Mapinduzi ya karne ya 18 ndio chanzo cha mtindo wa kuoana kwasababu ya mapenzi

Iliyochapishwa

"Ndoa" ndio jina la kazi iliyofanywa na Frederic Leighton kuanzia mwaka 1882, na - bila shaka - inaweza kuongezwa kwenye mapenzi, jambo ambalo limekuwa kama fasheni kwenye ndoa.

Tuweke wazi kuanzia mwanzo: tunachokijua kufikia sasa, mapenzi kwa waliooana ni kwamba yamekuwepo. Hata hivyo, lile la kuoana kwasababu ya mapenzi, nalo ni utamaduni wa hivi karibuni.

Katika historia ambayo imerekodiwa, mapenzi hayakuwa moja ya kigezo wakati wa kumchangua mwenza wako ili kuanza maisha ya familia.

Na, katika matukio mengi, bado hilo lipo hadi kesho.

Utafiti uliofanywa kwenye intaneti, kwa mfano, umeangazia makala moja katika gazeti la Times India - gazeti la tatu ambalo linasomwa sana Asia - kuanzia Oktoba 2020, ambapo inasemekana kuwa, licha ya "jamii kuendelea, pia imeanza kushuhudia ndoa zinazofungwa kwasababu ya mapenzi. Sio tena tamanio baya au kinyume na jamii", wanawake nchini India bado wanapendelea ndoa iliyotokana na mpenzi aliyependekezwa na wazazi kwasababu "utafiti umeonesha kuwa njia hiyo inafanya wanawake wanahisi kuwa salama zaidi."

Nchini china kuna mtazamo gani kuhusiana na suala hili? Katika tovuti makhususi kwa raia wanaotembelea China

"Ni sawa vijana kuwa na hisia ya mapenzi, lakini wanapofika umri wa kuoana, mapenzi yanachukuliwa kwamba sio muhimu lakini pia kitu hatari. Kinachozingatiwa zaidi wakati wa kumtafuta mwenza wako ni elimu bora, kazi nzuri na pengine nyumba nzuri ya kuishi."

Hadi pengine zaidi ya karne mbili zilizopita, maelezo hayo hayakuwa lazima kwa wageni kutoka nchi za magharibi kwasababu katika utamaduni wao mapenzi na ndoa vimekuwepo.

Ndoa imekuwa ikihusishwa karibu na uchumi zaidi kuliko mapenzi.

Ndoa nyingi ambazo sasa hivi tunasema zinaupendo na mapenzi awali zilikuwa ni kwa ajili ya pesa na kutengeneza muungano thabiti katika mabadilishano ya ardhi na mali.

Ingawa watu waliokuwa wanafanyakazi na jamii zinazokumbatia kilimo walikuwa na fursa nzuri ya kuchagua wapendwa wao - ukweli ni kwamba waliokuwa wa daraja la wastani na lile la juu kwao lilikuwa ni suala la kumuoa uliyechaguliwa na wazazi tangu utotoni na wala hukuweza kupinga lolote.

Kila wakati kulikuwa na walioasi na kukataa makubaliano ya ndoa zilizopangwa awali na simulizi zao za mapenzi zilinusurika.

Lakini hadi karne ya 18 hapo ndio kukaanza kupazwa sauti za kupinga utamaduni huo na ukawa ndio mwanzo wa mabadiliko katika mahusiano ya ndoa.

Namna mapenzi yalivyoanza kuingia kwenye ndoa

Kwanza, waliokuwa na msimamo mkali walikosoa hatua ya kuongeza matumaini kwa waliojadili suala la siri ya mafanikio ya ndoa kwa nguvu yao yote.

Wasiwasi pia ulijitokeza karne ya 13 kiasi kwamba serikali zilianza kuchukua hatua kuhusiana na suala la ndoa kama ilivyokuwa imeagizwa na kanisa.

Uingereza, kwa mfano, sheria ilianzishwa mwaka 1753 na kufuatiwa na zingine kusawazisha suala zima la ndoa na kusema kuwa idhini ya wazazi kwa wanandoa chini ya miaka 21 ni lazima.

Lakini hakuna ambacho kingeweza kudhibiti mapinduzi hayo ya mapenzi: Wakati wa kuliweka wazi suala hilo ulikuwa umewadia na kutetea haki za watu binafsi na msisitizo wake kwamba uhusiano wa watu kati ya jamii unastahili kuangaziwa kwa misingi ya haki wala sio kulazimishana.

Na moja ya kampeni zilizokuwa zinapinga utamaduni huo zilipendelea ndoa kwa misingi ya mapenzi na uhuru wa kumchagua mpenzi unayemtaka.

Utafutaji wa furaha

Mawazo hayo yalianza kusambawa na kundi la waliokuwa wanafanyakazi ambalo liliruhusu vijana kuanza kujitegemea mapema na kuoa punde tu baada ya kuanza kujikimu.

