Rais wa Peru Merino amejiuzulu baada ya waandamanaji kuuawa

Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri wa mpito wa Peru amejiuzulu baada ya watu wawili kufariki wakati wa maandamano dhidi ya serikali.
Manuel Merino, ambaye ni Spika wa zamani wa baraza la Congress, amekuwa mamlakani chini ya wiki moja.
Alichukua nafasi ya Rais Martín Vizcarra baada ya kuondolewa madarakani na bunge Jumatu kwa madai ya hongo, ambayo aliyakanusha .
Wanasiasa wa ngazi ya juu walikuwa wametoa wito wa kujiuzulu kwa Bw Merino kufuatia mashambulio dhidi ya waandamanaji waandamanaji dhidi yake.
Mawaziri kumi na wawili kutoka katika baraza lake alilokuwa amelichagua hivi karibuni alijiuzulu mapema siku ya Jumapili kupinga ukatili unaofanywa na polisi na namna rais anavyoshughulikia mzozo.
Maelfu ya waandamanaji -wengi wao wakiwa vijana-walishiriki katka maandamano yakumpinga Bw Vizcarra
Wailishitumu bunge la Congress nchini humo kwa kupanga mapinduzi ya bunge . Bw Vizcarra, mwenye umri wa miaka 57, amekuwa akipata uungaji mkono miongoni mwa wapiga kura walio wengi kwa majaribio yake ya kuleta mageuzi.
Maandamano ya Jumamosi mjini Lima yalikuwa ya amani kwa kiasi kikubwa lakini makabiliano yakaibuka majira ya jioni baina ya polisi na waandamanaji.

Chanzo cha picha, Getty Images
Polisi wana wanaripotiwa kufyatua gesi za kutoa machozi na risasi dhidi ya waandamanaji P, ambao baadhi yao walikuwa wkiwarushia mawe na vijinga vya moto.
Wanaume wawili mmoja mweye umri wa miaka 24 na mwingine mwenye umri wa miaka 25, waliuawa . Maafisa wa afya wanasema kuwa walikufa kutokana na risasi.
"Ninata nchi nzima itambue ninajiuzulu," Bw Merino alisema katika hotuba yake siku ya Jumapili.
Hofu ya kisiasa inaendelea kutanda huku Peru ikikabiliwa na mdororo wa uchumi uliosababishwa na janga la virusi vya corona.
peru ilitangaza moja ya vipindi vya mapema vya amri ya kukaa nyumbani -lockdown katika eneo la Amerika kusini ili kuzuwia kusambaa kwa virusi vya corona - lakini bado imekuwa ikishuhudia ongezeko la juu la haraka la idadi ya watu wanaoambukizwa corona.
Hadi sasa imeripoti kuwa watu 935,000 wameambukizwa maradhi hayo na wengine 35,000 wamekufa, kwa mujibu wa takwimu za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins University - na kulifanya taifa hilo kuwa na theluthi moja ya kiwango cha vifo kwa watu 100,000 duniani.
Bw Merino amekuwa amekuwa akitarajia kubaki mamlakani hadi mwezi Julai 2021- wakati muhula wa Bw Vizcarra ungemalizika.
Bw Vizcarra amekuwa katika malumbano makali na Congress, ambalo lina wabunge wengi kutoka vyama hasimu, tangu alipoingia madarakani Machi, 2018.
Alikanusha madai kuwa alikubali hongo ya thamani ya sole milioni 2.3 ($640,000; £487,000) alipokua gavana wa jimbo la kusini mwa Peru la Moquegua.













