Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mfahamu kijana 'anayeogopa zaidi kuishi kuliko kifo'
Bila shaka lazima uwe umepitia mengi maishani kiasi kwamba, una miaka 20 tu na unachoogopa zaidi maishani mwako ni kuishi kuliko kufariki.
Hivi ndio vile Aleixo Paz anavyohisi, kijana mdogo wa Uholanzi ambaye anasema anapitia machungu yasiyokifani katika maisha yake tangu alipokuwa na umri wa miaka minane.
Akiwa na umri huo, aliungua kwa asilimia 90 katika ajali mbaya.
Alikuwa amelala fofofo katika lori la baba yake la kubeba maelfu ya lita za mafuta ya diseli.
Lori hilo lilipata ajali na mafuta yakamwagika, Mvulana huyo aliamka na kujikuta anaungua.
Ni jambo la ajabu kwa Aleixo kunusurika ajali hiyo.
Miaka mingi imepita akiwa nyumbani au hospitalini. Kijana huyo amefanyiwa makumi ya oparesheni, amepandikizwa ngozi karibu kila sehemu ya mwili wake, amepitia maumivu ya ajabu, amekuwa akiota ndoto mbaya mno na moyo wake kujawa na hasira mara kwa mara.
"Ninaamka kila siku kwasababu ya hasira niliyo nayo moyoni mwangu. Hiyo ndio sababu pekee inayonifanya niwe hai. Kile ambacho nimepitia na ninachoendelea kupitia. Na kwamba sasa hivi ninafanya muziki, ambao unanipa moyo", Aleixo amezungumza na BBC kwa njia ya simu.
Kwa sasa vyombo vya habari vinamfuatilia baada ya maisha yake kuangaziwa kwenye makala maalum iliyopewa jina la "El Niño de fuego".
Kutengeneza filamu kulimgharimu sana, amesema muongozaji wake, Ignacio Acconcia.
Aleixo hapendi kuwa maeneo ya umma au kuangaliwa. Haamini mtu na imekuwa vigumu kwake kufunguka.
Pia hakupenda wazo la kwamba anafanyiwa filamu, kwasababu kamera zimekuwa zikimuandama kwa miaka kadhaa.
Aleixo hatarajii chochote kubalika. Na pia hajasahau alichopitia tangu alipopata ajali.
Kijana huyo amekuwa akijificha kwa kipindi cha miaka kumi.
"Mjomba, amka, hili halitakubadilisha kabisa"
"Pengine nyinyi wanahabari mumenichosha na mahojiano yenu?
Hapana, msiwe na wasiwasi.
Kwanza, naendelea kuwa vizuri kila uchao lakini sijazoea sana.
Ninachofurahia ni watu kujitokeza na kusema kuwa simulizi yangu imewasaidia au wanasikiliza nyimbo zangu.
Ukweli wa kwamba makala hiyo ilipewa jina la "Mtoto aliyeungua" na baadaye hilo likawa jina langu, hilo halikunifurahisha, lakini nilizoea na pia nililipenda kwasababu ya matokeo yake.
Lakini inafika wakati kisha najimbia, 'angalia uhalisia wa hali hii, hali hii haiwezi kubadilika.'
Kile kinachonipa faraja ni kwamba watu wanahisi vizuri baada ya kukutana nami.
"Bado sijakubali hali yangu"
Wala sitaki watu wafanye makosa ya kuniona kama mtu ambaye ni mfano wa kuigwa.
Hapana, ukweli ni kwamba napitia kile ambacho ni maisha yangu ambacho kila mmoja anapitia yake.
Kwa hiyo mtu akiona pengine kuna nguvu niliyonayo ambayo ni ya ajabu ndani yangu, usianze fikiria mambo mengine, nguvu pekee nilionayo ni kuvumilia.
Na ninapoendelea na maisha yangu sio kwasababu ya kingine chochote zaidi ya hasira ndani yangu.
