Je, mzozo utarejea tena baada ya walinda amani kuondoka Darfur?

Walinda amani wa UNAMID mjini Nertiti
Iliyochapishwa

Wakati walinda amani wa kimataifa wanapojiandaa hatimaye kuondoka katika eneo la Darfur lililokumbwa na vita nchini Sudan wasiwasi umeongezeka kuhusu usalama wa raia ikiwa makubaliano mapya ya amani huko yatashindwa, kama vile Mike Thomson wa BBC anavyoarifu.

Abdullah mwenye umri wa miaka kumi na nne amekaa kwenye gurudumu la zamani nje ya kibanda kibovu katika kambi kubwa na masikini ya watu waliokimbia makazi yao.

Alizaliwa katika kambi ya Abu Shouk, nje kidogo ya El Fasher Kaskazini mwa Darfur, na ndio nyumba pekee ambayo amewahi kuijua.

"Nimeambiwa kwamba familia yangu na jamaa wengine walikuwa wakiishi pamoja katika kijiji kizuri sana kilichozungukwa na ardhi ya kijani.

"Wazazi wangu wameniambia kwamba ilikuwa mahali pazuri na kwamba maisha yalikuwa mazuri sana huko."

Abdullah
BBC
We have to hide, there's nothing more we can do. If you confront them you'll be attacked"
Abdullah
Fourteen-year-old camp resident
1px transparent line

Abdullah, ambaye ameona televisheni mara moja tu maishani mwake, anaishi kwa hofu ya magenge yenye silaha ambayo mara nyingi huvamia kambi nyakati za usiku.

"Lazima tujifiche, hakuna kitu kingine tunachoweza kufanya. Ukikabiliana nao utashambuliwa."

Inatarajiwa kwamba makubaliano ya amani ya hivi karibuni yatamwezesha Abdullah na familia yake kwenda nyumbani, na mwishowe kumaliza mzozo uliodumu kwa miaka 17 huko Darfur, ambao umesababisha vifo vya watu 300,000 na kulazimisha watu milioni 2.5 kukimbia makazi yao.

Ramani ya Sudan

Vurugu zilianza mnamo mwaka 2003 wakati vikundi vyenye silaha vilipinga serikali, wakidai mkoa wao ulipuuzwa.

Khartoum ilijibu kwa kuwapa silaha wafugaji wahamaji wa Kiarabu, ambao walijulikana kama Janjaweed na kuwalipa ili kudhibiti uasi huo.

Makundi mengi ya waasi sasa yamesaini makubaliano ya amani na serikali, lakini takribani watu milioni 1.5, kama Abdullah, wamebaki katika kambi karibu 60 zilizo kote mjini Darfur.

Getty Images
Sudan's Darfur conflict

  • April 2003Fighting starts in Darfur

  • July 2007UN Security Council approves Darfur peacekeeping force

  • March 2009International Criminal Court (ICC) issues arrest warrant for President Omar al-Bashir for war crimes in Darfur

  • April 2019 Sudan's army ousts Bashir

  • February 2020 Government agrees Bashir can stand trial at the ICC

  • August 2020Sudan's government agrees peace deal with five rebel groups

Source: BBC
1px transparent line

Wengi, kama Zara, ambaye amekuwa katika kambi ya Abu Shouk kwa miaka 17, anatamani kwenda nyumbani, lakini bado hawezi.

"Hatuwezi kwenda kulima ardhi yetu kwa sababu tu inamilikiwa na wengine. Hao ndio waliotuua, wao ndio waliotukimbiza, na bado tuko hapa."

"Kila siku ni mauaji"

Safari ya kwenda jittery mjini Nertiti, karibu saa sita kwa gari kutoka kambi ya Abu Shouk, inaonesha sababu nyingine kwanini watu wengi waliokimbia makazi yao bado wanakataa kwenda nyumbani.

Wakulima wengi huko wanaogopa sana kwenda kwenye mashamba yao kufuatia vitendo vya mauaji na ubakaji.

Wale walio katika mji wenyewe hawako salama pia.

