Bilionea wa Kijapan anawatafuta watu wanane wa kupaa nao hadi mwezini

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

JBilionea wa Japan Yusaku Maezawa amewakaribisha watu wanane kutoka kwa umma kujiunga nae kwa ajili ya safari ya kuutembelea mwezi katika chombo cha anga za mbali cha Elon Musk SpaceX .

"Ninawataka watu wa matabaka mbali mbali kujiunga nami ,"aisema kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, ambako pia alitoa maelezo ya maelezo ya maombi kwa wale wanaotaka kwenda kupitia kiunganishi hiki shared a link to application details.

Amesema atalipia ghara zote za safari hiyo, kwahiyo wale watakaosafiri nae katika chombo hicho watasafiri bure.

Unaweza pia kusoma:

Chombo hicho kinachoitwa dearMoon, kimepangiwa kusafiri mwaka 2023.

Maombo yanahitaji waombaji wawe wametimiza vigezo viwili: wawe na malengo ya "shughuli yoyote" ambayo wanaifanya "kuwasaidia watu wengine na jamii bora kwa njia fulani ", na wawe tayari "kujitolea kusaidia wasafiri wengine ambao wana maono yanayofanana na yao ",alisema:

"Nimenunua viti vyote, kwahiyo itakuwa ni safari ya kibinafsi ," aliongeza.

Bw Maezawa, ambaye ni mwanamitindo maarufu na mkusanyaji wa sanaa, awali alisema anapanga kuwaalika "wasanii" kwa ajili ya safari katika roketi ya Starship, lakini mradi wake uliofanyiwa marekebisho "utawapatia watu kutoka maeneo mbali mbali ya dunia fursa ya kujiunga na safari yake ".

"Kama unajiona kama msanii, basi wewe ni msanii ," alisema.

Mwaka jana, pia alizindua kipindi cha kuwasaka marafiki wa kike kujiunga nae katika safari, kabla ya kuifuta kutokana na ''hisia mchanganyiko''

Mnamo mwaka 2018, Bw Maezawa alitajwa kama msafiri wa kibinafsi ambaye alitarajiwa kusafiri katika maeneo mbali mbali ya mwezi na kampuni ya SpaceX, inayomilikiwa na Elon Musk.

Zawadi ambayo Bw Maezawa alikubali kulipa kwa ajili ya tiketi yake bado haijatangazwa, lakini kulingana na Bw Tusk ilikuwa ni ''pesa nyingi''.

Safari hiyo iliyopangwa mwaka 2023, itakuwa ni ya kwanza ya kwenda mwezini kufanywa na binadamu tangu mwaka 1972.