Jinsi mwanafunzi alivyoanza kuuza 'notes' zake... na kupata mamilioni ya fedha

Eugene Cheow during a diving trip to Mexico's Cozumel island, 2019

Chanzo cha picha, Eugene Cheow

Maelezo ya picha, Eugene Cheow ni mwanafunzi wa masomo ya biashara
Iliyochapishwa

Eugene Cheow akiwa anatabasamu anasema, ni sawa na utani: " Ninaweza kuweka mtaala wote katika ramani ya akili yangu."

"Ninapiga mbizi pia na nnapenda kupata kahawa ya bure katika katika kituo cha biashara duniani," alieleza.

Hii ndio namna Cheow, mwenye miaka 24-mfanyabiashara mwanafunzi katika chuo kikuuu cha Singapore, alivyoeleza kwa ufupi kuhusu maisha yake wakati alipopigiwa simu kupitia Zoom.

Alizungumzia kuhusu masomo yake, biashara na kila kitu pamoja na ustadi wa historia ya maisha yake, ,kutoka maeneo ya maji kusini mwa Asia mpaka mjini Mexico.

An example of mind map by Eugene Cheow

Chanzo cha picha, Eugene Cheow

Maelezo ya picha, Cheow anasema ramani yake ya akili inasaidia wanafunzi kujifunza kwa haraka

Lakini nini sababu ya Cheow kujulikana kidogo.

Hivi karibuni , baada ya kufaulu mtihani wake mara mbili huko Singapore kwa matokeo ya kushangaza, Cheow aliamua kuweka 'notes' zake zote - ambazo aliziita ramani ya akili(minds of maps), na kuziuza mtandaoni.

Cheow hakuwa wa kwanza kujaribu kujipatia fedha kutokana na mafanikio , lakini yeye ameweza kuuza nyenzo zake za kusomea bila kutarajia.

Mpaka leo ameuza 'ramani ya akili' yake zipatazo 1,500 na kupata zaidi ya dola $1,000 kwa wiki- na kuamua kutumia daftari zake za kujisomea kuwa biashara.

Mahitaji yakawa mengi

Visitors take in the view from the aerial walkway of the Garden by the Bay's Supertree Grove in Singapore, 2017

Chanzo cha picha, Getty Images

Ili kuwa muuzaji wa nyumba Singapore, lazima mtu awe amehudhuria mafunzo ya saa 60-na kufalu mitihani yake ya awamu mbili.

Sio mchakato rahisi, kwa kuwa Singapore ina sheria ngumu kuzifuata, Cheow aliiambia BBC. "Niligundua kuwa kuna uhitaji mkubwa ya kuwa na njia rahisi ya kujifunza."

Kwa upande wa ada, mtumiaji anaweza kupekua nakala 16 za "mind maps" ambazo zilimsaidia Cheow kufaulu mitihani yake.

Ramani za akili ni njia za kielelezo ya kuwakilisha dhana na mawazo, ili kuufanya ubongo kuelewa kwa urahisi.

Akili ya Cheow katika ramani yake imejumuisha masuala ya kisheria, masomo ya biashara na masoko, fomula za hesabu na muundo wa mtaala.

"Ramani inaweza kumsaidia mtu kujifunza. Inatoa mtazamo wa somo lolote, lakini unaweza kuangalia kwa karibu katika kila kipengele," Cheow anaeleza.

"Na kama una swali kuhusu somo fulani, unaweza kutafuta taarifa katika ramani hiyo ya akili, badala ya kusoma daftari zima ili kupata jibu la swali lako."

"Ni namna nyingine ya kujifunza kiurahisi.

'Lugha si muhimu'

Eugene Cheow diving in a cenote (a natural sinkhole) in Mexico's Cozumel island

Chanzo cha picha, Eugene Cheow

Maelezo ya picha, Cheow anasema kazi yake ya kupiga mbizi imemfundisha kuwa mawasiliano si lazima uwe unatumia lugha fulani

Cheow amesema ujuzi wake wa kufundisha bila mawasiliano ya kuongea ni kitu ambacho anakipenda kwa muda mrefu na amejifunza wakati wa kupiga mbizi.

Amekuwa akizamia maji tangu akiwana miaka 14 na miaka tatu iliyopita, baada ya kuwa mwalimu wa kupiga mbizi, - alikuwa akichukua makundi ya watu kutembelea baharini ili kuona uzuri wa majini nchini Philippines, Indonesia, na Malaysia.

"Kama mwalimu wa kufundisha watu jinsi ya kuzamia majini, nimegudua kuwa lugha huwa ni kitu ambacho sio muhimu kabisa katika mawasiliano," alisema.

"Huwezi kuongea ukiwa kwenye maji, huwezi kusema hata habari, au barakoa yangu inavuja, kila kitu ni kwa lugha ya ishara peke yake."

Cheow amesema kupiga mbizi kunampa sifa mbili za ziada: kwanza, uwezo wa kuunganisha watu kutoka tamaduni mbalimbali duniani.

Suala la pili ni kupata burudani mpya "haswa kwa kijana kama mimi ambaye nimelelewa na kupata elimu kidogo".

Kuunganisha watu

Eugene Cheow representing Singapore at his Puebla university's International Day

Chanzo cha picha, Eugene Cheow

Maelezo ya picha, Eugene Cheow anasema anafurahiakuunganisha watu

Cheow anapenda kusimulia taarifa ya namna alivyofikia kwenye kupata kahawa kidogo katika kituo cha biashara duniani.

Kwa mwanafunzi wa masomo ya biashara anasema kutembelea kituo cha biashara duniani WTC ni kitu kikubwa sana kwake na alikuwa anakitamani sana".

Mwaka jana, Cheow alikuwa mwanafunzi wa Mexico kwa muda katika mji wa Puebla, kusini mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo.

Aliuelezea mji huo kuwa unavutia na kupendeza na una mazingira rafiki sana.

'Kuhesabu mafanikio'

Eugene Cheow pictured in front of Universidad de las Américas Puebla (UDLAP) wrapped in the Singapore flag

Chanzo cha picha, Eugene Cheow

Maelezo ya picha, Cheow anasema hana malengo ya kuwa dalali wa majengo licha ya kufaulu mitihani yake

Kampuni ya Cheow, 'RES Tutor', ni moja ya biashara ambayo inasaidia watumiaji kusoma kwa ajili ya kufanya mitihani na kuwa madalali wa kuuza majengo Singapore.

Anasema amejikita katika kupanua biashara yake ya soko la mtandaoni lakini wakati huo huo amesema anataka kutumia mafanikio kwa kupima ili kuhakikisha kuwa mbinu ya biashara yake inafanya kazi".