Jinsi hisabati zilivyogundulika kutoka maktaba ya Kiislamu iliotoweka Baghdad

Mwanahesabati wa Persia Muhammad Ibn Musa al- khwarizmi nchini Uzbekistan

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanahisabati wa Persia Muhammad Ibn Musa al- khwarizmi nchini Uzbekistan
Iliyochapishwa

Karne kadhaa zilizopita , maktaba moja ya Kiislamu ilizindua nambari za kiarabu duniani. Licha ya kwamba maktaba hiyo ilitoweka baadaye, hatua yake ya kuzindua nambari hizo ilibadilisha dunia.

Hakuna hata kifusi kimoja cha maktaba hiyo ilioharibiwa katika karne ya 13 kilibakia hivyobasi hatuwezi kubaini moja kwa moja ilikuwa wapi ama ilikuwa na umbo gani.

Lakini kituo hiki kinachoenziwa na wengi kilitoa mwamko mpya mjini Baghdad wakati wa mwaka wa Kiislamu wa dhahabu, na chanzo cha hisabu kote duniani.

Kilianzishwa kama makao ya kibinafsi ya kiongozi mmoja wa dini ya Kiislamu kwa jina kalifa Harun al Rashid katika karne ya 18 kabla ya kubadilishwa na kuwa shule ya umma. Miaka 30 baadaye kituo hicho kilivutia wanasayansi kutoka kote duniani .

Jumba hilo la hekima baadaye lilivunjwa wakati Wamongoli walipovamia Baghdad 1258 kulingana na maandishi yaliotupwa katika mto Tigris na kufanya maji yake kuwa meusi kutokana na wino.

Jumba la hekima lilivunjwa na Wamongoli walipovamia Baghdad

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini ugunduzi huo unawakilisha maarifa ya hisabati kwamba ufalme wa Kiislamu barani Ulaya na dunia kwa jumla utakumbatia.

Cha muhimu lakini sio maelezo ya kina yaliomo ama wapi au lini jumba hilo la hekima lilijengwa, anasema Jim Al Khalili, profesa wa fizikia katika chuo kikuu cha Surrey.

Cha muhimu zaidi ni historia ya mawazo ya kisayansi yenyewe na jinsi masomo ya kisayansi yalivyojitokeza kutokana na hilo.

Ugunduzi wa mambo ya kale kuhusu hisabati unahitaji kuangalia karne za nyuma hadi ile ya 15 na 16 , jina hilo hilo la Fibonacci linadaiwa kuangazia masomo ya hesabu barani Ulaya.

Akiwa mzaliwa wa Pisa mwaka 1170. Mwanahisabati huyo alisomea katika shule ya msingi katika eneo la Bugia, eneo la kibiashara ambalo lipo katika pwani ya Afrika kaskazini.

Wakati alipokuwa na umri wa miaka 20 ,Fibonacci alisafiri hadi katika eneo la mashariki ya kati . Wakati aliporudi kutoka Itali , alichapisha kazi yake ya kwanza kwa jina Liber Abbachi ambayo inaelezea nambari hizo za Kihindi na Kiarabu.

Tukitazama nyuma

Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati kitabu hicho cha Liber Abbaci kilipoonekana kwa mara ya kwanza 1202 , ni watu wachache walijua kuhusu mfumo wa nambari hizo za kiarabu na Kihindi ambao ulifanya kuongeza na kugawanya kuwa vigumu.

Kitabu hicho cha Fibonacci kinaelezea jinsi ya kufanya hesabu - mbinu zitakazotumiwa kutatua hesabu za kiwango cha ubadilishanaji wa sarafu za fedha na kuondoa faida.

Wale wanaotaka kujua kupiga hesabu , ni sharti wajue jinsi ya kutumia mikono yao, Fibonacci aliandika katika sura ya kwanza ya kitabu chake , ambacho kinaonesha nambari ambazo watoto wanajifunza shule.

Maktaba hiyo ilikuwa chanzo kikuu cha vitabu vingi vya sayansi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maktaba hiyo ilikuwa chanzo kikuu cha vitabu vingi vya sayansi

Werevu wa Fibonacci sio tu ujuzi wake kama mwanahisabati , lakini pia anaelewa faida ambazo amezipata kutoka kwa wanasayansi Waislamu katika karne zilizopoita na mbinu za kutatua hesabu hizo.

Fibonacci anatokana na mfumo wa algorithm wa karne ya 9 kutoka kwa mwanafizikia Al-Khwarizmi.

Kutokana na ugunduzi wake katika sekta hiyo, Al- Khwarizmi anaelezwa kuwa baba wa algebra - neno la Kiarabu la al-jabr, kurudisha vitu vilivyopotea na mwaka 821 aliteuliwa kuwa mtaalamu wa masuala ya angani na mkuu wa maktaba hiyo ya Baghdad.

Alipokuwa na umri wa miaka 20 Fibonacci alisafiri hadi mashariki ya kati

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alipokuwa na umri wa miaka 20 Fibonacci alisafiri hadi mashariki ya kati

Ilikuwa kitabu cha Al-Khwarizmi ambacho kilizindua ulimwengu wa mfumo wa hisabati kwa Waislamu. Kama anavyoelezea . "Al-Khalili ." Wengine kama vile Leornado na Pisa, walisaidia kuisambaza hadi katika maeneo mengine ya Ulaya.

Ushawishi wa Fibonacci katika hesabu za hivi karibuni ulimpa sifa Al-Khwarizmi, hivyobasi watu hao wawili ambao walikuwa wametengenishwa kwa karibia karne nne walikutanishwa katika maktaba hiyo ya enzi zilizopita.

Pengine kwa sababu kile kinachojulikana kuhusu jumba hilo la hekima ni kidogo, wanahistoria mara nyengine hujaribu kuonesha lengo lake, jambo ambalo linalipa jumba hilo hadhi ya kihistoria.

Wengi wanasema kwamba maktaba hayo sio ilivyokuwa mbele ya wengi ,Al-Khalili alisema.

Lakini ushirikiano wake na baadhi ya watu kama vile Al-Khwarizmi na aina ya kazi aliofanya katika hesabati na sekta nyengine za hesabu nje ya ushahidi uliopo ni kwamba maktaba hiyo ipo karibu na shule zaidi ya tafsiri ya vitabu .

Wataalam na wanaotafsiri katika maktaba hiyo walichukua kila hatua kuhakikisha kwamba umma unapata vitabu vyao.

Al Khwarizmi anajulikana kuwa baba wa algebra

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Al Khwarizmi anajulikana kuwa baba wa algebra

Jumba hilo la hekima lilikuwa muhimu sana - wasomi wa Kiarabu ambao walitafsiri maoni ya Uigiriki katika lugha yao - waliweka misingi ya kuelewa hisabati," alisema Juni Barrow Green, profesa wa hisabati katika chuo kikuu cha huko Uingereza.

Hata kabla ya mfumo wa kisasa wa hesabu, mfumo wa nambari kwenye kompyuta kabla ya mfumo wa hesabu wa Kirumi, watu walitumia mfumo wa nyongeza wa kuhesabu.

Ingawa sasa tunaweza kuziangalia hizi kama za zamani, nambari tofauti zinaweza kutufundisha mambo mengi na historia na utamaduni uliozipata.