Kwanini rais Donald Trump anataka Sudan kuwa na uhusiano mwema na Israel?

Chanzo cha picha, Getty Images
Sudan inapokabiliwa na hali ngumu ikiwa ni pamoja na kuzorota kwa uchumi, mfumuko wa bei unaobisha hodi na ukosefu wa chakula kote nchini, utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump pamoja na serikali ya Israeli zimepata fursa.
Matumaini ya demokrasia ya nchi hiyo yalipatikana baada ya mandamano ya amani yaliyodumu miezi 18 ambayo yalimuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir.
Lakini ikiwa Sudan itashirikiana na Israel basi Marekani itaiondoa katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi na kufungua milango itakayoimarisha hali ya uchumi.
Ni hadithi ndefu ambayo imedumu miaka 30 iliyopita siku za mwanzo za utawala wa Kiislam wa Sudan.
Baaada ya kuingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989, Rais Bashir aligeuza Khartoum kuwa kituo cha kimataifa cha wanamgambo wa kijihadi.
Al-Qaeda na makundi mengine yaliyo na misimamo mikali yalitumia Sudan Kama kambi ya kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani, Saudi Arabia, Misri, Ethiopia, Uganda, Kenya na kwengineko.
Baada ya shambulio la kwanza dhidi ya kituo cha kibiashara mjini New York mwaka 1993, Marekani ilitangaza Sudan kuwa nchi inayofadhili ugaidi.
Ushirikiano wa CIA
Vikwazo vya kimataifa vya uchumi, shinikizo kutoka kwa nchi jirani ambazo zilikuwa zinaunga mkono waasi nchini humo ziliifanya Sudan kumfukuza Osama bin Laden na wanajihadi wengine miaka mitatu baadae.
Muda mfupi baada ya shambulio la kigaidi la Septemba 11 mwaka 2001, huduma za usalama za Sudan zilitambuliwa kama mshirika na shirika la kijasusi la Marekani (CIA).
Kutokana na ushirika huo, Sudan ingelikuwa imeondolewa katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi.

Chanzo cha picha, AFP
Lakini wanachama wa congress walichukizwa na Khartoum kutokana na sababu kadhaa, miongoni mwazo vita vya Darfur na ukiukwaji wa haki za binadamu, hali iliyofanya iendelee kusalila katika orodha hiyo.
Na serikali ya Bashir iliendelea kufanya kazi kinyemela na makundi yenye misimamo mikali: kwa kudumisha ushirikiano wake na Iran na Hamas, na katika matukio mawili ambapo ndege za kivita za Israeli zilishmabulia msafara wa Sudan uliokuwa ukielekea pwani ya bahari nyekundu, kwa madai ya kuwapelekea silaha wanamgambo wa Hamas.
Mwaka 2016, kutokana na shinikizo kutoka kwa Saudi Arabia na Falme za Milki za Kiarabu, serikali ya Bashir ilivunja uhusiano na Iran.
Baada ya mapiduzi ya kidemokrasia ya mwaka jana, Washington DC bado inajivuta kuhusu msimamo wake dhidi ya Sudan.
Maafisa wa wizara ya mambo ya nje nchini Marekani walitaka kudumisha vikwazo kama silaha kali ili waendelee kuwa na ushawishi. Na pia walikua na hofu kwamba huenda utawala wa kidemokrasia hautadumu kwa muda mrefu.
Maseneta wapinga kuondolewa kwa orodha ya ugaidi
Tatizo ni kwamba kuendelea kuiwekea vikwazo Sudan huenda ni hatua itakayopelekea nchi hiyo kusambaratika.

Alimradi Sudan itaendelea kuwa katika orodha hiyo, vikwazo vya kiuchumi dhidi yake vitaendelea kutekelezwa.
Biashara halali ya Sudan zimelemazwa, uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja umedorora na mashirika ya kimataifa ya kifedha kama vile IMF na Benki ya dunia hayawezi kuifutia deni kubwa la - dola bilioni 72 ambalo linaendelea kuongezeka.

