Virusi vya corona: 'Kuna Watanzania walienda nje kupata chanjo badala yake wakatuletea corona ya ajabu ajabu'

Iliyochapishwa

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametahadharisha kuhusu chanjo ya Covid 19 ambayo imeanza kutolewa katika mataifa mbalimbali duniani.

Akizungumza katika uzinduzi wa shamba la miti huko wilayani Chato mkoani Geita, amezungumzia pia kuhusu hali ya corona nchini na kuwasihi wananchi kuendela kuomba pamoja na kujifukiza.