinda asilimia 70 ya mechi alizosimamia.
Msimu wake wa pili akiwa meneja wa klabu hiyo alifanikiwa kushinda kombe la La Liga mwaka uliopita na Zidane huenda akamaliza msimu huu kwa kushinda taji la ligi na kombe la klabu bingwa Ulaya.
Kabla ya mechi ya siku ya Jumatano dhidi ya Chelsea , mara yake ya mwisho kushindwa katika mechi 14 za klabu bingwa Ulaya ilikuwa jumla ya magoli 4-2 dhidi ya Manchester City katika michuano ya msimu uliopita.
Wapinzani wake hata hivyo wanataka kukandamiza mafanikio yake , wakisema kuwa alipata kikosi kilichokuwa thabiti alipopatiwa usimamizi wa timu hiyo bila uzoefu wowote wa kuwa mkufunzi hususan wakati ambapo mchezo wa Christiano Ronaldo ulikuwa wa kiwango cha juu akihusika katika kufunga magoli mengi.
Na baadaye kuna mifano ya ndani ya uwanja ambayo imempendelea raia huyo wa Ufaransa na kikosi chake.
Sare na baadaye upigaji wa penalty katika mechi kati ya klabu yake na Atletico Madrid katika fainali ya 2016, robo fainali ya kombe la klabu bingwa 2017 dhidi ya Bayern Munich ambapo timu hiyo ya Ujerumani ilicheza bila mchezaji mmoja ambaye alikuwa amepatiwa kadi nyekundu.
Katika mikondo yote miwili , walikosa penalti katika mkondo wa kwanza na wakanyimwa penalti ya wazi katika mkondo wa pili, huku Mohammed Salah akipata jeraha katika mechi yao dhidi ya Liverpool mbali na kukanganyikiwa kwa kipa Loris Karius katika fainali ya 2018.
Katika mafanikio yake Real Madrid, Zidane hapingi kuwa na bahati.

''Nakubali kwamba huenda nina bahati'', aliambia maripota mwezi Januari 2020.
''Nimekuwa na bahati katika maisha. lazima nishukuru na kufanyia kazi hilo. Iwapo unadhani nina bahati pia hio ni sawa, sio tatizo''
''Zidane hawezi kudhibiti bahati, lakini anaweza kudhibti jinsi timu yake inavyocheza uwanjani'',alisema.
Katika mazungumzo kuhusu kombe la Yuropa, anaonekana ni mjuzi zaidi ya sifa anazopewa.
''Kuna vitu vingi ambavyo Zidane hufanya vinavyobadili mechi '', anasema mwandishi wa kandanda nchini Uhispania Guillem Balague.
Mambo madogo kama vile dhidi ya Liverpool katika robo fainali ya kombe la klabu bingwa mkondo wa pili, kukiri kwao kwamba hawakuwa wakicheza vyema.
Liverpool wapo katika mkondo wao wa lala salama , huku kiwango cha mchezo wao ukiendelea kushuka.
Klopp alizungumza jinsi mchezaji wa ziada alivyobadili umbo na kasi ya mechi .
''Zidane alifanya uamuzi mzuri''
Laurens anaendelea na mandhari, akisema kwamba wakati Zidane anapobadili mwenendo wa mechi , hapongezwi kama vile wakufunzi wengine wanavyopongezwa.
''Kwanini anapigwa kofi la nyuma na kuitwa shabiki wa timu? Huu ni upuzi'', anaongezea.
Huenda asifikie kiwango cha Johan Cruyff ama Arigo Sacchi ama hata Pep Guardiola katika kuimarisha kandanda, lakini wakati Joao Cancelo anapocheza vizuri kutoka beki na kuingia katika kiungo cha kati watu husema ni kipaji kutoka kwa Guardiola .
Wakati Mendy ;anapoifanyia Real Madrid kazi kama hiyo hakuna mtu anayesema kwamba Zidane alikuwa mzuri.
''Huu ndio msimu mzuri katika uongozi wa Zidane'', aliongeza Balague.
Ukosefu wa Sergio Ramos na Dani Carvajal kupitia majeraha, hatua ya Ronaldo kujiunga na Juventus msimu uliopita ulimaanisha kwamba alilazimika kutumia wachezaji waliokuwepo.
''Wakati Zidane anapozungumza wachezaji humsikiliza''
Ancelloti , ambaye alikuwa akisaidiwa na Zidane katika klabu ya Real 2013-14, wakati mmoja alisema pale ambapo talanta ya ukufunzi wa raia huyo wa ufaransa ipo.
''Yeye Zidane ana vigezo vyote vya kuwa mkufunzi mzuri: haiba, utu na uzoefu. Wakati Zidane anazungumza, wachezaji wanamsikiliza, "alisema Muitaliano huyo.
Pia inaelezea kwanini Zidane ni bora kwa Real , klabu ambayo kihistoria imenunua wachezaji wakiwa katika viwango vya juu vya uchezaji wao badala ya kujenga vipaji kutoka ndani.
"Real Madrid itaendelea kuwasajili wachezaji bora'' , anasema balague.

Wanahitaji mkufunzi kama Zidane ambaye atakupatia vitu vichache lakini pia atakupatia uhuru wa kucheza."
Pengine ishara bora kuhusu mapenzi kati ya Real na Zidane ni jinsi klabu hiyo ilivyopata matokeo duni wakati ilipotengenishwa na Zidane katika nusu ya kwanza ya msimu wa 2018-19.
Chini ya Julen Lopetegui na mtagulizi wake Santiago Solari walimaliza katika nafasi ya tatu katika La Liga , pointi tisa nyuma ya washindi Barcelona na waliabishwa katika kombe la klabu bingwa na Ajax.
''Huwezi kusema Zidane ni bora zaidi kwasababu sio mzuri katika kuwaimarisha wachezaji'', anaongezea Balague.
Sio suala la kuwaimarisha wachezaji inapokuwa Zidane, na hayo ndio yaliokuwa malalamishi ya klabu hiyo - Je anaweza kuwaimarisha wachezaji wachanga?
''Anawapatia muda na motisha lakini kuwaimarisha hawezi''
'' Wakati unapotazama matokeo katika mechi kuu msimu huu, hakuna aliyefanya vyema Zaidi yake'' , anasema Laurens.
''Wanaweza kushinda La Liga na kombe la klabu bingwa kwa mara nyengine - na tayari amefanya hilo. Mpatieni heshima yake''.