Chanzo cha picha, EPA
Kiwango cha njaa kinachokabili Sudan kinaogopesha: ''Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu milioni 9.6 wanakabiliwa na baa la njaa''
Hali hiyo imechangiwa zaidi na janga la Covid-19 na mafuriko. Ni mzozo ambao hauwezi kutatuliwa kupitia msaada wa chakula - kinachotakikana ni msaada wa kufufua uchumi.
Katika miezi ya hivi karibuni, mpango wa kuiondoa Sudan katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi uliowasilishwa mbele ya bunge la Congress, ulikwama kutokana na matakwa ya jamaa za waathiriwa wa mashambulizi ya al-Qaeda Africa Mashariki na Yemen kwamba walipwe fidia.
Sudan ilikubali kulipa dola milioni 335. Lakini mwezi wa Septemba maseneta wawili wa chama cha Democratic - Chuck Schumer na Bob Mendez walipinga hatua hiyo, ili kutoa nafasi kwa familia ya wahanga wa mashambulio ya 9/11 endapo wataamua kuwasilisha kesi
Utawala wa Trump umetoa ofa kwa Sudan kuhusu jinsi itakavyojinasua kwenye mtego huo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Akizuru mjini Khartoum mwisho wa mwezi Augosti, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alipendekezea Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok: kwamba ikiwa Sudan itaitambua Israel, Rais Trump huenda akatafuta ufumbuzi wa mkwamo wa hali yao katika bunge la nchi hiyo.
Kufuatia uamuzi wa UAE wa mwezi uliopita, Sudan ambayo ni mwanachama wa Muungano wa nchi za kiarabu, itakuwa nchi ya nne ya Kiarabu kufanya hivyo.
Hatua hiyo huenda ikaimarisha kampeni ya utawala huo kufanya rasmi uhusiano wa nchi za Kiarabu na Israel wiki tatu kabla ya uchaguzi.
Kutambua Israel kutakuwa hatua muhimu wa Sudan - Na hilo ndilo lengo lao.
Mkataba mzuri kwa majenerali
Wanaopinga mkataba huo ni wanambo wa kiislam ambao sasa hawako madarakani. Lakini ni suala tata ambalo huenda ukazua mzozo wa kisiasa kwasababu baadhi ya viongozi wa muungano wa kiraia wanasisitiza kufikiwa kwa amani na Wapalestina kwanza.
Bw. Hamdok anafahamu kwamba muungano wa kiraia unaomuungamkono utavunjika akiamua suala hilo yeye binafsi.
Alimwambia Bw. Pompeo kwamba uamuzi kuhusu pendekeza lake utasubiri hadi serikali itakayoingia madarakani kupitia uchaguzi kubuni miaka mitatu ijayo.
Japo Bw. Hamdok yuko ofisini na baraza lake la mawaziri wa kiraia, ni majenerali wa Sudan ndio walio na mamlaka halisi.
Wakiungwa mkono na UAE, Saudi Arabia na Misri, mwenyekiti wa baraza la mpito, Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagolo, anayefahamika kama "Hemeti", wanaosimamia majeshi na fedha.
Ni hao majenerali ndio wanaoshughulika na Israel. Jenerali Burhan alikutana na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu mwezi Februari - bila kumfahamisha Bw. Hamdok - na wawili hao wanatarajiwa kukutana tena hivi karibuni.
Kwa Jenerali Burhan na Jenerali Hemeti, mkataba wa Marekani na Israel utawahakikishia kutambuliwa kimataifa wanaotafuta bila kupitia mchakato wa kidemokrasia.
Hiyo ndiyo sababu wanademokrasia wa Sudan wanataka uchunguzwe kwa makini.
Wakati wa maandamano ya mwezi Aprili yaliyomtoa Bashir madarakani, Jenerali Burhan na Jenerali Hemeti walichukuwa nafasi yake. Miezi miwili baadaye vikosi vyao viliwaua zaidi ya waandamanaji 100.
Hatua hiyo ilizua malalamiko makubwa hadi mkataba ulipofikiwa kati ya Marekani, Uingereza, Saudi Arabia na UAE, wakakubali kugawana madaraka na baraja la kirai la mawaziri.

Chanzo cha picha, Getty Images
'Masuala tofauti'
Ukweli ni kwamba majeshi yanavumilia viongozi wa kiraia kwasababu wanahitaji kutambuliwa na kuheshimiwa kimataifa. Watu wa Sudan hawajawasamehe majenerali hao kutokana na ukatili wao dhidi ya raia.
Wayahudi wa Israel na wale wa Ethiopias:
Lakini kwa vijana wa Kiisrael na washirika wao wa Marekani wanaopinga mauaji ya Darfur ya miaka 15 iliyopita, kuwahalalisha watu waliowaongoza wanamgambo waliotekeleza mauaji ya kikatili ni hatua ya kushangaza
Msimamo wa Bw. Hamdok kimantiki: Kuiondoa nchi katika orodha ya ugaidi na kuitambua Israel ni masuala mawili tofauti.
Anahoji kuwa Sudan inastahili kuondolewa katika orodha ya ugaidi, kwasababu imeondoa magaidi kutoka kwa ardhi yake na kwamba kuna haja ya kuokoa demokrasia yake.
Na ikiwa Israel itatambuliwa na nchi ya kiarabu iliyo na idemokrasia halisi itakuwa zawadi bora zaidi kujishindia.












