Uchaguzi Tanzania 2020: Watanzania waanza kushiriki katika zoezi la kupiga kura

Chanzo cha picha, AFP
Raia wa Tanzania wameanza kupiga kura katika uchaguzi mkuu huku kukiwa na ripoti za kuminywa kwa mtandao pamoja na kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani katika kisiwa cha Zanzibar.
Wapiga kura wana hadi mwendo wa saa kumi jioni kupiga kura.
Matokeo yanatarajiwa kutangazwa ndani ya juma moja .
Rais John Pombe magufuli ambaye chama chake cha mapinduzi CCM kimetawala Tanzania tangu uhuru 1961, anawania kwa muhula wa pili.
Mpinzani wake mkuu ni Tundu Lissu wa chama kikubwa cha upinzania Chadema , ambaye alinusurika mauaji miaka mitatu iliopita .
Alirudi kutoka Ubelgiji mwezi Julai ambapo alikuwa akifanyiwa matibabu ya majeraha ya risasi.
Takriban wagombea 15 wanawania urais akiwemo aliyekuwa waziri wa masuala ya kigeni Bernard Membe.
Mwadishi wa BBC Athuman Mtulya mjini Dar es salaam anasema kwamba Magufuli na Lissu wamevutia umati mkubwa katika kamepni zao.
Hatahivyo kampeni ya bwana Lissu iliahirishwa kwa siku saba baada ya kutuhumiwa kwa uchochezi na tume ya uchaguzi.
Aliripotiwa kusema kwamba bwana Magufuli alikuwa na mpango wa wizi wa kura , lakini tume hiyo ikasema kwamba hakuna jaribio kama hilo.

Chanzo cha picha, EPA/getty images