Makundi ya watu wenye silaha, wanaojulikana kama Janjaweed, hivi karibuni yalimuua kwa risasi mume wa Khadiga Ishag na mmoja wa wanawe kabla ya kumpiga risasi pia nyumbani kwao Nertiti.

"Hatuiamini serikali yetu, wanajeshi au polisi, kwa kweli hatuwaamini kabisa. Suluhisho lisipopatikana kutakuwa na mauaji ya kimbari hapa."

Khadiga Ahmede Ishag na familia Nertiti

Sababu ya Khadiga na wengine kuogopa jeshi ni kwamba safu yake kwa muda mrefu ilikuwa na wapiganaji wengi wa zamani wa Janjaweed, watu wale ambao waliwatisha kwa muda mrefu.

Sio hivyo tu lakini chini ya makubaliano mapya ya amani wanachama wa vikundi vingine vyenye silaha wanapaswa kujumuishwa katika jeshi la Sudan.

Kuna sababu nyingine pia.

Mwisho wa mwezi Desemba kikosi cha kimataifa cha kulinda amani Unamid, ambacho kilikuwa kikubwa zaidi ulimwenguni, mwishowe kinajiondoa Sudan baada ya miaka 13.

Licha ya imani iliyoshikiliwa sana kuwa kikosi hiki cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika hakijawahi kuwa na ufanisi katika kulinda raia hapa, uwepo wake unafikiriwa umesaidia kudhibiti ukiukwaji unaofanywa na vikosi vya usalama.

Mapambazuko

Wengi wanaweka matumaini yao kwa serikali mpya ya mpito ya nusu-raia-nusu-jeshi ya nchi hiyo.

Iliingia madarakani baada ya maandamano ya watu wengi mtaani mnamo mwaka 2019 kumuangusha Rais wa zamani Omar al-Bashir baada ya miaka 30 ya utawala wa kidikteta.

Tangu wakati huo amefungwa kwa mashtaka ya ufisadi na anashtakiwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa kwa uhalifu wa kivita huko Darfur.

Faisal Mohammed Mohammed Salih
BBC
All individuals accused of any kind of crime in Darfur will be put on trial. No-one will be exempt from this"
Faisal Mohammed Mohammed Salih
Minister of Culture and Information
1px transparent line

Waziri wa Utamaduni na Habari wa Sudan, Faisal Mohammed Mohammed Salih, mwanaharakati wa zamani wa haki za raia aliyewahi kufungwa na serikali ya zamani, ni sehemu ya serikali mpya ya mpito.

Wakati anakubali kwamba kuna hofu na ya raia kutoliamini jeshi, anasisitiza kuwa dhuluma hazitavumiliwa tena.

"Watu wote wanaotuhumiwa kwa aina yoyote ya uhalifu huko Darfur watafunguliwa mashtaka. Hakuna mtu atakayesamehewa kutokana na hili," alisema.

Wafugaji wakiwa na punda mjini El Fasher, Darfur Kaskazini

Chini ya makubaliano ya amani tume ya ardhi pia inaundwa kusaidia watu ambao ardhi yao imechukuliwa wakati walipokuwa kwenye kambi, na pia kuangalia haki za wafugaji wahamaji.

Hatahivyo, kwenye kambi ya Abu Shouk karibu na Fasher, hatua kama hizo hazina maana kwa wale ambao wameona mapambazuko mengi ya uongo tangu mzozo ulipoanza mnamo mwaka 2003.

Labda ni ngumu zaidi kwa vijana, kama Abdullah mwenye umri wa miaka 14, ambao hawajui chochote isipokuwa makambi ya vita, njaa na makazi yao.

Ameketi kimya nje ya kibanda cha familia yake akichora maumbo kwenye mchanga kwa kutumia tawi, ingawa akili yake mahali pengine.

"Katika ndoto zangu nitakuwa na maisha bila vitisho, ambapo watu huenda salama na kurudi salama kwenye mashamba yao.

"Mahali ambapo ninaweza kuwa na maisha mazuri. Lakini naona ni ngumu kufikiria hili, kwa sababu itakuwa tofauti sana na yote niliyoyajua."