Shimo jeusi angani linavyofanya kazi bila kujulikana

Chanzo cha picha, Lia Medeiros/Institute for Advanced Study/PA Wire
Mnamo Septemba 1964, Riger Penrose alikuwa ametoka kumtembelea rafiki yake.
Mwana anga wa Uingereza Ivor Robinson alikuwa amerejea England kutoka Dallas, Texas, alikoishi na kufanyakazi.
Kila wawili hao walipokutana hawakukosa kuzungumza lakini wakati huu gumzo lao halikuwa na mwisho.
Wawili hao walipokuwa wanatembea karibu na ofisi ya Penrose chuo cha Birkbeck London, wakasimama kidogo wakisubiri kupungua kwa msongamano wa magari.
Wakati huo, fikra za Penrose zilikuwa zimefika mbali, ilisafiri kipimo cha bilioni 2 cha mwendo wa mwanga kupitia ombwe la anga la mbali hadi mzunguko wa sayari.
Alifikiria kujikunyata kwa vyombo vya anga la mbali, kujikunjua kwa makundi ya nyota karibu na eneo katikati.
Na miaka 56 baadae, likamwezesha kushinda Tuzo ya Nobeli ya Fizikia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kama wavumbuzi wengi mfano Albert Einstein alivyotumia muda wake mwingi kufuatilia nadharia ya uwiano kwenye fizikia - Penrose alitumia miaka ya awali ya 1960 alifuata nyayo hizo.
Einstein alichapisha Nadharia yake kwa ujumla mwaka 1915, na kuleta mabadiliko katika sayansi' kuelezea uelewa wa anga la mbali, muda, mvutano, vitu vya kwenye anga la mbali na nishati.
Kufikia miaka ya 1950, Nadharia ya Einstein ilikuwa imefanikiwa kwa kiwango kikubwa lakini utabiri wake kwa kiasi kikubwa ulikuwa unachukuliwa kama usio na uhakika na uwezo wake wa kutokea ulikuwa chini.
Mahesabu yake yalionesha, kwa mfano, kwamba nadhari ya vitu kujikunja na kujikunjua husababisha uzito mkubwa kwenye eneo dogo kungesababisha hali ambayo hata mwanga haungeweza kujitokeza.
Na hayo yakafahamika kaa mashimo meusi.

Chanzo cha picha, PA Media
"Kwa kipindi kirefu kumekuwa na mashaka," anasema Penrose.
"Watu walitaraia kwamba kungekuwa kuna kitu ambacho kingeanguka na kuzunguka kwa namna isioeleweka na na kuanza kusonga tena nyuma."

Chanzo cha picha, Reuters
Miaka ya mwisho ya 1950, waangalizi kutoka nyanja ya wanaanga walikuja na mawazo mengine.
Walibaini vitu vingine vilivyoonekana vinavyong'aa, vilivyombali na vidogo.
Mara ya kwanza vilifahamika kama nyota - vilijitokeza kuonesha nguvu ya ajabu kwenye anga la mbali.
Ingawa ilionekana kutowezekana, kila uchunguzi mpya iliashiria kuwa nyota ilikuwa ni kundi la nyota za zamani zilizo kwenye mchakato wa kuanza kuachana na kuwa moja moja.
Huko Austin, Princeton, na Moscow, katika chuo cha Cambridge na Oxford, Afrika Kusini, New Zealand, India, na kwengineko, wanaanga walikuwa na wakati mgumu kupata ufafauzi wa nadharia inayoweza kuelezea uhalisia wa nyota.

Chanzo cha picha, ESO via EPA
Penrose, wakati huo akiwa msomi wachuo cha Birkbeck London, alichukua mwelekeo mwingine.
Alipendelea sana kutafuta suluhu, Alitumia muda mwingi Birkbeck akiwa na ubao na kuchoro michoro ya mikunjo kwa miundo yake mwenyewe.
Mwaka 1963, kundi la wanasayansi kutoka Urusi likiongozwa na Isaac Khalatnikov lilichapisha utafiti wao uliothibitisha kile ambacho wanasayansi wengi walikiamini.

Chanzo cha picha, Reuters
"Nilihisi kabisa kwamba njia wanazotumia hazitawawezesha kufikia hitisho la uhakika," anasema. "Kwangu niliona tatizo linatakiwa kutazamwa kwa ujumla hatua ambayo ilikosekana."
Wakati anakataa nadharia yao, hakuweza kutoa suluhu kwa tatizo hilo.
Nishati hiyo, mwenendo wake na kusinyaa kwa vitu vya anga la mbali kungesababisha joto kali kiasi kwamba miale ingelipuka katika kila urefu kila upande.
Jinsi ilivyokuwa ndogo na kusafiri kwa haraka, mng'ao wake ungeongezeka.
Ingefika wakati, mwanga, anga na muda vyote vingesimama na hatimae kutokea kwa shimo jeusi.












