Mapinduzi ya Myanmar: Simulizi nyuma ya picha ya kushangaza ya mtawa aliyepiga magoti mbele ya polisi

sista

Chanzo cha picha, Reuters

Iliyochapishwa

Picha ya iliyojitokeza kwenye televisheni na kuishangaza dunia: Mtawa Ann Rose Nu Tawng aliyekuwa amepiga magoti mbele ya maafisa kadhaa wa polisi kuwalinda baadhi ya watoto na wakazi.

Sista Ann Rose Nu Tawng amekuwa ishara ya umoja katika nchi ambayo imekumbwa na mshituko kutokana na mapinduzi ya kijeshi.

Kipindi mtawa huyo wa Kikatoliki alipolikaribia kundi la polisi kuliomba kunusuru maisha ya waandamanaji kaskazini mwa mji wa Myanmar wa Myitkyina kimesifiwa kote miongoni mwa waumini wa Kibudha walio wengi nchini humo.

Na picha za ukaidi wake wa kutoogopa amri ya maafisa wa usalama cha kutoshiriki maandamano zilisambaa sana kwenye mitando ya kijamii na kugonga vikwa vya habari kote duniani.

Sista aliyekuwa amepiga magoti na kunyanyua mikono yake juu aliwaomba poliosi hao kuondoka eneo la iglesia.

"Sitakata tamaa hadi mtakapoondoka," aliwaambia.

Polisi wawili miongoni mwao walijiunga naye ardhini, wakapiga magoti naye na kuonekana wakiweka mikono yao juu kana kwamba walikuwa wanaomba, lakini walimwambia kuwa wao pia walikuwa na kazi ya kutekeleza.

sista

Chanzo cha picha, EPA

"Kama mnahitaji kuua, ni vyema zaidi mkanipiga risasi mimi, tafadhali, Nitatoa maisha yangu ," Mtawa huyo aalikiambia kikosi cha usalama .

"Niliwaambia 'kama kweli mnahitaji kuua, Ninaweza kutoa maisha yangu ' halafu wakaondoka," alisema mtawa huyo.

Maandamano makubwa yaliibuka kote nchini Myanmar tangu jeshi liliponyakua mamlaka kwa mapinduzi mwezi Februari.

Takriban watu 54 wamekufa katika maandamano, ambapo waandamanaji walitoa wito wa kumalizika kwa utawala wa kijesho na kufunguliwa kwa viongozi wa serikali iliyochaguliwa, akiwemo Aung San Suu Kyi, ambao walipinduliwa na kufungwa.

Kuwalinda watoto

sista

Akizungumza na BBC Burma baada ya tukio lililotokea katika mji wa Myitkyina, Sista Ann Rose alielezea kile kilichokuwa kikiendelea wakati ule alipokuwa na maafisa wa polisi.

"Kulikuwa na watoto waliokuwa wamekwama na walikuwa hawajui wakimbilie wapi, walikuwa na uoga mwingi ," alisema.

"Halafu watoto wakakusanyika karibu name, walikuwa wenye njaa, kiu na uoga mwingi, na hawakudiriki kwenda nyumbani ," mtawa huyo alisema.

Lakini polisi waliendelea kufyatua risasi kwenye umati wa waandamanaji waliokua wakipinga mapinduzi katika eneo hilo.

"Ilikuwa ni kama dunia imepasuka, kulikuwa na milio ya risasi iliyosikika kila upande kiasi kwamba ilibidi nikimbilie kanisani" aliiambia BBC.

"Nilikua napiga kelele nikiwaambia watu walale chini, lakini hakuna mtu aliyenisikilizawakati ule ."

waandamanaji

Chanzo cha picha, EPA

Maelfu ya waandamanaji wamekuwa wakifanya maandamano katika mitaa ya Mynmar tangu mapinduzi yalipofanyika.

Licha ya juhudi zake kubwa, hofu kuu ya mtawa Ann Rose Nu Tawng ilikuwa halisi.

Kifo cha takriban mtu mmoja kilitokea sio mbali na pale alipokuwa.

Alikuwa ni mvulana mdojgo ambaye alikuwa amepigwa risasi kwenye fuvu lake Alikuwa na jeraha kubwa huku aliwa amelala kwenye dimbwi la damu.

"Nilitaka kumbeba mtu aliyeumia," alisema Sista Ann Rose, aliyemkimbilia mvulana huyo amchukue.

"Lakini nisingeweza kumnyenya peke yangu, kwahiyo nilipaza sauti kuwaomba watu wengine, tafadhali njooni mnisaidie ."

Lakini wakati ule, sista na wasaidizi wake walipigwa gesi za kutoa machozi.

"Macho yangu yalikuwa yanaungua, sote tulisikia joto na kizunguzungu. Tuliweza kuubeba mwili, lakini watoto wote waliokuwa wametuzingira walikuwa wanalia ," alikumbuka .

Umoja wa Mataifa umeelezea kuhofia kuongezeka kwa ghasia baina ya polsi na raia kote nchini Myanmar katika miaka ya hivi karibuni.