Uchaguzi wa Uganda: Madai yasiyo sahihi kumuhusu Joe Biden na wengine

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Peter Mwai
- Nafasi, BBC Reality Check
- Iliyochapishwa
Huku uchaguzi wa uganda ukitarahiwa kufanyika mwezi Januari, kuna taarifa nyingi za upotoshaji ambazo zinasambazwa katika kameni za uchaguzi ambao umekuwa na gasia kubwa.
Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa wagombea 11, miongoni mwao mwanamuziki anayefahamika kama Bobi Wine.
Baadhi ya taarifa za upotoshaji kuhusu kampeni huhusisha ubunifu wa maudhui na wakati mwingine dhana ya video hubadilishwa au kupotoshwa.
Joe Biden haungi mkono upinzani

Chanzo cha picha, Getty Images
Mfano wetu wa kwanza ni video ya sauti ambayo ilisambazwa sana , huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakidai inaonesha rais mteule wa Marekani Joe Biden katika tukio akitoa witi wa kuachiliwa huru kwa Bobi Wine (jina halisi Robert Kyagulanyi).
Badhi hata wanadai inaonesha Bw Biden akimuidhinisha katika uchaguzi wa Uganda.
Mwanaume mwenye mvi anayeonekana akizungumza katika video hiyo anasikika akisema : "Sote tunajali kuhusu uhuru wa kuabudu katika dini zetu. Sote tunasimama pamoja, tunahitaji demokrasia nchini Uganda ."
Lakini mwanaume huyo haongei na Joe Biden , na video hiyo imekuwepo kwa miaka miwili.
Tuligundua kuwa ilikuwa ni moja yavikundi vya waandamanaji wanaounga mkono upinzani nchini Uganda wakati wa maandamano yao yaliyofanyika katika miji mbalimbali kote duniani baada ya kukamatwa kwa Bobi Wine Agosti 2018.
Tukio hili lililochukuliwa kwenye video lilifanyika katika mji wa Boston, na mwanaume anayezungumza ni Nick Carter, mwanasiasa wa Democratic ambaye alikuwa akigombea uchaguzi huko.
Anasikika akisema kwa muda wa dakika tatu katika video hiyo, akiongelea uungaji mkono kutoka jamii ya eneo hilo kwa ajili ya azma yake kupata kiti katika baraza la Gavana la Massachusetts.
Pia tulizungumza na maafisa wa habari wa Bw Biden, ambao walituambia kuwa : "Rais mteule hajatweet au kutoa taarifa yoyote kuhusiana na suala la uchaguzi wa Uganda.
Walisema kuwa tweet halisi kuhusu Uganda iliyotumwa kutoka kwa Biden kuhusu Uganda ilitumwa Oktoba 2019 kuhusiana na suala la haki za wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia LGBT.
Na Barack Obama pia hajajiunga pia
Mwezi uliopita, rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alianza kuonekana katika jumbe za mitandao ya kijamii zinazounga mkono upinzani.

Bw Obama anaonekana katika jumbe zilizotumwa kupitia kampeni ya mtandaoni au hashtag #FreeBobiWine, kwa kutumia jina lake la Twitter.
Lakini hakuna rekodi inayoonesha Bw Obama alituma kauli ya aina hiyo, ingawa picha ya simu ya tweet hiyo inaonesha ujumbe huo ulishirikishwa kwa umma karibu mara milioni.
Pia inaonesha makosa madogo ya kisarufi huku neno "iPhone" likiandikwa kimakosa kwa kuanza na herufi kubwa.
Na alama ya vyema ya blu ambayo kwa kawaida huonesha mmiliki halisi wa akaunti ya twitter ni ya rangi nyeupe.
Picha za simu zilizo sawa na tweets ziliandaliwa kwa kutumia programu ya bure ya mtandao kwa ajili ya kutunga jumbe za Twitter za uzushi.
Je Bobi Wine aliepuka kuzungumzia rekodi yake ya kisiasa ?
Akaunti za twitter zinazounga mkono serikali zilituma jumbe zinazodai kuwa mgombea wa upinzani Bobi Wine alikwepa swali kuhusu rekodi yake kama mbunge wakati wa mahojiano na radio.

"Muongozaji, sinamuda wa kutosha hapa katika radio, hebu tuendelee na swali jingine ,"ndio swali analosemekana Bobi Wine kutoa.
Lakini kuna mambo kadhaa hapa.
Video ya picha ya kituo cha radio iliyotumiwa ni ya Radio Wa 89.8 FM iliyopo kaskazini mwa Uganda.
Lakini alikuwa katika kituo hicho katikati ya mwezi Novemba, na picha hizi zilizotumwa zote ni za matikati ya mwezi wa Disemba.
Pia walisema kuwa mahojiano aliyoyafanya katika wilaya ya Kabale kusini- magharibi mwa Uganda, ambako kuna radio tofauti ya eneo hilo inayoitwa 100.4 Hills FM.
Ni kweli kwamba Bobi Wine alikuwa hewani kwa mahojiano hayo hapo tarehe 16 Disemba. Lakini kituo hicho cha radio kilituambia kwamba alizungumzi rekodi yake kama mbunge , ambapo alizungumzia mambo kadhaa aliyoyafanya.
"Ndio, aliulizwa na akajibu kwa ukakamavu juu ya miradi mbali mbali aliyohusika nayo," alisema meneja wa radio Nick Kanyesigye.
Afisa kutoka chama cha Bobi Wine aliithibitishia BBC hili , akiongeza kuwa alimuomba muongozaji wa kipindi wakati huo kuendelea na swali jingine, na kwamba haya yalikuwa ndio mahojiano pekee ya radio aliyoyafanya tarehe 16 Disemba
Hii sio sampuli ya karatasi ya kupigia kura

Nakala ya kile kinachoonekana kama karatasi rasmi ya kupigia kura yenye majina ya wagombea na nembo za vyama imekua ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Lakini Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo inasema karatasi hiyo ya kura sio ile waliyoitoa wao.
"Tume ya Uchaguzi haijatoa muundo wa karatasi ya kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2021. Tafadhali ipuuze " tume inasema.
Kuna viashiria vya ukweli kwamba kuna kitu ambacho sio sahihi
Katika uchaguzi uliopita, makaratasi ya kupigia kura yalionesha majina katika safu ya kwanza , halafu picha zao na nembao za vyama, na kisanduku kitupu katika safu ya mwisho na halafu eneo ambapo mpigakura angeweka alama yake ya kuchagua.
Lakini ile inayoonekana ikisambazwa inaonesha picha kwanza
Paul Bukenya, msemaji wa tume ya uchaguzi , alituambia kuwa inata sampuli ya karatasi ya kupigia kura kwa madhumuni ya kutoa elimu ya upigaji kura tkabla ya siku ya uchaguzi.
Lakini pia alisema kuwa hawatumii majina halisi, picha wala alama za wagombea au vyama vya siasa -ni vya kubuniwa tu.














