Osiris-Rex: Nasa huenda ikapoteza sampuli kutoka sayari ndogo ya Asteroid

Iliyochapishwa

Chombo kilichotumwa na shirika la anga za juu la Marekani (NASA) kuchukua sampuli ya mchanga kwenye mwamba uliopo kwenye sayari ndogo( Asteroid) mamilioni ya kilomita kutoka ardhini kimepata sampuli nyingi za mawe hadi imeanza kuvuja na kumwagika.

Maafisa wanaendesha chombo hicho kwa jina Osiris-RexOsiris-Rex, kilichotua katika eneo la Bennu mapema, wanasema oparesheni ya huenda ilifanya kazi nzuri.

Picha zilizotumwa ardhini zinaonesha mwamba ulioegemea chombo hicho umesababisha mlango kufunguka na sasa lampuli hizo zimeanza kuvuja, Nasa imesema.

Nasa kwa saa inajaribu kuiweka salama.

"Sehemu ya sampuli iliyokusanywa kinaonekana kikimwagika kutika kwa chombo hicho," mkuu wa oparesheni hiyo Dante Lauretta amesema.

Chombi hicho kinaaminika kuchukua kama gramu 400 ya mchanga kutoka kwa mwamba, alisema.

Ameongeza kuwa chombo hicho kingelikusanya sampuli vyema zaidi. "Hofu yangu sasa ni kwamba sampuli hiyo itapotea kwasababu tumegeuka wahanga wa mafanikio yetu."

"Wakati wa kuokoa sampuli hiyo ni muhimu," Thomas Zurbuchen, Msimamizi mwenza wa Nasa wa sayansi, aliwaambia waandishi wa habari wakati shirika hilo la anga za mbali likijizatiti kuhakikisha sampuli zaidi haipotei.

Wahandisi walikuwa wametengeneza kifaa cha kutunza sampuli hizo ambacho kitawekwa kwenye chombo cha Osiris-Rex katika mkono wa roboti na kwenye eneo la juu la Bennu.

Chombo hicho sasa kitasimamishwa angani, kumaanisha itakuwa vigumu kubaini ni kuiwango gani cha sampuli kilichokusanywa.