Prince Philip: Mipango ya mazishi yake ipo vipi?

Chanzo cha picha, PA MEDIA
Maandalizi ya mazishi Prince Philip, mume wa Malkia Elizabeth II, ambaye alikufa Ijumaa akiwa na umri wa miaka 99 yanaendelea .

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo yatatangazwa katika siku zijazo, lakini inatarajiwa kuwa hafla ya itakayofuata utaratibu wa kisherehe badala ya mambo makubwa ya kiserikali ambayo kawaida huhusishwa na kifo cha mtu kutoka familia ya kifalme
Ni kipi kitakachofuata?
Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa Bendera ya muungano na bendera za mataifa zitapepea nusu mlingoti kwenye majengo yote ya serikali hadi 08:00 BST siku iliyofuata mazishi. Bendera za muungano katika majengo ya kifalme, ambapo Malkia hayuko makazini, pia zitapeperushwa kwenye nusu mlingoti
Bendera ya kifalme (Standard Royal), ambayo inawakilisha enzi kuu na uendelezaji wa kifalme, haitapeperushwa nusu mlingoti na itapeperushwa kikamilifu maeneo ambako Malkia yupo
Salamu za bunduki zitafanyika saa 12:00 BST Jumamosi kwa heshima ya mtawala huyo. Bunduki katika maeneo kote Uingereza na huko Gibraltar zitafyatuliwa kwa raundi 41 kwa raundi moja kila dakika kwa dakika 40.
Meli za Royal Navy baharini, pamoja na HMS Diamond na HMS Montrose, pia itapiga saluti hiyo, kama risala kwa mtawala huyo, ambaye aliwahi kuwa afisa wa majini wakati wa Vita vya pili vya dunia na alishikilia, kati ya majina mengine, ofisi ya Lord High Admiral.
Umma unahimizwa kuzingatia saluti za bunduki kutoka nyumbani, mtandaoni au kwenye runinga.
Kwa heshima, vyama vikuu vya kisiasa nchini England, Scotland na Wales vimesimamisha kampeni za uchaguzi wa mwezi ujao.Bunge litakaa Jumatatu kwa wabunge kutoa risala zao kwa Mtawala huyo wa Edinburgh
Umma unawezaje kutoa heshima zao?
Masharti ya kuzuia usambaaji wa Coronavirus kwa kuepuka mikusanyiko ya watu inamaanisha kwamba mipango ya siku kadhaa kabla ya amzishi imebadilishwa England

Chanzo cha picha, PA
Wananchi wametakiwa kutohudhuria hafla zozote za mazishi kwa mujibu wa kanuni na ushauri wa Mamlaka ya afya ya umma
Familia ya kifalme pia imewataka watu wasiache maua na ujumbe wa rambirambi katika makao ya kifalme.
Kwenye Tovuti ya Familia ya Kifalme, wananchi wametakiwa kuzingatia kutoa mchango wa mashirika ya uhisani badala ya kuacha rambi rambi zao kupitia maua kumkumbuka Prince Philip. Kitabu cha kutoa faraja na rambi rambi cha mtandaoni pia kinapatikana kwa umma kutoa pole zao
Jalada ambalo lilioneshwa nje ya Makazi ya Buckingham, ikitangaza kifo cha Prince Philip , baadaye liliondolewa kwa sababu ya wasiwasi kwamba ingevutia umati.
Hatahivyo, watu wameanza kuacha maua, kadi na pole zao nje ya makazi ya kifalme ya Windsor, licha ya ombi la kutofanya hivyo.
Je mwili wa Prince Philip utalazwa wazi kutazamwa?
Prince Philip inaripotiwa aliomba kuwa na mazishi yasiyo na mbwembwe na alitaka hafla ndogo ambayo mwili wake usitazamwe na umma . Badala yake jeneza lake litakuwa katika Kasri la Windsor .Heshima ya mwili kulazwa wazi ili kutazamwa na umma ilipewa washiriki watatu wa kifalme wa mwisho pamoja na Mama Malkia mnamo 2002, wakati watu wanaokadiriwa kuwa 200,000 walipiga foleni kutoa heshima zao kwa zaidi ya siku tatu katika Jumba la Westminster katikati mwa London.
Diana, Malkia wa Wales pia alipewa aina ya mazishi ya kifalme ya sherehe licha ya kuwa hakuwa tena na taji la Utukufu wa Kifalme.

Lakini College of Arms, ambacho kinasaidia kuandaa hafla za serikali, kilisema mipango ya mazishi ya mtawala huyo "ilikuwa kwa mujibu wa taratibu na matakwa yake
Bendera ya kifalme ya mtawala huyo inatarajiwa kuonyeshwa katika hafla.
Bendera hiyo inawakilisha vitu vya maisha yake, kutoka urithi wake wa Uigiriki hadi vyeo vyake vya Uingereza.Wakati mtawala huyo alipochumbiana na Malkia Elizabeth wa wakati huo mnamo 1946, alikataa jina lake la Uigiriki na kuwa raia wa Uingereza , akichukua jina la mama yake, Mountbatten.
Familia ya Mountbatten kwa hivyo pia inawakilishwa katika bendera hiyo, pamoja na kasri kutoka mikono ya Jiji la Edinburgh - alikua Duke wa Edinburgh alipooa.
Nani atahudhuria mazishi?
Chini ya mipango ya mapema katika siku za baada ya kifo cha mtawala huyo , iliyoitwa jina la Forth Bridge, maelfu ya watu wangetarajiwa kukusanyika London na Windsor, na wengine hata wangepiga kambi kupata mahali pa kutazama gwaride la jeshi.
Mamia ya wanajeshi wangekuwa wamejipanga barabarani kwa heshima ya kiongozi huyo, pamoja na maelfu ya maafisa wa polisi kudhibiti umati.
Lakini tangu janga lilipoanza, waandaaji wamekuwa wakifanya kazi juu ya mipango ya dharura ambayo ingeepuka kuvutia mikusanyiko ya watu katika tukio ambalo mkuu huyo angefariki.
Malkia sasa anazingatia mabadiliko ya mipango ya mazishi na sherehe, kwa kuzingatia ushauri wa sasa wa serikali na miongozo ya watu kujitenga Siku ya mazishi, inaaminika jeneza lake litapelekwa umbali mfupi kwenda St George's Chapel kwa huduma ya misa
Masharti ya kuzuia virusi vya corona huko England yanamaanisha kuwa ni watu 30 tu, waliojitenga isipokuwa iwapo wanaishi pamoja ndio wataruhusiwa kuhudhuria.Maelezo ya wageni waalikwa au wanafamilia bado hayajatangazwa.
Hatahivyo, Prince Harry anaweza kuhudhuria kulingana na Press Association. Mtawala huyo wa Sussex anaishi Marekani na duchess wa Sussex na hajarudi Uingereza tangu ajiuzulu kutoka majukumu ya kifalme mwaka jana.
Wafalme, malkia na wakuu kifalme huzikwa katika Royal Vault ya kanisa hilo.
Hivi majuzi, St George's Chapel ilikuwa eneo la sherehe za familia, kwa harusi ya Prince Harry na Meghan Markle na Princess Eugenie na Jack Brooksbank mnamo 2018.












