Kwanini wanawake wanabadili majina yao ya mwisho na kutumia ya waume zao?

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika kupanga harusi, suala la mke kuchukua jina la mume wake limekuepo kwa kizazi na kizazi. Ni utamaduni ambao umekuwa bado ukiendelea katika nchi mbalimbali duniani.
"Inashangaza sana, kwani utamaduni huu unatokana na historia ya mfumo dume, kuanzia kwenye wazo la kwamba mwanamke aliyeolewa anakua mali ya mume,"anasema Simon Duncan, profesa kutoka chuo kikuu cha Bradford, wa nchini Uingereza ambaye amekuwa akifanya uchunguzi kuhusu utamaduni huu anaeleza.
Imekuwa tamaduni ambayo inatumika sana na waingereza ingawa wazo la kumiliki mke kama mali limekuwa halipo, na suala la kuasili jina la mume kisheria limekuwa halipo.
Hata nchini Norway, taifa ambalo linaongoza kwa usawa wa jinsia na lenye historia kidogo ya mfumo dume,bado wanawake wengi wanatumia majina ya waume zao.
Utamaduni wa mfume dume
Kuna sababu kadha wa kadha zinazoeleza sababu ya kwanini wanawake wanaweza kubadili majina yao .

Chanzo cha picha, Getty Images
Sababu ya kwanza ni suala la kuwa na familia nzuri , inaaminika kuwa kutumia jina la mpenzi wako inaonyesha ishara ya kujitolea na kuunganisha familia kuwa kitu kimoja.
Baadhi ya wapenzi au wanandoa wanakubali kubadili jina kwa sababu ni utamaduni , kuwa na jina la mume wako.
Kubadili kwa jina la pili kunahusianishwa na utamaduni mwingine wa kutaka kuoa.
"Ni sehemu ya mapenzi," alisema Corinna Hirsh, mwenye miaka 32-kutoka Ujerumani, ambaye alibadili jina lake na kuchukua la mume wake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Suala lingine ambalo mtafiti ameweza kulibaini ni namna ya kuonesha kuwa na umoja na kujitoa kwa dhati.
"Nahisi jina linatoa utambulisho wa familia zaidi ya mtu mmoja mmoja," Lindsey Evans kutoka California ameeleza.
Wanawake wengi uamua kutumia jina la mume wake kuwa jina lake la mwisho ili kuonesha umoja katika familia.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Nilitaka kufanya hivyo ili kurahisisha mahusiano yangu na mwanangu na sio kwenye karatasi tu," alisema Jamie Berg wenye miakaa 36-mkazi wa Norway.
Alidai kuwa alikuwa hataki kumchanganya mwanae, kuhoji ni nani anatengeza familia,anadhani jina linaweza kumchanganya mtoto.

Chanzo cha picha, Getty Images
Aidha wasomi wametofautiana katika kuangalia namna sheria inavyofanya kazi ili kufanikiwa na jitihada za usawa wa jinsia.
Duncan ameeleza kuwa ni hatari sana kama wanandoa watabadilisha jina kwa sababu ya utamaduni pekee.
"Inaonesha kuwa mume ndio mwenye mamlaka….utamaduni wa kuwa mume ndio kichwa cha familia, ameeleza mtafiti.
Madai hayo yameungwa mkono na wanawake kama Nikki Hesford, 34,ambaye ni mfanyabiashara huko kaskazini mwa England.
Yeye ameachana na mume wake lakini alikataa kuacha kutumia jina la aliyekwa mume wake na anashangaa kwanini baadhi ya wanawake wakiachana na waume zao wanaacha kutumia majina hayo.
Baadhi ya wanawake wanadhani kutumia majina ya waume zao hakusaidii harakati ya wanawake

Chanzo cha picha, Getty Images
"Wanawake huwa wanalalamika kuwa wanaishia kuwa walezi wa watoto nyumbani, kwa wale ambao wanaacha kazi zao wakati mtoto anapougua, au wale ambao wanahangaika na ajira zao", Hilda Burke anasema.
"Mpenzi wangu hajawahi kuniambia kubadili jina langu la mwisho, nadhani ninaweza kufanya maamuzi ambayo yatanipendeza zaidi, " anasema Evans.
Wanawake wengi wa Afrika au Marekani ni ngumu sana kubaki na jina la mume baada ya kuachana.













