Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Zitto, watu wengine wanne wapata ajali ya gari Kigoma
Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-wazalendo, Zitto Kabwe na wenzake wanne wamepata ajali, huko jimboni Kigoma Kusini, Wilaya ya Uvinza, mjini Kigoma, Magharibi mwa Tanzania.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa bara, Joran Bashange, ajali hiyo imetokea akiwa kwenye shughuli za kampeni, akitoka katika eneo la kata ya Kalya kuelekea Lukoma.
''Gari lake liligongwa nyuma kisha likapoteza uelekeo na kupinduka zaidi ya mara mbili.''
Imeelezwa kuwa gari lake lilikuwa na abiria watano ambao wote wako salama, lakini wamepata maumivu na majeraha.
''Wamekwishapata huduma ya kwanza, na chama kimechukua hatua za kukodisha ndege kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Akizungumza na BBC, Afisa habari wa chama hicho Arodia Peter amesema bado chama hakijapata taarifa rasmi kama Zitto ameshawasili Dar es Salaam.