Pakistan kuwahasi wabakaji kwa kemikali

Women protest against sexual violence in Karachi, October 2020

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Maandamano dhidi ya ubakaji yamekuwa yakifanyika kote nchini Pakistan katika miezi ya hivi karibuni baada ya ubakai mbaya uliotokea mwezi Septemba.
Iliyochapishwa

Rais wa Pakistan amesaini sheria mpya itakayotoa adhabu kali dhidi ya wahusika wa ubakaji.

Kulingana na sheria hii , serikali itaweka sajili ya watu wanaopatikana na makosa ya ubakaji, kulinda utambulisho wa waathiriwa na matumizi ya kemikali kuwahasi baadhi ya wabakaji.

Kulingana na sheria hii, kesi za ubakaji zitaharakishwa. Mahakama zinatarajiwa kukamilisha kesi ya ubakaji ndani ya kipindi cha miezi minne.

Serikali imesaini sheria mpya dhidi ya ubakaji baada ya malalamiko megi ya watu dhidi ya unyanyasaji huo wa kingoni baada ya wanaume kadhaa kumbaka mwanamke mmoja nje ya jiji la Lahore.

Walimbaka mwanamke huyo kando ya barabara inayoelekea katika jiji hilo mbele ya watoto wake wawili. Mkuu wa polisi alisema kuwa muathiriwa kwa upande mmoja alikuwa na makosa.

Wanaharakati wakipinga utamaduni wa mauaji ya heshima Pakistan

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wanawake na watoto wa kike wamekuwa wakibakwa na kuuawa nchini Pakistan

Kauli yake pamoja na unyanyasaji huo wa kinyama viliwakasirisha watu nchini humo ambao walisema kuwa amegeuza ukatili huo kuwa kitu kidogo. Maandamano makubwa yamekuwa yakiendelea kuilazimisha serikali kuchukua hatua dhidi ya ubakaji.

Waziri Mkuu Imran Khan na baraza lake la mawaziri waliidhinisha sheria hiyo na Rais Arif Alvi akaisain kuwa sheria Jumanne.

Serikali ilipewa siku 120 na umma kuwa imeidhinisha sheria hiyo na kupitishwa na bunge.