Wanademocrat wataka Trump atiwe hatiani vingenevyo ' vitendo hivyo vitatokea tena'

Wandamanaji wakivamia jengo la Capitol

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Wanademocrat wamehitimisha hoja zao kwamba Donald Trump alichochea ghasia za Capitol tarehe 6 mwezi Januari, wakionya "anaweza kufanya hivyo tena" ikiwa hatatiwa hatiani.

Waendesha mashtaka siku ya Alhamisi walitumia maneno ya waandamanaji kumunganisha Bw Trump na vurugu hizo huku wakisema kuwa vurugu hizo ilisababisha madhara ya muda mrefu pia.

Wanademocrat pia waliwasilisha ushahidi kutoka kwa polisi, wafanyakazi, maafisa wa ujasusi na vyimbo vya habari vya kigeni .

Timu ya ulinzi ya rais wa zamani itawasilisha hoja zao Ijumaa.

Baraza la Wawakilishi linaloongozwa na Democrat lilimshtaki Bw Trump mwezi uliopita, likimtuhumu kwa kuchochea ghasia. Wabunge kutoka Bunge hilo wamekuwa wakiwasilisha hoja kwa maseneta wiki hii.

Mawakili wa Bw Trump wamesema alikuwa akitumia haki yake ya uhuru wa kusema wakati wa kutangaza uchaguzi wa urais wa Novemba mwaka jana kuwa una udanganyifu.

Theluthi mbili wanahitajika kumtia hatiani Bw Trump katika baraza la Seneti lenye viti 100, lakini kuna uwezekano kusamehewa kama idadi kubwa ya maseneta wa Republican wameendelea kuwa waaminifu kwake hadi sasa.

Ikiwa Bw Trump atapatikana na hatia, hata hivyo, Baraza la Seneti pia linaweza kupiga kura kumzuia kushika wadhifa wa kuchaguliwa tena.

Ghasia kali huko Capitol nchini Marekani, ambayo ilisababisha watu watano kupoteza maisha yao, ilikuwa jaribio la wafuasi wa Trump kuzuia matokeo ya uchaguzi kuthibitishwa.

Waendesha mashtaka wa Democrat

Chanzo cha picha, Getty Images

Wanademocrat wamesema nini?

Siku ya Jumatano kesi hiyo ilioneshwa picha mpya za vurugu hizo Bw Trump anatuhumiwa kuchochea. Wanademocrat walitaka kufafanua jinsi Bwana Trump alivyosababisha shambulio la Capitol na kuwapitisha maseneta hatua katika matukio ya siku ya vurugu.

Siku ya Alhamisi, walianza hatua ya mwisho ya mashtaka yao: madhara wanayosema Bw Trump alisababisha kwenye mali, watu na demokrasia.

"Kwa sababu kushtakiwa, kuhukumiwa na kuondolewa ofisini sio tu suala la zamani zamani. Ni kuhusu siku za usoni," Mbunge Ted Lieu alieleza wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, baada ya kusema kwamba Bw Trump pia hakuonesha kujutia matendo yake.

"Inahakikisha kuwa hakuna afisa wa siku za usoni, hakuna rais wa baadaye atakayefanya vitendo kama hivyo."

Wanademokrat walionesha vipande vy video za waandamanaji wenyewe wakisema wamekuja Washington DC kwa sababu waliamini kwamba ndivyo Rais wa wakati huo Trump alitaka.

Mbunge mwenzake David Cicilline alitumia nyaraka za video na za korti kuonesha madhara yaliyofanywa kwa "Congress na mchakato wa Kidemokrasia"

Aliongeza kuwa wafanya vurugu wengine walikiri walipanga kumuua Makamu wa Rais Mike Pence na Spika wa Bunge Nancy Pelosi, wakati wengine walizungumza juu ya "kuwafungia" wabunge katika chumba cha chini ambapo walijificha na "kuwasha gesi".

"Kamwe hakuna yeyote kati yetu aliyefikiria kwamba tutakabiliwa na hatari ya mauti na umati uliolengwa na rais wa Marekani" Bwana Cicilline alisema.

Pia alitoa ushahidi kutoka kwa wafanyqkazi ambao walikuwa katika Capitol wakati wa ghasia. Mfanyakazi mmoja, anasema, aliacha kazi yake baadaye. Mfanyakazi mwingine, ambaye ni mama wa watoto watatu, alisema "uasi ulivunja hisia zangu zote za kuwa salama kazini".

2px presentational grey line

Wanademocrat pia walisema mwenendo wa Bw Trump unasababisha "madhara ya muda mrefu" kwa usalama wa ndani na msimamo wa kitaifa duniani.

Mwendesha mashtaka ya jinai Diana DeGette alisema vitisho kutoka kwa vikundi vyenye msimamo mkali wa ndani "vilikuwa na vimezidishwa zaidi na kukataa kwa Rais Trump kuwajibika na kukataa kwake kwa nguvu kukasababisha FBI yake mwenyewe iligundua kuwa ni mambo hatari zaidi kwa nchi yetu".

Mbunge Joaquin Castro alisema washirika wa Marekani walishtushwa na shambulio hilo wakati wapinzani waliikejeli Marekani.

"Ulimwengu unatazama na unashangaa ikiwa sisi ni wale ambao tunajipambanua kwayo," akasema Bw Castro.

Kiongozi wa mashtaka Jamie Raskin alihitimisha kwa kuelezea maswali kwa timu ya ulinzi ya Donald Trump, kwani Bwana Trump mwenyewe amekataa kutoa ushahidi:

-Kwa nini Rais Trump hakuwaambia wafuasi wake waache kufanya mashambulizi Capitol mara baada ya kujua hilo?

-Kwanini Rais Trump hakufanya chochote kuzuia mashambulizi kwa takriban saa mbili baada ya shambulio kuanza?

-Kwanini hakupeleka msaada kwa askari waliokuwa wamezidiwa kwa takribani saa mbili baada ya shambulio kuanza?

-Tarehe 6 mwezi Januari kwanini Rais Trump hakufanya chochote kulaani vitendo hivyo?