Mapinduzi ya Myanmar: Raia wa Marekani watakiwa 'kukaa mahali salama'

Chanzo cha picha, Reuters
Marekani imewataka raia wake walio nchini Myanmar 'kukaa mahali salama' baada ya ripoti za harakati za jeshi na uwezekano wa kuingiliwa kwa miundombinu ya mawasiliano ya simu.
Wiki mbili zilizopita, jeshi lilifanya mapinduzi huko Myanmar (pia inajulikana kama Burma), na kuondoa serikali ya kiraia iliyoongozwa na Aung San Suu Kyi.
Siku ya Jumapili, magari ya kivita yalionekana kwenye barabara za jiji kuu, Yangon, kwa mara ya kwanza tangu wakati huo.
Mapema, waandamanaji waliingia mitaani kwa siku ya tisa ya maandamano.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa mjini Yangon imesema siku ya Ijumaa kuwa zaidi ya watu 350 walikamatwa tangu yalipofanyika mapinduzi. Bi Suu Kyi yuko kwenye kizuizi cha nyumbani.
Wafanyakazi wa kampuni za mawasiliano Myanmar zimewashauri wateja wao kuwa wameambiwa wazime mtandao wa intaneti, kuanzia Jumapili jioni mpaka jumatatu majira.
Tahadhari imetolewa kupitia ubalozi wa Marekani mjini Yangon.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kinachoendelea Myanmar
Siku ya Jumapili magari ya kivita yalionekana yakizunguka katika mitaa ya Yangon ya kati.
Magari hayo yalionekana baada ya maelfu ya watu waliojiunga na maandamano ya siku ya tisa kote nchini kupinga jeshi kushika madaraka.
Siku ya Jumamosi, jeshi lilisema hati za kukamatwa zilikuwa zimetolewa kwa ajili ya kukamatwa kwa wanaharakati saba maarufu wa upinzani na kuonya Umma kutokuwapa hifadhi wanaharakati wa upinzani wanaokimbia kukamatwa.
Picha za video kutoka Myanmar Jumamosi zilionesha watu wakijibu kwa ukaidi, wakigonga sufuria na sufuria kuwatahadharisha majirani zao kuhusu uvamizi wa vikosi vya usalama wakati wa usiku.
Wanajeshi Jumamosi pia walisitisha sheria zinazohitaji amri ya mahakama kuwazuia watu zaidi ya saa 24 na kukagua mali binafsi












