Je ni nini kilichowafanya wasanii Davido na Burnaboy 'kukunjiana ngumi' katika kilabu ya burudani Ghana

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Wasanii wawili wakubwa wa Nigeria Davido na Burna Boy wamedaiwa kupigana katika klabu moja ya burudani nchini Ghana.

Kulingana na BBCPidgin, zogo lilizuka baada ya Burna Boy kuingia katika klabu ambayo Davido alikuwa anawatumbuiza mashabiki wake.

Video iliyovuma mitandaoni inamuonesha Davido aliyekuwa na hasira akizuiliwa na walinzi asipigane.

Hijabainika ni nini hasa kilichosababisha vurugu hizo lakini walioshuhudia wanasema Davido tayari alikuwa katika klabu ya burudan akiendelea na onesho lake.

Lakini baada ya Burna Boy kufika hapo, hali ya taharuki ikatanda. Inadaiwa wasani hao hawapatani.

Licha ya Davido na Burna Boy kulumbana, kuna video nyingine iliyosambazwa mitandaoni inayomuonesha msanii Wizkid akiwa katika eneo la tukio.

Lakini Wizkid hakujihusisha na ugomvi huo badala yake aliendelea na shughuli zake.

Ujumbe wa Davido kwenye Twitter wazua gumzo

Aliingia katika mtandao wa twitter baada ya majibizano yote hayo na kuandika nitamwachi huu muziki

Hivi ndivyo mashabiki wao walivyopokea madai ya zogo hilo

Mashabiki wao walitumia mtandao wa Twitter kubishana juu ya ni nani mkali kati Davido na Burna Boy.

@julimilliboy aliandika '' Ukweli kwamba Wizkid na Burnaboy wote wamekaa Ghana kwa siku kama 2 na vyombo vya habari haivkujua uwepo wao hadi Davido alipofika Ghana jana ni isha wazi kwa ni kwanini Davido alisema....Ni mimi nawapatia umaarufu''