Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Binti yangu ni wa kwanza katika kizazi cha makahaba kwenda chuo na sina majivuno'
"Alipokua mtoto alikuwa na ndoto ya kuwa mwalimu, lakini aliishia kuwa kahaba kama mama yake, bibi yake na bibi mzaa bibi ."
Karina Núñez ni kizazi cha nne cha familia ya Uruguway ya wafanyabiashara wa ngono na anakumbuka maisha yake ya utotoni yakiwa magumu wakati wote.
" Ilitokea wakati wakati wa utawala wa kidikteta nchini Uruguay na mwanaume aliyemchukua mama yangu kama kahaba aliamua kunilea na kunikuza kama binti yake binafsi ," alisema katika mahojiano na BBC .
"Halafu mwanaume huyo alikuwa mfungwa wa kisiasa na hapo ndipo maisha yetu yalipobadilika kabisa: mama yangu alilazimika kurejea tena mitaani kuendelea na biashara ya ngono ."
Hatahivyo maisha yake ya utotoni hayakuwa rahisi na kwa ujumla anasema yalikuwa yamegubikwa na umasikini, shida na ukahaba mwingi, leo anasema kwamba ameamua ''kuvunja minyororo''
Na kweli ameweza. Sasa amekuwa mmoja wa viongozi maarufu wa muungano katika nchi ya Uruguay.
Pamoja na kutetea haki za wanawake na wafanyabiashara wa ngono, Karina anaendesha mapa,mbano dhidi ya unyanyasaji wa kingono wa watoto na vijana wadogo.
Sambamba na hilo, "kwa usaidizi wa wanawake wengine," aliweza kumfanya binti yake Valeska, kuwa mtu wa kwanza katika familia yake kusoma Chuo Kikuu na hilo anajivunia. Lakini safari haikuwa rahisi.
"Unapozaliwa katika mazingira ya ukahaba, kujinasua sio rahisi ni vigumu sana ."anasema.
Kiwango cha juu cha unyanyapaa kilichokikumba kizazi changu hakikuwa mazingira mazuri kwangu ya kukulia. Na pia ilinifanya niichukie jamii ili kuyajenga maisha yangu ya sasa.
Maishani mwangu nimekua kila mara nikifikiria kuwa mtu anapaswa kujisimamia mwenyewe , na kama kitu kibaya kikikutokea basi ni kwasababu umefanya kosa fulani na ni lazima uvumilie
Umefanya uamuzi mbaya basi vumilia.
Sikuwahi kufikiria kuwa mambo yaliyonitokea yalisababishwa na hali ya hatari niliyokuwemo ambayo nimekuwa nimeibeba kwamba nilikuwa ni kizazi cha nne cha familia ya wafanyabiashara ya ngono.
Mchakato wa kunyanyaswa kingono niliishi nao kwa muda mrefu kama kitu cha ushujaa.
Baada ya miaka mingi ya uchungu , ninaweza kuelewa kuwa hakuna ushujaa wowote kuhusu kunyanyaswa kingono.
Sasa ninayaona maisha yale kama tukio la maafa katika maisha yangu na hilo limechochea nguvu nilizonazo sasa.
Uelewa huu umenisaidia kubaki katika nafasi ya muathiriwa na kujiimarisha mwenyewe ili baadae niweze kuwasaidia makahaba wengine kuondokana na ukimya, na matatizo mabli mbali wanayoyapitia.
Kila mtu ana jinsi anavyoona ni wapi yuko salama zaidi na palipo na hatari zaidi kwake kwa njia tofauti.
Kwa wengine wetu ambao walikulia katika utoaji wa huduma za ngono na ambako kuzungumziwa kwa huduma ya ngono kilikuwa ni kitu cha kawaida, ni dhahiri kwamba hatutataka kutafuta mahala pengine.
"Nilitaka tu kuwa Karina aliye bora zaidi"
Wakati Karina Nuñez alipotambua kuwa hataki binti yake afuate mkondo wake, wala njia ya bibi zake, baada ya kuwa mwenye kupata uzoefu wa ukahaba , hatari ya mfanyabiashara wa ngono na maisha yote waliyopitia mchana na usiku , alitaka kupambana na hali hiyo.
Nilipobisha hodi na kuomba haki za makahaba wenzangu, walinitambua kuwa sauti ya kuaminika, kwani nilikuwa kahaba halisi.
Ni wao ndio walionipatia cheo cha mwanaharakati wa muungano na sijui kingine,lakini kusema kweli nilitaka kuwa Karina aliye bora zaidi.
Mwaka 1999, nilipinga mtandao wa ulanguzi wa makahaba ambao uliwachukua wasichana wawili Italia na kutokana na hilo makahaba wawili walinipiga hadi nikalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa siku 11 na ilinichukua miezi mitatu kuweza kutembea tena .
Baadaye nilipoweza kufanya hivyo tena, kwa msaada wa magongo, nilirejea tena katika chumba cha malalamiko. Ilinibidi nisubiri miaka saba kwa wao kunisikia na kumshitaki mlinzi ambaye alikuwa ameniuza kwenye mtandao wa makahaba.
''Lakini kile ninachoweza kusema nilichokifanya kilikuwa cha maana'', anasema Karina
Nchini Uruguay, shughuli za ukahaba zilikatazwa tangu mwaka 2002 na kwa sasa ni moja yanchi za Amerika Kusini zenye sheria huru kuhusiana na ukahaba.
Katika nchi nyingi za kanda hiyo bado kuna biashara ya ukahaba inafanyika huku nyingine zikiichukulia biashara hiyo kama haramu.