Hicho ndicho kinachonifanya nisonge mbele.
Nina maumivu makali sana ya tumbo na machungu ninayopitia kila siku.
Maumivu hayo huwa yananifanya mara moja nianze kunyongonyea.
Haijalishi watu wataniambia mambo yako sawa, ukweli ni kwamba kila kitu kitasilia jinsi kilivyo.
Na bila shaka, nitaendelea kupigania maisha yangu.
"Aleixo haniwakilishi mimi"
Ninapojiangalia nilipokuwa mtoto, huwa sijitambui, Yaani hakuna uhusiano wowote na muonekano wangu kimwili, kitu ambacho pengine kila mmoja huenda ndicho atakachofikiria kwanza.
Tangu niliopoungua, kuanzia wakati huo, nilijua ni kitu gani kimenitokea na kwamba sitaweza kuwa jinsi nilivyokuwa kimwili, lakini hilo kwangu halina maana tena.
Kile ambacho siwezi kukizungumzia ni kuwa na matumaini, kutaka kuwa na furaha, Siwezi tena kuwa hivyo.
Tangu ajali ilipotokea nimelazimika kujihami tena.
Jina langu ni Aleixo, lakini haliniwakilishi mimi. Aleixo, ni jina la aliyekuwa mtoto wala sio kijana niye sasa hivi.
"Naogopa zaidi kuishi kuliko kifo"
Watu wanaweza kusema kuwa mimi ni shujaa kwasababu najitahidi kusonga mbele lakini sio hivyo.
Ukweli ni kwamba tangu nilipopata ajali, naogopa zaidi kuishi kuliko kifo.
Ajali hiyo siwezi kuisahau maishani mwangu, na kila ninapoanza kufikiria najawa na fikira chungu nzima.
Wakati nilipokuwa ninaungua hakuna muda hata dakika moja nilipoteza fahamu zangu.
Ni vigumu sana kusahau kilichotokea.
'Sina haja ya kuwa sawa, Sijui namna ya kuwa sawa na sijazoea kuwa hivyo. Kwanza, huwa nahisi kuwa na nguvu zaidi, ninapoamka na kujiona siku hiyo siko sawa kwasababu wakati huo, hasira ndio inayonisukuma', amesema Aleixo.
Sina lazima ya mimi kuwa sawa mradi familia yangu iko sawa, inatosha.
'Familia yangu ikijisikia vibaya, mimi sitakuwa sawa. Hili ndio ninaloogopa, kwa hiyo ni kheri niharibikiwe peke yangu. Nimezoea maumivu ya tumbo, ya mwili na kihisia za machungu'.
'Kuwa na ndoto mbaya imekuwa kitu cha kawaida kwangu na hiyo ndio sababu huwa napata usingizi kwa muda kidogo sana na mara nyingi naamka ghafla huku moyo wangu ukiwa unadunda huku namwagika jasho', amesema Alexio.
"Muziki hunipa matumaini"
"Tangu nilipojitosa kwenye muziki wa rap nimepata matumaini kidogo: nimekuwa na lengo na jambo la kunifanya nisonge mbele.
"Muziki umekuwa mkombozi wangu. Sasa basi usichukulie kuwa mimi ni muimbaji, hapana, na wala sina malengo yakufika mbali sana kimuziki".
Pia huwa ninafanya muziki kwasababu ya mshauri wangu, Isaac Real "Chaca" ambaye aliniunganisha na muziki na kunipa fursa wakati ambapo sikuwa na chochote na tukarekodi muziki wetu wa kwanza lakini naweka wazi kwamba mimi sio mwanamuziki na kwamba ni vigumu sana kupata kipato kupitia njia hii.
Lakini kitu kimoja kieleweke, muziki umekuwa mkombozi wangu. Kabla, sikuwa na cha kuondoa hasira zangu, lakini siku hizi nafanya hivyo kwa kuandika muziki".