Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi wa Marekani 2020: FBI yahusisha Iran na tovuti zinazolenga maafisa wa uchaguzi
Wadukuzi wa Iran "huenda walihusika" katika uendeshaji wa tovuti kadhaa na akaunti za mitandao ya kijamii ambazo zilikuwa zikiwatumia ujumbe wa vitisho maafisa wa ngazi ya juu waliyopewa dhamana ya kusimamia uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, mashirika mawili ya usalama nchi Marekani yametangaza.
Katika taarifa ya pamoja iliyochapishwa Disemba 23, Shirika la upelelezi la Marekani FBI na Shirika la usalama wa mtandao na na miundo mbinu ya usalama (Cisa) zilisema zina taarifa ''za kuaminika'' zinazoashiria kwamba Iran ilikuwa ikiendesha mpango huo.
Oparesheni hiyo "inaashiria nia ya Iran ya kusababisha mgawanyiko na kutokuaminiana nchini Marekani na kudhoofisha imani ya umma katika mchakato wa uchaguzi wa Marekani ", iliongeza.
Tovuti na akaunti ya mitandao ya kijamii zilizo na majina,"Maadui wa Watu" na "Maadui wa Nchi", zilibuniwa mapema mwezi Desemba na kujumuisha majina, picha na maelezo kuhusu mahali wanakoishi maafisa 38 wa serikali kuu na majimbo ya Marekani, pamoja na watu binafsi - ambayo huuza programu ya elektroniki ya kupiga kura na vifaa.
Rais Trump, wanasheria wake ana washirika wake kadhaa hivi karibuni wametoa madai juu ya udanganyifu mkubwa wa upigaji kura wa elektroniki katika majimbo kadhaa ya yaliyo na ushindani mkali.
Lakini mahakama zimetupilia mbali kesi ambazo ziliashiria madai hayo.
"Watu wafuatao wamesaidia na kupitisha uchaguzi wa ulaghai dhidi ya Trump," ilisomeka barua kwenye vikoa hivyo.
"Kubadilisha kura na kufanya kazi dhidi ya rais ni uhaini na Wamarekani wazalendo hawapaswi kusahau wale waliosaidia kupindua demokrasia yetu, " iliongeza.
Shirika hilo pia liligundua anauani nne ya barua pepe zinazohusishwa na tovuti ambazo zilituma "barua pepe za kuwatishia" maafisa.
Oparesheni katika akauti za mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter, Parler, V-Kontakte, Pinterest na Gab ilisambaza vikoa hivyo na utoa wito kwa wafuasi wa Trump kuongeza maelezo ya watu zaidi ambao "walisaliti nchi yetu na maadili ya kidemokrasia".
Mkuu wa Shirika la upelelezi la Marekani FBI Christopher Wray, Mkuu wa zamani wa Cisa Chris Krebs - ambaye alifutwa kazi mwezi uliyopita ba Bw. Trump kwa kujichanganya katika madai yake ya udanganyifu wa kura- Gavana wa Michigan Gretchen Whitmer, Waziri wa mambo ya nje katika jimbo la Georgia Brad Raffensperger na meneja wa utekelezaji wa mifumo ya kupiga kura Gabriel Sterling walikuwa kati ya maafisa ambao maelezo yao yalionekana kwenye tovuti hiyo.
Mapema mwezi huu, Bw. Sterling aliwakemea Warepublican, akiwemo rais, kwa madai ya udanganyifu katika jimbo baada ya wafanyikazi kadhaa wa uchaguzi kutishwa na wengine kutishiwa kuuawa.
Tovuti zote zilizohusishwa na oparesheni hiyo pamoja na maelezo yaliyohifadhiwa pembeni zimefutwa.
Akaunti nyingi za mitandao ya kijamii pia zimefutiliwa mbali. Lakini akaunti zilizo kwenye VK na Parler bado zipo, japo akaunti ya Parler zimewekwa kuwa za kibinafsi.
Joe Slowik, mtafiti wa ngazi ya juu wa masuala ya usalama washirika la DomainTools,alisema katika chapisho la blogi kwamba maelezo ya usajili wa kikoa yaliyopatikana hadharani yaliwekwa ili kuonyesha kana kwamba operesheni hiyo ilitokea Urusi
Hata hivyo barua pepe zinazohusiana na wasajili wa kikoa zilitumia "yandex.com" inayolenga ulimwengu badala ya lugha ya Kirusi "yandex.ru".
"Hii inaweza kuwa ya mazingira, au inaweza kuunga mkono nadharia kwamba shughuli inayohusika inajaribu kuonekana kama vitendo vya Urusi lakini ukosefu wa ujuzi wa lugha ulisababisha utumiaji wa tovuti ya com badala ya ru ya lugha ya Kirusi," Bw Slowik aliongeza katika sahihisho la baadaye.
Hii ni mara ya pili maafisa wa Marekani wamehusisha Iran na jaribio la kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mwezi Oktoba, maafisa wa usalama wa kitaifa walisema Iran ilihusika katika visa vya kutuma ujumbe wa barua pepe wa kutishia wapigakura wa Democratic.
Barua pepe hizo zilionekana kutoka kundi la mrengo wa kulia linaojiita Proud Boys, linalounga mkono- kundi la Trump lililopangwa "kuchochea ghasia", Mkurugenzi wa Upelelezi wa Kitaifa John Ratcliffe alisema.
Iran imekana kuhusika na barua pepe hizo, na haijatoa tamko lolote kuhusu taarifa ya FBI.
Twitter ilifuta karibu akaunti 130 zinazohusishwa na Iran ambazo zilijaribu ''kuvuruga mazungumzo ya umma'' wakati wa mdahalo wa kwanza wa urais.
Baadhi ya akaunti ziliweka ujumbe wa Twitter unaomuunga mkono Bw. Trump huku zingine zikimuunga mkono Joe Biden.