Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi Tanzania 2020: Matukio katika picha Dodoma na Dar es Salaam
Zaidi ya watu milioni 29 wamejiandikisha kupiga kura nchini Tanzania.
Raia wa Tanzania wanachagua raisi, wabunge na madiwani.
Uchaguzi huu una wagombea 15 wanaowania nafasi ya urais na wawili kati yao ni wanawake.
Foleni ndefu za watu wakiwa wanasbiri kuupiga kura katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Mchakato wa upigaji kura ulianza saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi jioni saa za Afrika Mashariki.
Zoezi la upigaji kura ilichukua saa 10 ,zaidi vituo 85,000 katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania vilifungwa majira ya saa kumi jioni.
Wananchi wakiangalia majina yao kabla ya kupiga kura.
Wagombea wa upinzani walitoa tuhuma kuwa baadhi ya vituo kulikuwa kura feki.
Wagombea wakipiga kura
Rais John Magufuli akipiga kura jijini Dodoma , leo asubuhi.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Tundu Antiphas Lissu akipiga kura ya Uchaguzi Mkuu leo Oktoba 28, 2020, mchana, Ikungi, Mkoani Singida.
Hussein Mwinyi apiga kura yake Zanzibar
Hussein Mwinyi anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwaSeif Sharif Hamad wa chama cha ACT Wazalendo.