Na wazo la ndoa kwa ajili ya mapenzi likaanza kusambazwa.

Huko Urusi, Tsar Peter the Great alitangaza kwamba kuanzia mwaka 1724 ndoa za lazima ni haramu na kuagiza kuwa bibi na bwana harusi lazima watangaze kwamba wamependana kwa hiari.

Nchini Uingereza, upendo huo ulijitokeza miaka ya 1760 na miaka 1770 wakati sawa na kipindi ambacho watu wa kawaida nchini Ufaransa walianza kujadili juu ya ndoa ya aina hiyo ambayo watu wa tabaka la juu bado walikuwa wanachukuliwa kuwa utajiri ndio njia ya kuwa furaha katika ndoa.

Na hapo ndipo mawazo ya mapenzi ya hiari yakaingia eneo la Atlantiki.

July 4, 1776, mapinduzi ya Marekani yakapelekea azimio la uhuru ambalo liliendeleza haki za msingi za "kuishi, uhuru, na utafutaji wa furaha yako."

Muda mfupi baadaye, vijana wadogo wakaanza kukumbatia mawazo mapya ya "mahusiano ya ndoa" yaliyoongozwa na mapenzi.

Kulingana na wasifu wa Martha Skelton akiwa Ikulu ya Marekani, mtunzi wa nyaraka ya Thomas Jefferson, alikuwa na msemo wa kufuata unachotaka wakati unamchagua mpenzi wako.

"Bila shaka upendo ulidhihirika na kuchangia kukoleza mapenzi; Jefferson alicheza violin na moja ya samani alizoagiza nyumbani kwake ilikuwa ni kinanda kwa ajili ya mchumba wake."

Wengine walikuwa bora zaidi

"Kujitokeza kwa ndoa kwasababu ya mapenzi mwisho wa karne ya 18 kuliongeza tofauti kati ya wanaume na wake zao," amesema Cootz.

"Ndoa ilifafanuliwa kama muungano wa watu wawili ambao penzi lao ni kwa misingi ya kwamba ni watu wa jinsia tofauti. Wanaume na wanawake walielezwa kama wenye majuku mu tofauti kabisa ya kijamii, uwezo wa kimwili na hisia tofauti.

"Katika karne ya 19, wanaume walitambuliwa zaidi kama watafutaji riziki kuliko siku za nyuma, huku wanawake wakitambuliwa kama wenye kuketi nyumbani na kwa kiasi kikubwa kama wanaohusishwa na mapenzi."

Hadi wakati huo, mchango wa wanawake kiuchumi katika familia na kibiashara ulikuwa umetambulika, na makubaliano ya kijamii ambayo yalikuwa yanachukuliwa kuwa sehemu yao yalipunguzwa hadi kuwa mke wa nyumbani tu na kama mama.

Mapenzi yalikuwa yamezidi nguvu ndoa lakini bado kulikuwa na yale ambayo yako pembeni.

Kuna walioamini kwamba kupata furaha ya kudumu ni kutojumuisha mapenzi na kutouliza chochote kutoka kwa mke wako zaidi ya kumuomba akupikie chai na kuzaa watoto.

Wale waliokuwa wamepigania kufanya maamuzi ya kuamua mwenza wako wewe mwenyewe, walisahau kwamba uhuru kamili wa kweli hauwezi kufikiwa kwa mapenzi peke yake: kungehitaji mabadiliko ya msingi katika tabia kunakoungwa mkono kisheria katika masuala ya mali na kazi.

Wakati huo huo, wakati pekee wanawake walikuwa wanaonesha udhibiti ni wakati wa uchumba.

Wakati huo wanaume waliokuwa wanaoa waliendelea kutambulika kama kichwa cha nyumba na wake zao walikuwa na maisha tofauti. Hivyobasi, ikawa ni lengo la wanawake kuchelewesha mchakato wa kuoana kadiri inavyowezekana ili waweze kuendelea kuwa na nguvu.

Lakini katika pande zote mbili wanawake walikuwa kama wanaomilikiwa na wazazi wao na baada ya kuolewa wanaanza kumilikiwa na waume zao.

Kuelekea mwisho wa karne ya 19, kukatokea mabadiliko mengine kimya kimya

Watoto waliopata fursa ya kuishi na familia kuongezeka, wanandoa walianza kutumia njia za mpango wa uzazi kawaida tu kuzuia mimba, hivyobasi ikawa ni kama kuondoa upatikanaji wa watoto katika ndoa.

Sasa karne mpya ikawadia na suala la kupungua kwa idadi ya watoto katika familia likaanza kupewa kipaumbele waka sio tena mapenzi.

Na mapenzi pekee hayakutosha kufanya ndoa kuwa na furaha: na ikawa lazima katika maisha ya ndoa, mapenzi yawe ni yenye kujitosheleza.