Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rais Magufuli ametahadharisha kuhusu matumizi ya dawa za kupambana na Covid-19 zinazotoka nje
- Author, Munira Hussein
- Nafasi, Reporter
- Iliyochapishwa
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewataka watanzania kutumia dawa za asili katika mapambano dhidi ya Covid-19
Akizungumza Jijini Dodoma hii leo, amesisita juu ya matumizi ya miti shamba pia kujifukiza katika mapambano dhidi ya Covid-19.
Aidha amesema kuwa si kila dawa zinazotoka nje ya nchi ni nzuri kwa watanzania.
''Kuna dawa inaitwa Covidol, Bugiji zinafanya kazi kwasababu zimekua proved na mkemia mkuu, kamwe msifikirie kila dawa inayotoka nje ni kwa ajili yenu, ingekua hivyo Malaria ingeisha. Tujitaambue tusitumike. Madawa haya yalipigwa vita na wakoloni kwasasab ya uchumu, ukiw ana mti wako hata kama unaponesha malaria utaambiwa ni wa kishamba''. Alisema Magufuli
Ameitaka pia Wizara ya Afya kutoa ushirikiano kwa wagunduzi wa dawa za asili.
''Mungu ametuma hii mimea na ikabarikiwa, tuitumie, lakini tuitumie kwa kufuata masharti na utaalamu mzuri, kwa hiyo Taasisi yetu ya Wizara ya Afya inayosimamia dawa za asili, huu ni wakati wa kuyatumia kikamilifu. Na Wizara ya Afya isiwakatishe tamaa watu hawa, na madaktari wanatumia hizo hizo dawa, wao wanaenda wanakunywa, wanajifukiza wakija huku wanawatwanga masindano'' Alisema.
Ameongeza pia kuwa Watanzania kwa wakati wote wamemtanguliza Mungu na kuendelea kujilinda hivyo wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari.
Viongozi wa ngazi mbalimbali pia wameendelea kuhamasisha matumizi ya dawa asili katika mapambano ya Covid-19.
Hata hivyo Shirika la Afya duniani (WHO) limetahadharisha kuhusu matumizi ya dawa za asili ambazo huenda zikaleta madhara kwa binadamu.
Kauli hii ya Magufuli inakuja muda mchache baada ya WHO kutangaza mpango wa muda kuhusu jinsi nchi zitakavyopewa chanjo za corona mwaka huu, huku Tanzania na Burundi zikiwa hazimo katika orodha yake.
Shirika hilo la afya duniani linasema kuwa nchi ambazo hazimo katika orodha yake ya kupewa chanjo ya corona ni kwasababu "zilijinunulia chanjo zake zenyewe, hazikuomba chanjo, au hazijawekwa bado katika orodha ya nchi zitakazopewa chanjo
Tanzania imeendelea kukunusha taarifa za uwepo maambukizi ya Covid-19 nchini humo.
Mara ya mwisho Tanzania ilitoa taarifa rasmi juu ya maambukizi na vifo vilivyosababishwa na Covid-19 mwezi Aprili, mwaka 2020 ambapo wakati huo wagonjwa walikuwa ni 506 na vifo 21.